VIDEO: Prof. Lipumba akiri kumsaidia Rais Kikwete katika Uchaguzi 2010

Wakuu,

Katika zunguka zangu nikitafuta video ya kinachodaiwa kunaswa na Tanzania Daima (Ref Lipumba akiri kumsaidia Kikwete Uchaguzi 2010), nimefanikiwa kuipata video hii katika YouTube. Nimetafuta Part 2 ya Video hii sijaipata, nawashirikisha Part 1 yake ili tunapojadili mambo kama haya tusiuziwe mbuzi katika gunia.

Kinachoshangaza, tumefikia hatua hii kama nchi? Ndizo siasa zilizo nyuma ya pazia na wananchi tumefumbwa macho?

Video yenyewe hii hapa:

Sasa hapa CUF nayo ina jiita ni chama cha upinzani?
 
Last edited by a moderator:
Tendwa yuko wapi? kama kweli anaipenda hii nchi anatakiwa atoe tamko dhidi ya CUF. Sidhani kama Lipumba aliitwa kwenye ule msikiti kama individual, na hata kama ni ivyo,aliambiwa kabisa kuwa theme ya mazungumzo yake iwe hali ya siasa nchini, which means alikua anaongea sio kama individual, but kama mwenyekiti wa chama anavyoona siasa za nchi hii. kwanini Tendwa asi act on that? au kwakua CCM imetajwa kama beneficiary wa udini wa mwaka 2010?
 
Hii inaitwa Liwalo na Liwe....wanasiasa wengi wanajitahidi kumtuhumu Jakaya Kikwete katika suala la udini kwenye kampeni...lakini mambo haya yameonekana kuwahusisha nao moja kwa moja....
Tujisahihishe kama Taifa katika suala hili la udini.......!
 
kwa hiyo huyu bwana alikubali kumsaidia kikwete ili ashinde kwa kuwa kikwete ni muislam mwenzie? kwa jinsi hii huyu bwana pamoja na kikwete wake wote hawafai kuwa viongozi kwa maslahi ya wananchi wote; kumbe kwao uislamu kwanza taifa baadae...HAWAFAI KWA MUSTAKABALI WA TAIFA HILI...takbirrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr..............
 
my observation and lesson meant from the video
1. Lipumba yupo kwa ajili ya maslahi ya dini yake na siyo maslahi ya watanzania wote
2. Lipumba ni adui no. 1 wa wakristo kwani hata pale alipoona ameshindwa ilibidi wachakachue matokeo ili mwilislamu mwenzake JK atangazwe mshindi. Ina maana JK hakushinda uchaguzi.
3. Lipumba anataka sasa kutumia dai la waslamu kuhusu mahakama ya kadhi, na geographia ya waslamu walio wengi ambao ndo wapo ukanda wa pwani, ili waslamu wamchague this time kwani JK hakuweza kufanya vizuri yale waliyokua wamekubaliana
3. Lipumba anajarinu kutumia matatizo ya waslamu ambayo siyo tofauti na ya wakristo, na kujifanya yeye ndiye mkombozi wa hayo matatizo na hiyo wafanye juhudi wamweke madaraka hata kwa kuchakachua kama walivyofanya kwa JK
4.Lipumba anajaribu kupandisha joto la waslahimu kwa kuwadanganya kuwa eti upande wa wakriso wamejiandaa, bila kutoa ushahidi wamejiandaa vipi
5. Lipumba amedhihirisha yeye yupo kwa ajili ya kutetea imani yake na waislamu zaidi, na kukosa kabsa utaifa
6. Lipumba amedhihirisha bila shaka yeyote kuwa CUF ni chama cha Waislamu na kipo kwa ajili ya maslahi ya waislamu, ndo maana hata kampeni zake huwa zinaishia ukanda wa pwani
7.Lipumba ameendelea kudhihirisha ya kuwa JK ni mdini, na walikua na deal ya udini na yeye
 
Serikali ya ccm ilimkamata LWAKATARE kwa eti alipanga ugaidi,lakini mchana kweupe mr Lipumba amehamasisha waumini pale msikitini Dar wasichague mtu wa dini nyingine.Huyu ni mtaalamu aliyebobea eti kwenye uchumi,polisiccm kama hawaoni huu ni ugaidi basi wasubiri kuona mengi b4 2015.CUF kama huyu ndie mwenyekiti wao basi hiki chama hakina uhalali wa kuwepo kisheria,Lipumba inabidi ahamie SOMALIA au sudan kwa AFRICA NDIZO NCHI ZINAZOONGOZWA kwa mfumo na uelekezi wa imani yake.Wana CUF inabini chama kitoe tamko au ndio mwisho wa ushirika wenu na ccm.Sasa tumeona kwa nini wabunge wa CUF ni mabubu bungeni wanaamini kuwa ipo siku Tanzania inaongozwa kwa misingi ya dini moja tu.Mungu ibariki tanzania na tuepushe na viongozi kama akina LIPUMBA.
cc to ritz,zemaclopolo,zombi na wenzenu wote.
 
Haya jamani Prof. Lipumba kasha fungua kampeni rasmi ya kuja kuwa raisi wa Waislamu Tanzania. Maana mtu anagombea uraisi lakini anazungumzia maslahi ya dini moja. Halafu kuna watu wanajiuliza kwa nini CUF ilionekana kuwa chama cha kiislamu? Sikilizeni hotuba hiyo ya mwenyekiti taifa.

Cha kujiuliza hapa ni je baada ya hotuba hii bado ana tegemea kupigiwa kura na Watanzania wote? Je bado ana amini Wakristo watamuamini kuwa atakua mtetezi wao akija kuwa raisi? Je ana amini anaweza shinda bila kura za Wakristo? Je hakujua hotuba hii inarekodiwa na itaonekana na wote?

Thank God for technology walau leo tumejua kwa nini Ibrahim Haruna Lipumba amekua akiusaka uraisi kwa udi na uvumba. Nyerere alisha tuonya kwamba yoyote anaekimbilia ikulu basi ana yake na wala si maslahi ya taifa. Asante sana mh. Ibrahimu Lipumba, raisi mtarajiwa wa Jamhuri ya Waislamu Tanzania 2015.
 
Lipumba inabidi akamatwe na polisi maana huyu ndiye gaidi no 1 ni mchochezi na hata fujo za wana mtwara nina wasiwasi yeye ni muhusika mkuu kama kuna usalama wa taifa sasa ni muda muafaka kuwaeleza polsi wamkamate mchochezi mkubwa huyu.
 
nashauri zitengenezwe CD za kutosha kusambaza makanisa yote nchi ili na wajue sera za CUF kuelekea uchaguzi mkuu 2015 ambazo zimetangazwa na mwanyekiti wake lipumba
 
Wakuu,

Katika zunguka zangu nikitafuta video ya kinachodaiwa kunaswa na Tanzania Daima (Ref Lipumba akiri kumsaidia Kikwete Uchaguzi 2010), nimefanikiwa kuipata video hii katika YouTube. Nimetafuta Part 2 ya Video hii sijaipata, nawashirikisha Part 1 yake ili tunapojadili mambo kama haya tusiuziwe mbuzi katika gunia.

Kinachoshangaza, tumefikia hatua hii kama nchi? Ndizo siasa zilizo nyuma ya pazia na wananchi tumefumbwa macho?

Video yenyewe hii hapa:

umesikiliza alichoongea Sita leo kanisani, kuwaponda viongozi wengine kwamba,hawafai kuchaguliwa kuwa maraisi wa nchi hii isipokuwa yeye na watu wengine wanne. hayo ameyaongelea kanisani. hivyo kuongea siasa kanisani inaruhusiwa lakini misikitini hairuhusiwi. nchi hii lazima ama waislam au wakristo kama noma na iwe noma
 
Last edited by a moderator:
Semeni hii ni mere hypothesis -- lakini mtu huwezi kukosea sana ukisema ingelikuwa ni Dr Slaa au Mbowe ndiyo alitamka kanisani kuhusu Ukristo na CCM kama alivyofanya Prof Lipumba kule msikitini (kuhusu Uisilam na CCM) saa hizi hao viongozi wawili wa CDM wangekuwa wameshakamtwa kwa uchochezi na kufunguliwa mashitaka.

Hypothesis hii naweza pia kuisemea Mtwara na matukio yake ya hivi karibuni. Ingekuwa ni Moshi au Arusha ndiyo yametokea kama ya Mtwara -- saa hizi Lema, Mbowe, Nassari nk wangekuwa tayari wana kesi ya uchochezi mahakamani.

Nchi hii haina haki hata kidogo na ndiyo maana amani inalegalega sana!
 
Kutokana na jinsi magamba walivyo na usongo na viongozi wa CDM kuwavizia wafanye kosa, hiyo hypothesis yako ni very plausible. Kuna mengi ya Chadema serikali ya CCM inayaangalia chini ya darubini kali kuliko ya vyama vingine vya upinzani. Hii kila mtu anajua. Hujakosea sana.
 
Semeni hii ni mere hypothesis -- lakini mtu huwezi kukosea sana ukisema ingelikuwa ni Dr Slaa au Mbowe ndiyo alitamka kanisani kuhusu Ukristo na CCM kama alivyofanya Prof Lipumba kule msikitini (kuhusu Uisilam na CCM) saa hizi hao viongozi wawili wa CDM wangekuwa wameshakamtwa kwa uchochezi na kufunguliwa mashitaka.

Hypothesis hii naweza pia kuisemea Mtwara na matukio yake ya hivi karibuni. Ingekuwa ni Moshi au Arusha ndiyo yametokea kama ya Mtwara -- saa hizi Lema, Mbowe, Nassari nk wangekuwa tayari wana kesi ya uchochezi mahakamani.

Nchi hii haina haki hata kidogo na ndiyo maana amani inalegalega sana!

Hizo ni hisia zako na fikra zako unatoa hukumu kwa kitu ambacho hakijatokea.
 
Wana CCM wanaugua ugonjwa mmoja hatari unaoitwa CHADEMA. Wake Zao CCM-B wanaeneza udini lakini wao kimya. Hawaoni aibu kumpikia mtu kesi heti ughaidi.
 
Hypothesis hii naweza pia kuisemea Mtwara na matukio yake ya hivi karibuni. Ingekuwa ni Moshi au Arusha ndiyo yametokea kama ya Mtwara -- saa hizi Lema, Mbowe, Nassari nk wangekuwa tayari wana kesi ya uchochezi mahakamani.

Nchi hii haina haki hata kidogo na ndiyo maana amani inalegalega sana!

Kwani kwa Tanzania HAKI ni nini na inaanzia wapi na mipaka ya haki ni ipi?. Halafu kulingana na bandiko lako, hata hiyo HAKI ZAIDI YA KIDOGO ikoje?.

Kwa Tanzania ambayo haina HAKI HATA KIDOGO ina maana kwa aliyoyafanya Prof.Lipumba Msikitini ni KOSA kwa vile haipo HAKI HATA KIDOGO au siyo kosa kwa vile Tanzania haina hata HAKI KIDOGO?.
 
Back
Top Bottom