Nawatakia kila la kheri CUF, ila Prof. Lipumba rejea "Long Walk To Freedom" By Nelson Mandela

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,580
18,157
Nimekua nikijizuia sana kutoa maoni kuhusu Kitendo Cha Prof.Lipumba kuondoka ndani ya CUF kwa sababu alizozitoa na yote aliyoendelea kusema na kutenda hadi kufikia siku za jana .Hii ni kwa sababu ya kanuni niliyojiwekea ya kuheshimu Mchango wake katika mageuzi,kujitoa kwake sadaka na pia kuitumia taaluma yake kwa ajili ya mapambano ya Fikra.

Vilevile nimekua nikijiepusha sana kujadili masuala yanayotokea ndani ya vyama washirika wa UKAWA tangu tuiingie katika muungano huu.Nk sehemu ya malezi ya kitaaluma na kiuongozi niliyojifunza

Lakini kwa kauli na matendo ya Prof.Ibrahim Lipumba Jana amenikumbusha nirejee kitabu cha Nelson Mandela "Long Walk To Freedom'' (Safari ndefu kutembea kuekekea katika Uhuru) aliandika "It is better to lead from behind during victory when nice things occur.And Take the Front line during danger.Then people will appreciate your leadership(Ni vizuri zaidi kuongoza kwa kukaa nyuma wakati wa kusheherekea ushindi yaani wakati mambo mazuri yanatokea .Na kuingia mstari wa mbele kuongoza wakati wa hatari.Hapo ndipo watu watakapoutambua na kuuheshimu Uongozi wako)"

Prof.Lipumba alidai kwamba ameona atengue barua ya kujiuzulu kwake baada ya kuona Demokrasia inaminywa nchini na pia wito kutoka kwa viongozi wa dini na wanachama wa CUF

Hilo la Wito wa Viongozi wa Dini sitaki kulijadili lakini hili la kujitetea kuwa ameona Demokrasia Inaminywa Nchini

Kipindi kile alipojiuzulu alisema alijiuzulu kutokana na Edward Lowassa kukaribishwa ndani ya CHADEMa na UKAWA. Lakini Hadi Sasa Lowassa yupo ndani ya CHADEMA na UKAWA.Je,kwa sababu Lowassa yupo akipata Uenyekiti atakiondoa CUF kutoka UKAWA?

Anapodai ameona Demokrasia inaminywa labda ameshindwa kujenga utetezi wake kisiasa vizuri.

Katika uchaguzi wa Mwaka jana,kwa matamshi na matendo yake alishiriki kuuingiza madarakani uongozi huu.Alishiriki kuuzuia UKAWA kushika Dola kwa kitendo chake ambacho kwa kiasi fulani kiliathiri muungano huu na kushusha morali ya baadhi ya wapiga kura kwa kuona kwamba jemedari wa mapambano amerudi nyuma

Kwa hiyo kama utawala huu unaminya Demokrsia na kutokidhi matarajio ya wengi yeye Binafsi hawezi kukwepa lawama.Ni dhahiri alipojiuzulu hakua na nia njema na kwa matendo na kauli zake za kugeukageuka(Flip-Flop) ameondoa doubt kwa sisi tulimpa Benefit of Doubt.Wengine tulidhani ni Principle zake tu

Kuna Video aliyorekodiwa 2013 akikiri kushiriki Kumnusuru Jakaya Kikwete Uchaguzi Mkuu 2010.Huyu ni Mzoefu wa kunusuru.

Jemedari huyu alirudi nyuma wakati wa mapambano lakini sasa anataka asimame mstari wa mbele wakati wa kusheherekea CUF kuongeza wabunge wa Majimbo Huku Bara,Wabunge wa Viti Maalum na pia kupitia Muungano wa UKAWA kushiriku kuongoza Halmashauri za Wilaya,Miji na Majiji

Profesa alikisoma vibaya kitabu cha Mzee Madiba Cha Long Walk to Freedom.Yeye badala ya kuongoza kutoka nyuma ya Mistari wakati wa kusheherekea sasa anataka awe mbele wakati wa Kusheherekea

Katika kipindi hiki ambacho Maalim Seif Shariff Hamad akiwa Ziarani nje ya Nchi kuhusisha jumuiya ya kimataifa juu ya uminywaji wa Demokrasia kule Zanzibar na Tanzania kwa ujumla yeye anafanya Press Conference huku kutaka kurudi kwenye Uenyekiti. Lengo ni kuchanganya Umma na pengine jumuiya ya kimataifa.Confusion!

Nimetafakari sana nikafikiria ni kwanini iwe kipindi hiki? Suala la Timing kwenye siasa ni kila kitu.Hata kama angekua na nia njema lakini amefeli vibaya sana kwenye Timing

Nikajiuliza ni kwanini Profesa huyu mwenye uzoefu sana kisiasa maana aligombea Urais kwa mara ya Kwanza na akiwa Mwenyekiti mimi nikiwa Darasa la Nne kule Hiti,Inakuwaje ashindwe kuyahisi mawimbi makali ya kisiasa hasa kipindi hiki ambacho wanaharakati a wapinzani tunaunganisha nguvu kupambana na udikteta yeye anaibuka katikati na kutonesha vidonda vinavyovunja moyo na kuchanganya wananchi kukumbushia uenyekiti wake?

Hoja zinazojengwa kuwa CUF kimekosa mtu sahihi wa Kuongoza chama huku Bara ni hoja ambazo kama nitazichukulia kwa uzito nitamgeuzia kibao Prof.Lipumba Mwenyewe

Yeye amekuwa Mwenyekiti kwa Zaidi ya Miaka 20 .Alishindwaje kuwaanda mfumo mzuri wa Succession Plan na kuandaa damu mpya kuongoza chama?Maana umaahiri wa kiongozi ni kuandaa viongozi wa baadae.Kinyume na hapo ni udhaifu

Hata kwenye Makampuni na Mashirika makubwa ,nadharia ya Uongozi wa Mashirika(Corporate Governance) inaelekeza kuwa ni jambo muhimu kuandaa Succession Plan

Kwa hiyo wanaomtetea watafute hoja nyingine maana hii itamfanya azidi kuonekana dhaifu

Mwisho,Nawatakia viongozi na wanachama wa CUF kila la Kheri.

Kama wanachama na uongozi wa CUF utaona anafaa basi hakuna tatizo kaa sababu kikubwa ni Kuzingatia katiba

Natoa Rai,Msikubali kuingia katika mgogoro na kutoka nje ya mjadala wa mapambano dhidi ya utawala wa kidikteta

Vyama vyote washirika wa UKAWA na nje ya UKAWA pamoja na asasi za kiraia,Taasisi na watu binafsi tunahitaji kuunganisha nguvu kipindi hiki kuliko kipindi kingine

Condoleezza Rice alisema "We need a Common Enemy To Unite Us" Ndio tunae adui ambae ni "Udikteta"

Kule Zanzibar CUF wanaweza kupambana na CCM wenyewe na Mambo yakaenda na Huku Bara CHADEMA kinaweza kufanya hivyo na Mambo yakaenda lakini Dunia ya sasa inahitaji Siasa za ushirikishwaji( Politics of Inclusiveness ).

Tusikubali kutoka kwenye mstari.

Utawala Mpya umeanza kupelekeshwa Puta.Katika mazingira haya ya Desperation wanaweza kutumia silaha yoyote kisiasa kama walivyofanya kipindi cha uchaguzi 2015 kwa falsafa ya Divide and Rule (Wagawe ili Uwatawale)

Nawapongeza CUF na wanachama wake kwa kuweza kuhimili misukosuko ile iliyotendwa kwa falsafa ovu ya "Mpige Mchungaji na Kondoo Watawanyike". Kondoo hawakutawanyika ,Mchungaji anajitega kwa mara nyingine apigwe ili Kondoo watawanyike

Sasa Mchungaji Mwema angekua na haja gani ya kujitega hadi apigwe ndipo Kondoo Watawanyike? Si angeweza kuwatawanya tu? Maana Kondoo huitambua sauti ya mchungaji.

Aluta Continua,Victory Ascerta......

Ben Saanane
 
Profesa: Mimi nilishiriki sana kumnusuru kikwete asishindwe...hali ilikuwa mbaya....ilibidi niwambie waislam mumpigie kura kikwete

Profesa: CCM ni Interahamwe chini ya uenyekiti wa Kikwete

Profesa:Lowasa ni mtu safi....kwani miaka yote minane yuko nje ya serikali kuna wizi mwingi umetokea...tatizo ni CCM

Profesa:Mmmmmm...Nafsi yangu inanisuta kumpokea Lowasa...najiuzulu

Profesa:Nimetengua maamuzi ya kujiuzulu kwa sababu demokrasia inagandamizwa.....ninarudi kwenye uenyekiti..hukuhuku alipo lowasa

Haya makada wa CCCM kujaaaaaa...Piga makofiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mr ben saanane,maelezo yako ni sahihi na yamejitosheleza kabisa! Labda mchungaji anataka akajaribu kwa mara nyingine kuja kuwatawanyisha kondoo! First attempt ili fail
 
Amenishangaza sana huyu Profesa, loooh! ina maana zile sababu alizosema zimemuondoa zimeondoka na uchaguzi? Yaani kuomba kurudi CUF kama mwenyekiti amajiaibisha kuliko siku alipotangaza sababu za kujiondoa CUF, huyu jamaa ni mtu wa ajabu sana, alichukua hela zza ccm akaenda kuhiji macca leo mwezi mtukufu anatubu tena kutaka kurudi cuff, hebu aanzishe chama chake kama anautaka sana uendekiti wa chama.
 
Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.
Source: Mwananchi
THURSDAY, AUGUST 6, 2015
 
Nimekua nikijizuia sana kutoa maoni kuhusu Kitendo Cha Prof.Lipumba kuondoka ndani ya CUF kwa sababu alizozitoa na yote aliyoendelea kusema na kutenda hadi kufikia siku za jana .Hii ni kwa sababu ya kanuni niliyojiwekea ya kuheshimu Mchango wake katika mageuzi,kujitoa kwake sadaka na pia kuitumia taaluma yake kwa ajili ya mapambano ya Fikra.

Vilevile nimekua nikijiepusha sana kujadili masuala yanayotokea ndani ya vyama washirika wa UKAWA tangu tuiingie katika muungano huu.Nk sehemu ya malezi ya kitaaluma na kiuongozi niliyojifunza

Lakini kwa kauli na matendo ya Prof.Ibrahim Lipumba Jana amenikumbusha nirejee kitabu cha Nelson Mandela "Long Walk To Freedom'' (Safari ndefu kutembea kuekekea katika Uhuru) aliandika "It is better to lead from behind during victory when nice things occur.And Take the Front line during danger.Then people will appreciate your leadership(Ni vizuri zaidi kuongoza kwa kukaa nyuma wakati wa kusheherekea ushindi yaani wakati mambo mazuri yanatokea .Na kuingia mstari wa mbele kuongoza wakati wa hatari.Hapo ndipo watu watakapoutambua na kuuheshimu Uongozi wako)"

Prof.Lipumba alidai kwamba ameona atengue barua ya kujiuzulu kwake baada ya kuona Demokrasia inaminywa nchini na pia wito kutoka kwa viongozi wa dini na wanachama wa CUF

Hilo la Wito wa Viongozi wa Dini sitaki kulijadili lakini hili la kujitetea kuwa ameona Demokrasia Inaminywa Nchini

Kipindi kile alipojiuzulu alisema alijiuzulu kutokana na Edward Lowassa kukaribishwa ndani ya CHADEMa na UKAWA. Lakini Hadi Sasa Lowassa yupo ndani ya CHADEMA na UKAWA.Je,kwa sababu Lowassa yupo akipata Uenyekiti atakiondoa CUF kutoka UKAWA?

