Tundu Lissu ataka Rais Magufuli asusiwe kila mahali na mataifa mengine duniani

LISSU.jpg


Ila nashauri wajiangalie. Kule kwetu kuna mengi hayana majibu. Wangemaliza haya ingesaidia sana kujua tunapelekwa wapi 2020.

CCM inatupumbaza kwa kutumia wapumbavu. Na wapo wanafanyakazi.

======
Dar es Salaam.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), Tundu Lissu amesema Ukawa wanatangaza vita na CUF ya Profesa Ibrahim Lipumba kama walivyo vitani na CCM ya Rais John Magufuli.

Lissu ameyasema hayo leo (Jumatatu Julai 17) wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho.

Lissu amesema Profesa Lipumba amewasaliti kwa kuwa yeye ndiye aliyempitisha Lowassa (Edward) kuwa mgombea wa uraisi kwa tiketi ya Ukawa.

"CUF ya Lipumba ilitusaliti kama Yuda Iskariot alivyomsaliti Yesu,"amesema Lissu.

Pia Lissu amelishauri jeshi la polisi kuacha kupambana na upinzani na badala yake wakapambane na wahalifu wanaofanya mauaji Kibiti.

Chanzo: Mwananchi
 
Mie nadhani chadema wanamcoach huyu Tindu agombee nafasi ya urais..

Mnamuona mwenzenu anabwabwaja, hamjui ni strategy ya kujikuza jina ili 2020 agombee and na kuzuia Chadema isipotee hewani, manake reputation ya chama imeshuka recently.
Tundu lissu ni zaidi ya mwanaume. Nani anathubutu kufungua mdomo kwenye huu utawala huko CCM? Wote mmefanywa kama makondoo.rais anavunja katiba waziwazi anavunja taratibu za manunuzi ,ubinafsi , kuuwa upinzani. Lissu kamweleza waziwazi kama atachukia anywe sumu.
 
"CUF ya Lipumba ilitusaliti kama Yuda Iskariot alivyomsaliti Yesu,"amesema Lissu.

Mara keshasahau yeye na CHADEMA yake walivyowasaliti mamilioni ya Watanzania kwa kumkumbatia fisadi?

Tena fisadi ambaye waliwaaminisha Watanzania kwa miaka nenda rudi kuwa ndo fisadi mkuu...

Aende zake naye huyu...tushaanza kuzichoka tararira zake.
 
waalimu hatujapata ajira na yeye alikua mwalimu nyongeza za mishahara hakuna kodi kila mahali maisha magumu ivii anenda kujenga uwanja chato wakati wa dar tu wenyewe haujakamilika.. ni nini anafanya huyu baba na serikali yake ya mabavu..
Bora kama walimu mmeanza kuliona hilo.nasikia na watumishi wa serikali wameambiwa mshahara ni huo huo hakuna nyongeza wala chochote asiyetaka aache kazi.poleni sana. Michango ya mwenge mmeshalipia?
 
Nimeisikiliza clip mwanzo mpaka mwisho na binafsi sioni jipya zaidi ya kuwa malalamiko haya ni kama yamerasimishwa kuliko ilivyokuwa mwanzoni ambapo yalikuwa yakiongelewa chinichini.
Naamini Mheshimiwa Raisi ana sababu za kufanya yote aliyoyafanya pia serikali ina majibu kwa hoja za Lissu kwa hivyo ni bora tusubiri response ya serikali kwa haya aliyoyataamka TL.
Jambo moja ni dhahiri,Lissu kajilipua.Amejiamini kitu gani,SIJUI!!
Magufuli hataweza kujibu tuhuma hizi mkuu , hii si mchezo ! Kumkamata Lissu pia haitawezekana , maana itabidi apelekwe mahakamani , swali ni nani ataweza kukanusha tuhuma hizi mahakamani ?
 
Back
Top Bottom