VIDEO: Prof. Lipumba akiri kumsaidia Rais Kikwete katika Uchaguzi 2010

Ex Spy

JF-Expert Member
Jan 15, 2007
213
1,726
Wakuu,

Katika zunguka zangu nikitafuta video ya kinachodaiwa kunaswa na Tanzania Daima (Ref Lipumba akiri kumsaidia Kikwete Uchaguzi 2010), nimefanikiwa kuipata video hii katika YouTube. Nimetafuta Part 2 ya Video hii sijaipata, nawashirikisha Part 1 yake ili tunapojadili mambo kama haya tusiuziwe mbuzi katika gunia.

Kinachoshangaza, tumefikia hatua hii kama nchi? Ndizo siasa zilizo nyuma ya pazia na wananchi tumefumbwa macho?

Video yenyewe hii hapa:

 
Last edited by a moderator:
Lipumba hafai hata kuwa Imamu wa msikiti, akiwa Imamu atataka awe Imamu wa Maisha kama alivyokuwa Mwenyekiti wa Maisha huko CUF

Waislam for 50 yrs bado tunalalamika na kuendelea kuichagua CCM badala ya kuangalia maendeleo ya nchi, sisi tunakadhania Uislam na Ukiristo huku Rasilimali zetu zinaibiwa na Wawekezaji walioletwa na Kikwete na CCM yake

Rais
Jaji Mkuu
Mkubwa wa Usalama wa Taifa
IGP
Hao wote ni waislam na bado tunalalamika kuwa tunaonewa, ni nani hasa anayetuonea kama sio sisi wenyewe tunaoneana? Tusitafute mchawi wakati mchawi wetu tunamchua kuwa ni CCM.

Badala ya kufikiria Maendeleo ya Taifa letu bado tumegubigwa udini na kunyooshea wenyewe kwa wenyewe vidole, sisi wote ni Watanzania na tuna haki ya kuishi katika Taifa letu bila ya kujali dini. Adui wa Muislan ni CCM hakuna mwengine.

Kikwete nchi imemshinda asitafute mchawi, aondoke kabla halijaangamia hili Taifa.

Sisi Waislam tujue kuwa Ukiristo, Uislam, Ubaniani, Ugalatia na dini nyingine zitakuwepo Tanzania na zitaendele kuwepo, as long the world still exist na hizo dini zitakuwepo.

Kwa hiyo wahubiri wa dini, Get lost

Adui wa Waislam ni CCM, tukifanikiwa kumtoa hii nchi itatulia na maendeleo ya nchi yatapatikana

Bado Nina Mashaka na Elimu ya Prof Lipumba naona haiimsaidi kujua lipi ni zuri na lipi ni baya kulisema kwenye jamii, hafai hata kuwa Kiongozi wa Mtaa. Shame on him.

Huyu Lipumba hana lolote anajitia anatatea haki za dini kumbe uchu wa madaraka kama alivyo Kikwete, Lipumba hafai hata kuongoza kwao urambo hatoweza.
 
hatimaye gazeti la Tanzania daima limethibitishwa kusema ukweli, hawakuongeza neno wala kupunguza neno. sasa lipumba kesho na keshokutwa atajifanya kuwa oohoo sikumahanisha inabidi ajiuzulu hafai kuwa kiongozi wa cuf ambacho kinawafuasi wa kiislamu na kikristo
 
Sijaelewa Lipumba kwenye issue ya kesi ya Mnyika na Ubungo, labda inaelekea anajaribu kumahanisha kuwa chama tawala ilibidi kitumie dola yake kupindua maamuzi ya kisheria au vipi?

Mtu huyu anaamini kweli hata katika uhuru wa mahakama? Anapigania demokrasia gani huyu?
 
Juzi Mh. Rais Kikwete alisema live hataachwa mtu hata awe na "mapembe".

Tunasubiri kuona mapembe yakikatwa na naamini ahadi ya Mheshimiwa Rais itatekelezwa sawia. Haiwezekeni waroho wachache kama akina Lipumba waipeleke nchi "Jehanam" kwa choko choko zao za kipuuzi kwenye majumba ya ibada.

Huyu Profesa aliyeishiwa vision alazimishwe kujiuzulu haraka kuinusuru CUF.
 
Pengine watu hatupendi tu kusoma alama za nyakati,ILA 2010 inajulikana CUF waliingia makubaliano na top leaders wa CCM,masheikh waliitwa na kupewa maelekezo na fungu kubwa lilikuwepo kwa CUF na Kuna wakati Lipumba alijisahau kwenye kampeni Mtwara akamshambulia Jeykey baadala ya kumshambulia Slaa,CUF walifokewa na kukumbushwa mkataba wa ndoa ya na CCM na hatimae Jusa aliomba radhi!!!

Lipumba ni mnafiki na mchumia tumbo tu na hana uzalendo wowote, kinachonisikitisha ni waislamu wenzangu kuamini uzandiki na propaganda za makuwadi wa waovu wa taifa hili kwa kupotoshwa na viongozi watawala kwa kutugawa,

Taifa linahitaji kiongozi mkweli,msafi,mchukia maovu na unyonyaji kwa kujaa uzalendo wa maendeleo ya taifa hili na wala sio uislamu wala ukristo,mioyo michafu na wizi hauchagui dini!!!

Waislamu tukatae kutumika,tusichqgue dini,tuchague watu sahihi kwa mustakabalii wa taifa na vizazi vijavyo!!!!
 
Mmmh, nimeisikiliza hii video hadi Mwisho. Naweza kusema Lipumba amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa CUF. Maana ameonyesha dhahiri kwamba yeye ni kiongozi wa waislam na si wakristo. Kwa msingi huo CUF ni chama cha waislamu.
Pia Kikwete amepoteza uhalali wa kuwa Rais wa nchi, kutokana na kutumia udini kujipatia urais. Lipumba anathibitisha bila shaka kwamba Kikwete alishinda kwa njia ya udini, je ana haja gani ya kuendelea kuwa Rais? Ajiuzuru!

pia amethibitisha hoja ya LEMA kuwa jk ndiye mwasisi wa udini TZ!
 
aya bana dini imeingiliwa wenye uwezo mdogo wakufikili wana haminishwa ujinga wanaamini ndio maana tunaona makanisa yakibomolewa nawachache wasio jitambua ebutufikilie watanzania kwanini tunakubari kugombanishwa ili rasilimali zetu ziondoke ninini kilichopo nyuma ya mgogolo huu wa kidini lipumba mungu anagawa karama ww ulipewa za darasani lakini sizakutawala tanzania we unadhiki yakutawala
 
Back
Top Bottom