Video: Ole Sabaya, Anavuna alichopanda Mapema!

Video: Ole Sabaya, Anavuna alichopanda Mapema!

Ndugu usipoteze nguvu zako hamna kesi hapo wanamchisha kutaka wamualibie CV yake
Ana CV gani??yaani kakaa Jela tangu Mei 2021 mpaka Septemba hii 2022 bado unasema hamna Kesi!!!acha kujipa moyo wakati unakula vizuri na mwenzako anaishi kwa filimbi Jela na analala sakafuni
 
Sabaya vumilia ni muda mchache tu Mwenye Enzi Mungu atakuinua tena maana hayo ni mapito ya binadamu!
Msifu Mwenye Enzi Mungu kwa yote!
Iko siku utakuwa huru tena na utanyanyuliwa na kuwa juu tena walahi nasema!
Kuna ule uwimbo unao sema “usifurahi juu yangu maana niangukapo mimi nitasimama tena”
Pole sana na uwe na afya na uzima!
 
Lakini serikali aliyotumikia ndio hiyo hiyo imemtia ndani
 
Hizi ni futuhi tu. Hawa ni wahuni waliolipwa (fedha alizopora Sabaya enzi za ushetani) kwenda kufanya hii futuhi mahakamani.

Mm bado sijaona chozi kwa Sabaya, natamani kumuona akifungwa miaka 80 jela
 
Kosa lake ni kuwataja waliomtuma, asingetoa siri
 
Sabaya anaonewa tu.

Huko ccm yote wamejaa majizi na madhulumati kama sabaya au zaidi ili wanalindwa na mamlaka.
Ni bahati mbaya tu Sabaya amekuwa na nyota ya punda. Amebeba madhambi kwa niaba ya wengine.
 
Wenzake wameachiwa
Wenzake wameachiwa mara baada ya kukiri makosa na wakaenda kupatana na DPP, kwakuwa makosa ni uhujumu uchumi wakalipa Tsh 1,050,000/= ila Sabaya ye bado anakana mashtaka.

Msingi wa hawa kukubali ili wawe huru mambo yaishe waendelee na maisha yao, msingi wa Sabaya kukaa ni utumishi wake na nsoto bado za kuwa mtumishi wa umma, unafikiri anashindwa kulipa one million? Nop hashindwi ata kdgo.
 
Hao jamaa wanaolia n kweli wanamaanisha au ndo hivo ka asali kametembea kuwa mislead jury??
Sikuhizi unaambiwa kuna vikundi vya kukodisha kulia mpaka kwenye misiba. Kulia kwa namna hiyo wala hakuashirii huzuni yoyote.

Sijawahi kusikia kama kuna watu waliwwhi kulia kutokana na kutoweka kwa Hitker. Tanzania ni salama zaidi bila ya uwepo wa watu kama hawa kwenye mifumo ya uongozi.

Kuwaweka majambazi kwenye mifumo ya uongozi, wanaweza kupanda, kiasi kwamba siku moja mkashtukia mmojawapo ameshika nafasi ya juu kabisa, kisha akawajaza waovu wenzake kwenye mifumo ya uongpzi, na jamii nzima ikataabika na kujuta.
 
Ndugu usipoteze nguvu zako hamna kesi hapo wanamchisha kutaka wamualibie CV yake
Jàmbazi anaharibiwa vipi CV? CV yake ipo mitaani kwenye vichwa vya watu aliowakata masikio,kwenye miguu ya watu aliowapigilia misumari, na kwenye mioyo ya watu aliowapora pesa.
 
Ana CV gani??yaani kakaa Jela tangu Mei 2021 mpaka Septemba hii 2022 bado unasema hamna Kesi!!!acha kujipa moyo wakati unakula vizuri na mwenzako anaishi kwa filimbi Jela na analala sakafuni
Sabaya hajafungwa mzee ila yupo mahabusu, Kesi yake haina dhamana tu hicho ndo kinafanya asiwe uraiani kumbuka kesi za mwanzo alishashinda ila DPP akaona amuundie nyingine Moshi ndo maana mpaka leo yupo ndani na wenzake watatu juzi wamekiri makosa wakaenda kupri bergain na DPP wakalipa Milion mona na elfu hamsini wakaachiwa huru ila Sabaya hajakiri makosa na wala hajaenda kupre bergain ila anaamini hakuna kesi atakuwa na hatia na ndiyo maana upande wa mashtaka mpaka leo wanachelewadha tu kesi kuwa upelelezi haujakamilika.

Sabaya akikiri makosa atakuwa amepoteaa vingi, atakuwa hafai tena kuwa mtumishi wa uuma, atakosa mengi na ndiyo maana nakuambia CV yake itachafuka na ndiyo maana kabaki pekee huko mahabusu kwenye ile kesi anakomaa nayo,. Labda achoke tu ila naye ana mdoto ila kiukweli upande wa mashtaka hawana ushahidi wowote pale zaidi kumnyima tu haki zake na kumtesa kisaikolojia kwasasa maana kumfunga ishakuwa ngumu tena.
 
Sabaya vumilia ni muda mchache tu Mwenye Enzi Mungu atakuinua tena maana hayo ni mapito ya binadamu!
Msifu Mwenye Enzi Mungu kwa yote!
Iko siku utakuwa huru tena na utanyanyuliwa na kuwa juu tena walahi nasema!
Kuna ule uwimbo unao sema “usifurahi juu yangu maana niangukapo mimi nitasimama tena”
Pole sana na uwe na afya na uzima!
Mkata masikio ya watu, mporaji wa mali za watu, mpigiliaji wa misumari miguu ya watu, atanyanyuliwa kwenda wapi? Huyu amebeba laana kuu.

Anachotakiwa ni kukiri uovu wake, kuujutia, kuwaomba msamaha aliowadhulumu, kisha kufanya toba ya kweli, ndipo apokee msamaha wa Mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom