Prof. Lipumba asema haungi mkono hatua ya Mbowe kusoma hadharani barua aliyomwandikia Rais, adai CUF haitasusia Uchaguzi katika Mazingira yoyote

Cybercrime

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
3,248
2,000
Hatua ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) – Taifa, kusoma hadharani barua aliyomuandikia Rais John Magufuli, imekebehiwa. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF – Taifa amekejeli hatua hiyo na kusema, ‘unapoisoma hadharani na pengine haijafika kwa Rais, unategemea nini?’

Tarehe 3 Februari 2020 mbele ya wanahabari, Mbowe alisoma barua aliyomwandikia Rais John Magifuli akiainisha mambo kadhaa ikiwemo kufuta uchaguzi wa serikali za mitaa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Leo tarehe 1 Februari 2020, Prof. Lipumba amesema, suala hilo linahitaji mbinu za kisiasa katika kumshawishi Rais Magufuli, kukubali maridhiano na vyama vya siasa vya upinzani.

“Unamwandikia barua rais, kabla hajaipata iko mitandao ya kijamii, unategemea nini? Lakini unapohitaji, mundikie na mpe muda. Unakuja kueleza umemuandikia barua, haijafika iko mitandaoni unategemea unayemuandikia ataimpa uzito.

“Hata mimi inawezekana nimeandika barua kuhitaji jambo, lakini siwezi kuiweka mitandao ya kijamii. Kuna namna inahitaji diplomasia ya hali ya juu katika hali hii,” amesema Prof. Lipumba.

Akizungumza kususa uchaguzi, Prof. Lipumba amesema, kwa mazingira yoyote yale, chama chake hakitasusa kushiriki.

Amesema, suala la kutoshiriki uchaguzi huo kutokana na kutokuwepo tume hiyo, haliungi mkono, licha ya kukiri ya kwamba, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haiko huru.

“Mtu anasema bila Tume Huru hatuwezi kuingia kwenye uchaguzi, hilo huwezi kusikia kutoka kwangu sababu najua hata kupigania Uhuru, wazee wetu Tanganyika walipigania Uhuru katika mazingira magumu,” amesema Prof. Lipumba.

Wakati huo huo, Prof. Lipumba amemshauri Rais Magufuli kuanza utekelezaji wa ahadi yake, katika kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru, aliyoitoa mbele ya mabalozi hivi karibuni.

“Kwa kuzingatia kwamba Rais ametuhakimishia hilo mbele ya wanadiplomasia
 

jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,758
2,000
Hii issue naona CHADEMA wameifanya kama strategy fulani, kwamba tumeshawaeleza nini kifanyike ili uchaguzi uwe huru na wa haki, na jamii husika nayo ijue kwamba tulishawaeleza, na ulimwengu mzima, kwamba CHADEMA hawako tayari kuona haki yao ikikandamizwa wakati wa uchaguzi mkuu.

Hivyo matukio yoyote/ viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani vikitokea (mf. kuibwa masanduku ya kura na mengine kama hayo) CDM kama chama cha upinzani hakitayavumilia, na ushahidi kwamba walishatoa onyo upo tayari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,865
2,000
Nimependa "hatutasusia uchaguzi Karina mazingira yoyote Yale" huyu ndio mwanasiasa mkomavu,amejifunza kwa kilicho mkuta Mwalimu,sio huyu mbowe na hekaya same zisizo na mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom