Video: Ole Sabaya, Anavuna alichopanda Mapema!

Video: Ole Sabaya, Anavuna alichopanda Mapema!

Jamii ya kimasai; haitasahau kamwe manyanyaso ya awamu hii ya sita.

Kwanza imewafukuza kwenye ardhi yao ya asili Ngorongoro.

Na pili inamtesa kijana wao mahakamani kwa kesi ambazo hazina tija yeyote.
Hilo la kijana wao kuteswa, tusilihusishe na jamii yao
 
Avune alichopanda... hakuna hata kiongozi mmoja wadini amewahi mtetea ni wajinga wachache wakupangwa!!!
 
Huyu jamaa alitesa sana watu.
Sasa hivi na yeye anateseka, he found karma very early.

Tujifunze kutenda Mema!!View attachment 2355918
Huyu bwana alikuwa na tabia mbaya sana...

Lakini hapa nimemuhurumia aisee...

Lazima atakuwa amejifunza hata kama atatoka kesho...

Atakuwa amejifunza kuwa, kumbe kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe. Kwamba, ukiwatendea wanadamu wenzako wema na haki, utapata dhawabu au matunda ya wema na haki..

Kinyume chake ni kuwa, kila tendo la uovu malipo yake unayabeba mwenyewe peke yako..

Rafiki zake wako wapi hapo? Rais wake Magufuli anayedai kuwa alikuwa anamtuma kufanya uovu, yuko wapi kumsaidia? Na mke wake si ajabu hayupo, alishamkimbia...!

Looh, this is the very important life teaching lesson kwa viongozi wa umma...

Mimi nimeshamamehe. Bila shaka hata Mungu alishamsamehe iwapo ameomba msamaha kwake...

Na tukumbuke kuwa Mungu husamehe dhambi/makosa na kusahau kabisa. Lakini matokeo ya dhambi huweza kukaa ndani ya mtu kwa muda kidogo lakini mwisho wa siku neema ya kuondoka huja na athari za makosa hayo (kama anazohangaika nazo huyu jamaa) huondoka na mtu akasahau kabisa...

Ole Lengai Sabaya atatoka tu. Na nashauri akitoka, aende akahubiri Injili ya Yesu Kristo na aachane na active politics...
 
Haka kajambazi wanasubiri nini kukaweka nyuma ya nondo?

Ila sitashangaa wakikaachia ila hakawezi kukatiza mitaa ya Hai kwa miguu mchana kweupe .
 
Kama kesi zingekuwa zinaamuliwa kwa machozi hizo jela tunazozisikia na kuziona zisingekuwa na maana kuwepo kwake.

Wamuache ale matunda ya kazi yake.
 
Back
Top Bottom