VIDEO: Kilichotokea Chuo cha Uhasibu Arusha, Lema alivyowatuliza wanachuo

Waliyokosa busara ni polisi na mkuu wa mkoa,pamoja na yote hakukuwa na sababu za msingi za polisi kuwatawanya wanafunzi kwa mabomu ya machozi kwani hawakumfukuza Mkuu wa mkoa wala kumtupia mawe,wala hizo chupa alizosema ametupiwa kwani wangeondoka kimya kimya bila kutupa mabomu ya machozi wasingejulikana kama ni polisi?Mchochezi wa kwanza hapa ni Mkuu wa Mkoa na Polisi.Ifike mahali watanzania KOLEO tuiite KOLEO na siyo kijiko kikubwa.Inatia hasira na uchungu.Amka Lukolo hata kama wewe ni kada mzuri kuwa realistic,wafungue macho viongozi wetu.
Nilikuwa kada wa CCM kuanzia mwaka 1995 hadi kufikia mwaka 2007 niliitupa rasimi kadi ya CCM na kuchukua kadi ya CHADEMA. Lakini kuwa kwangu CHADEMA hakunifanyi niwe kipofu kiasi cha kutokuona kwamba Lema alikosa busara katika kauli yake. Jiweke kwenye viatu vya Mulongo! Na wewe ndiyo kiongozi wa mkoa halafu unaowaongoza wanakufanyia hayo! Halafu uniambie how it feels!

Kwenye suala la kuwashambulia wanafunzi ambao walikuwa hawaleti fujo hilo ni kosa, na sijaona kabisa sababu ya kuwapiga mabomu wakati hakuna amri ya polisi waliyokataa kutii. Ninachojua mimi kabla ya kupiga mabomu huwa kuna kile kitambaa chekundu na matangazo ya polisi yanayosema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawataka mtawanyike, na msipotii ndiyo mnapigwa mabomu. Sasa sijaona hiyo procedure kwenye hili tukio. Katika hilo, sheria zimevunjwa. Lakini uamuzi wa Mulongo kumsaka Lema upo sahihi, kwa kuwa Lema alimdhalilisha mkuu wa mkoa mbele ya wanafunzi.

Mimi nasema ule tu mwitikio wa mkuu wa mkoa kwenye tukio hili ulikuwa ni ustaarabu tosha. Maana angetaka angegoma na kumtuma mkuu wa wilaya au afisa mwingine yeyote wa mkoa au wilaya. Lakini yeye alitoka mwenyewe ofisini kwenda kuonana na wanafunzi. Hilo pekee linastahili pongezi. Yaliyojiri hapo, haikuwa kazi ya Lema kuyaelezea.
 
Nimeangalia hii Video kwa makini; bila kuegemea mrengo wowote wa kiitikadi ninachoweza kusema Mh. Lema alivuka mipaka kwenda kuhutubia wanafunzi bila kukaribishwa na uongozi wa chuo, mbaya zaidi katika kuongea nao alikuwa akiwaita "makamanda" na hivyo kufanya uwepo wake pale kuwa wa kisiasa zaidi badala ya utatuzi wa tatizo la uvamizi wa vibaka. Hata kumpigia simu Mh. Mkuu wa mkoa haukuwa wajibu wake bali wajibu wa uongozi wa chuo kuomba msaada wa polisi kusaidia kutuliza fujo. Haya ni maoni yangu huru kabisa

Kama hayo ni maoni yako HURU basi una matatizo ya kiakili. Umeambiwa Lema alifuatwa na wanafunzi kwa kuwa anaishi jirani na chuo hicho. Pia aliwarudisha wanafunzi wasiandamane hadi kwa mkuu wa mkoa ila wamsubiri mkuu wa mkoa aende chuoni, sasa hapo unataka aombe kibari cha uongozi wa chuo kuwarudisha wanafunzi waliokuwa wanaandamana. Hayo ni maoni ya KITUMWA sio huru. SERUKAMBA
 
Kama hayo ni maoni yako HURU basi una matatizo ya kiakili. Umeambiwa Lema alifuatwa na wanafunzi kwa kuwa anaishi jirani na chuo hicho. Pia aliwarudisha wanafunzi wasiandamane hadi kwa mkuu wa mkoa ila wamsubiri mkuu wa mkoa aende chuoni, sasa hapo unataka aombe kibari cha uongozi wa chuo kuwarudisha wanafunzi waliokuwa wanaandamana. Hayo ni maoni ya KITUMWA sio huru. SERUKAMBA

wehu bana...achana nao....hzo ni nyumba ndogo za mwigulu
 
Kwa kweli serikali ya ccmafisi imekwisha. Kwanza anaeitwa mkuu wa mkoa wa Arusha hastahili kabisa cheo icho, hana kabisa qualification ya vyeo vyao ambazo hazitakiwi. Ukiangalia video 1.

