- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwa na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa dereva mmoja alimsaidia mwenzake ambaye gari lake lilipata hitilafu ya tairi moja. Katika video hiyo, dereva huyo anatajwa kuwa shujaa kutokana na hatua yake ya kumsaidia mwenzake.
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwapo na kipande cha video kinachosambaa kikionesha kitendo cha kustaajabisha ambapo gari moja la mizigo lilipata hitilafu na baad ya muda likaja gari linine la mizigo lilitoa msaada kama inavyoonekana kwenye video.
Video hiyo imeibua maswali mengi juu ya uhalisia wa video hiyo, iwapo ni ya kweli ama imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde (AI))?
Uhalisia wa video hiyo
Ufauatiliaji wa kina wa JamiiCheck kupitia nyenzo za kididgitali umebaini kuwa video hiyo imehariririwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde.
Video hiyo inaonekana kuwa na baadhi ya dosari ikiwemo kubadilika kwa baadhi ya vitu katika hali isiyo ya kawaida;
Mathalani rejelea lori lilikuwa limebeba kasha (Container) awali lilikuwa na alama ya kampuni ya CAT (Caterpillar's supply chain arm na baada ya muda kidogo likawa halina alama na kisha baadae likaonekana tena kuwa na alama ya kampuni ya ONE (Ocean Network Express)
Aidha kwa kutumia nyenzo za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya AI imebainisha kuwa video hiyo ina viashiria vya AI kwa takribani 99%.
Lakini Je, tukio halisi lilitokea?
Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa video hiyo ilihaririwa kutoka katika video halisi iliyosambaa hapo awali mtandaoni.
Tukio halisi lilitokea katika barabara ya Al-Mahalla, Misri ambapo dereva wa Lori lilitoa msaada anaitwa Imad Jalal. Imad anaeleza alitoa saada huo na kufanikiwa kulisogezza gari hilo hadi takribani mita 500 mbele hadi lilipoweza kusimama tena. Soma pia hapa na hapa.
Gari lililosaidiwa lilikuwa limebeba mzigo wa pamba, na kilichopasuka hayakuwa matairi kama watu wengi walivyodhani bali ni "sunspession".