Anapodai ameona Demokrasia inaminywa labda ameshindwa kujenga utetezi wake kisiasa vizuri.

Katika uchaguzi wa Mwaka jana,kwa matamshi na matendo yake alishiriki kuuingiza madarakani uongozi huu.Alishiriki kuuzuia UKAWA kushika Dola kwa kitendo chake ambacho kwa kiasi fulani kiliathiri muungano huu na kushusha morali ya baadhi ya wapiga kura kwa kuona kwamba jemedari wa mapambano amerudi nyuma

Kwa hiyo kama utawala huu unaminya Demokrsia na kutokidhi matarajio ya wengi yeye Binafsi hawezi kukwepa lawama.Ni dhahiri alipojiuzulu hakua na nia njema na kwa matendo na kauli zake za kugeukageuka(Flip-Flop) ameondoa doubt kwa sisi tulimpa Benefit of Doubt.Wengine tulidhani ni Principle zake tu

Kuna Video aliyorekodiwa 2013 akikiri kushiriki Kumnusuru Jakaya Kikwete Uchaguzi Mkuu 2010.Huyu ni Mzoefu wa kunusuru.

Jemedari huyu alirudi nyuma wakati wa mapambano lakini sasa anataka asimame mstari wa mbele wakati wa kusheherekea CUF kuongeza wabunge wa Majimbo Huku Bara,Wabunge wa Viti Maalum na pia kupitia Muungano wa UKAWA kushiriku kuongoza Halmashauri za Wilaya,Miji na Majiji

Profesa alikisoma vibaya kitabu cha Mzee Madiba Cha Long Walk to Freedom.Yeye badala ya kuongoza kutoka nyuma ya Mistari wakati wa kusheherekea sasa anataka awe mbele wakati wa Kusheherekea

Katika kipindi hiki ambacho Maalim Seif Shariff Hamad akiwa Ziarani nje ya Nchi kuhusisha jumuiya ya kimataifa juu ya uminywaji wa Demokrasia kule Zanzibar na Tanzania kwa ujumla yeye anafanya Press Conference huku kutaka kurudi kwenye Uenyekiti. Lengo ni kuchanganya Umma na pengine jumuiya ya kimataifa.Confusion!

Nimetafakari sana nikafikiria ni kwanini iwe kipindi hiki? Suala la Timing kwenye siasa ni kila kitu.Hata kama angekua na nia njema lakini amefeli vibaya sana kwenye Timing

Nikajiuliza ni kwanini Profesa huyu mwenye uzoefu sana kisiasa maana aligombea Urais kwa mara ya Kwanza na akiwa Mwenyekiti mimi nikiwa Darasa la Nne kule Hiti,Inakuwaje ashindwe kuyahisi mawimbi makali ya kisiasa hasa kipindi hiki ambacho wanaharakati a wapinzani tunaunganisha nguvu kupambana na udikteta yeye anaibuka katikati na kutonesha vidonda vinavyovunja moyo na kuchanganya wananchi kukumbushia uenyekiti wake?

Hoja zinazojengwa kuwa CUF kimekosa mtu sahihi wa Kuongoza chama huku Bara ni hoja ambazo kama nitazichukulia kwa uzito nitamgeuzia kibao Prof.Lipumba Mwenyewe

Yeye amekuwa Mwenyekiti kwa Zaidi ya Miaka 20 .Alishindwaje kuwaanda mfumo mzuri wa Succession Plan na kuandaa damu mpya kuongoza chama?Maana umaahiri wa kiongozi ni kuandaa viongozi wa baadae.Kinyume na hapo ni udhaifu

Hata kwenye Makampuni na Mashirika makubwa ,nadharia ya Uongozi wa Mashirika(Corporate Governance) inaelekeza kuwa ni jambo muhimu kuandaa Succession Plan

Kwa hiyo wanaomtetea watafute hoja nyingine maana hii itamfanya azidi kuonekana dhaifu

Mwisho,Nawatakia viongozi na wanachama wa CUF kila la Kheri.

Kama wanachama na uongozi wa CUF utaona anafaa basi hakuna tatizo kaa sababu kikubwa ni Kuzingatia katiba

Natoa Rai,Msikubali kuingia katika mgogoro na kutoka nje ya mjadala wa mapambano dhidi ya utawala wa kidikteta

Vyama vyote washirika wa UKAWA na nje ya UKAWA pamoja na asasi za kiraia,Taasisi na watu binafsi tunahitaji kuunganisha nguvu kipindi hiki kuliko kipindi kingine

Condoleezza Rice alisema "We need a Common Enemy To Unite Us" Ndio tunae adui ambae ni "Udikteta"

Kule Zanzibar CUF wanaweza kupambana na CCM wenyewe na Mambo yakaenda na Huku Bara CHADEMA kinaweza kufanya hivyo na Mambo yakaenda lakini Dunia ya sasa inahitaji Siasa za ushirikishwaji( Politics of Inclusiveness ).

Tusikubali kutoka kwenye mstari.

Utawala Mpya umeanza kupelekeshwa Puta.Katika mazingira haya ya Desperation wanaweza kutumia silaha yoyote kisiasa kama walivyofanya kipindi cha uchaguzi 2015 kwa falsafa ya Divide and Rule (Wagawe ili Uwatawale)

Nawapongeza CUF na wanachama wake kwa kuweza kuhimili misukosuko ile iliyotendwa kwa falsafa ovu ya "Mpige Mchungaji na Kondoo Watawanyike". Kondoo hawakutawanyika ,Mchungaji anajitega kwa mara nyingine apigwe ili Kondoo watawanyike

Sasa Mchungaji Mwema angekua na haja gani ya kujitega hadi apigwe ndipo Kondoo Watawanyike? Si angeweza kuwatawanya tu? Maana Kondoo huitambua sauti ya mchungaji.

Aluta Continua,Victory Ascerta......

Ben Saanane
Ben sio kulalamika Naona sio kulalamika msomi answers kuwamwanasiasa prof lipumba Nimsomi lakini si mwanasiasa Ila nyini mtanaka kutumia usomi wake kujijenga kisiasa matokeo take ndio haya anayoyafanya lipumba
 
Ben unapoint sana!
Lipumba kuna mengi ya kujiuliza juu ya dhamira yako ya kurudi cuf!
Pia siasa zako zinachanganya maana kuna saa unaonekana kuongozwa na misingi ya kiimani zaidi kuliko itikadi za siasa, kuna wakati uñakuwa mpinzani zaidi na kuna saa unaegemea serikalini zaidi (hasa mwanzoni mwa awamu ya 5) kuliko upande wa upinzani!
Karibu CUF na useme nini motives juu ya ujio wako mpya?
Sema una kipi tofauti ambacho unataka kukileta cuf kwa sasa! Inawezekana kwa sasa kuna dalili za udikteta kama ndio changamoto kuu, mihura yote iliyopita, serikali zilikuwa hazitendi haki (hii ni sehemu ya kauli zako) ambayo kimsingi haina tofauti na udikteta unaodai! So kipi kitakufanya this time uibuke mshindi over kitu kilichokushinda for over 20 years?
Kwako Ben Saanane hii succession plan unayoizungumza ni falsafa unayoiona haipo cuf tu? Hebu sema chadema hiyo plan ikoje? Ni katika ukoo wa viongozi au ni plan ya Taasisi? Ni ccm pekee wenye plans ambapo uvccm wanapanda na mNEC yeyote anaweza akawa ameiva kuwa chochote ktk chama! Lkn pamoja na hayo ccm wenyewe hawa entertain hiyo plans na cohorts zinapokezana vijiti, ingawa Mara zote haikutokea kama ilivyopangwa, Ila luckly ccm wana structure ya uongozi ambayo hata outsiders wakipush wanaweza kufikia summit, ref: Nyerere to Mwinyi: Mkapa to Kikwete na hii ya Kikwete to Magufuli! Plans hazikuwa hizo Ila structures zimewa accommodate hao outsiders na wamekubalika chamani tena against kambi za wenyeviti ktk nyakati tofauti, na wajumbe kugomea mapendekezo ya wenyeviti!
Huko kwenu, Zitto alitaka kutest uenyekiti, the prince akadai anafanyiwa uhaini, chama hakina mifumo ya kubeba outsiders!
Back to our point, namuelewa Lipumba kwa sababu hizo za kuwa na system za kifalme ktk vyama! Possibly hata some documents za chama zinaweza kuwa home kwake, and so hata uongozi mpya ufanye nini bado watakwama!
Vyama vya nchi nzima lkn vina ofisi 1 tu na funguo zinalala kwa mwenyekiti, lazima chairman akiondoka chama kiyumbe!
Hivyo vyama vyenu ni kama NGO ndugu yangu Ben, ni ujinga kuamini kuwa kwa mfumo huu mnaweza kuiondoa ccm, wote tutasubiri muwe taasisi za kisiasa ndio tuwape nafasi, ile long walk to freedom sio kwa viongozi pekee, hata taasisi zinapaswa ziwe na visions zenye tija!
 
Hakuna kazi ya ziada hapo zaidi ya kuanzisha chama chake! Njaa iko kichwani! Anaweweseka! Hatumtaki! Aende CCM watampa u DC kama issue ni njaa!

Makubaliano alifanya ns mkwere. Sasa yuko Sukuma haelewi somo. Mambo yamebuma anatafuta kichaka cha kujifichia aibu aliyopata.
 
Maelezo yako mareeeefu lakini hayachoshi kusoma.

Prof Lipumba alishajimwaga,anataka sasa watu wamsikie na kumuinua. Hana jipya analolileta!
Kama nafsi yake ilimsuta kwa sababu alimpokea Mh Lowassa basi iendelee kumsuta tu kwa sababu Lowassa bado yupo ndani ya UKAWA na chama chake yaaani CUF hakijajiondoa ndani ya umoja huu!

Je,anataka kuuvunja Muungano huu ambao aliupuuzia na bado ukazidi kuwa imara zaidi ya ilivyokuwa? Nini ajenda yake haswa?

Maalim Seif na viongozi wengine wanatakiwa kuwa imara Sana katika kutolea maamuzi hili suala. Kama anaipenda CUF abaki kuwa mwanachama wa kawaida wala asipewe nafasi ypyote zaidi.
 
Kuna sehemu umeigusia.....Lipumba ameongoza miaka 20 na hakuandaa succession plan ( ukasema huo ni udhaifu).

Je jambo hili halipo chamani CDM ndugu saanane.

Mengine yote nakubaliana nayo
 
Makubaliano alifanya ns mkwere. Sasa yuko Sukuma haelewi somo. Mambo yamebuma anatafuta kichaka cha kujifichia aibu aliyopata.
Down payment imeisha kaenda kufuata cha juu wamemgeuka! Nani sasa atachezea pesa? Zitoke wapi? Za kuendesha chama tu hakun sembuse za kulipa wazandiki?
 
yani nikiunganisha na yule dr.aliyekua mkuu wa mkoa morogoro yani sitamani hata kusoma walau master maana naona kama kidogo akili itaenda mirembe,nikichanganya na ile misemo ya zamani ya kitaaa kwamba ukisoma sana unakua chizi daaaah niacheni na kadegree kangu
 
Point sana. Niliona video Prof yeye akiwa mgombea wa Urais CUF akikiri alimsaidia Kikwete mgombea wa CCM kwenye uchaguzi wa 2010
 
Pia mwambie mboe aandae viongozi wa kumrithi umwenyekiti. Asiwe mwenyekiti wa maisha kwa sababu ya ruzuku.
 
Back
Top Bottom