Lema kajitaidi sana kuwatuliza wanafunzi na kama mbunge, mzazi, kaka, rafiki yao kawapa maeno ya kuelemisha kuliko kawaida na walimwelewa sana.

Video 2
Anaeitwa mkuu wa mkoa ukimwangalia toka anavyoongea, yani tayari alikuwa na hasira na ghadhabu.
Ni kijana ambaye kiuongozi hawezi yani hafai anawaharibia vijana na kuonekana kuwa vijana hawawezi.

Ni yeye ndie alietoa amri kwa Jeshi lake kuwafyatulia wanafunzi mabomu baada ya kuona wanafunzi wanamzomea. Hafai yani alishindwa uvumilivu. Kwani angehamua kuondoka yani kupanda gari na kuondoka ile hali isingetokea kwasababu wanafunzi walikuwa chuoni kwao na hawakuwa wakipigana na watu au kikosi chochote. Yeye angejiondokea wanafunzi ikafungwa geti lao na wangeendelea kubaki chuo.
Katika ili Kikwete hafai kama ndio umakini wake wa kuchagua viongozi ndio hivi. Nasema ndio mana nchi kila kona mabomu.
Kwa hili Mulongo anaondoka Arusha. Kwani yeye ndie alieamrisha wanafunzi kupigwa mabomu ivyo inabidi hashtakiwe.

Mwisho nawapa pole wanafunzi kwa kupigwa mabomu kupoteza vitu vyao vya dhamani halafu wanarudishwa nyumbani, kwa kweli ni uonevu mkubwa sana uliyofanywa na serikali. Na pia nawapa pole wazazi wa mwanafunzi aliyeuwawa
 
Hapa wamevuliwa nguo. Natarajia polisi waichukue hii haraka sana itumike kama ushahidi kama walivyoichukua ile ya rwaka.
 
Kama hayo ni maoni yako HURU basi una matatizo ya kiakili. Umeambiwa Lema alifuatwa na wanafunzi kwa kuwa anaishi jirani na chuo hicho. Pia aliwarudisha wanafunzi wasiandamane hadi kwa mkuu wa mkoa ila wamsubiri mkuu wa mkoa aende chuoni, sasa hapo unataka aombe kibari cha uongozi wa chuo kuwarudisha wanafunzi waliokuwa wanaandamana. Hayo ni maoni ya KITUMWA sio huru. SERUKAMBA

Ulukolokwitanga Sikatai Lema kwenda kama jirani ila kwenye maneno yake aliyowaambia wanafunzi baada ya mkuu wa mkoa kudai kipaza sauti ndipo aongee yalivuka mipaka na yaliwaongezea wanafunzi hasira na huo ndio unaitwa uchochezi; after all baada ya mkuu wa mkoa kufika pale chuoni; mwenyeji wake alistahili kuwa Mh. Lema au uongozi wa chuo? Pili, kueleza mambo ya michakato ya chaguzi za madiwani nayo yalikuwa ni mahali pake?
 
du hii thread ipo bize mno, ok ntaiangalia usiku. ila magesa kachemka. jamaa mtupu sana.
 
Nimeamua kuweka video hapa ili watanzania muweze kuamua kama kweli Mhe. Lema alihusika na mauwaji na kuchochea vurugu chuo cha uhasibu Arusha kama mkuu wa Mkoa wa Arusha (Mulongo) anavyodai.
Part I
[video=youtube_share;_z-Cl4nNva0]http://youtu.be/_z-Cl4nNva0[/video]

Part II
[video=youtube_share;Y1Zy44AokSw]http://youtu.be/Y1Zy44AokSw[/video]

Wakuu nisaidieni sipati link Kabisa
 
Hujaichakachua na kuweka yale ambayo roho yako inataka?!,mbona walipoweka ile ya Lwakatare mliwahi kusema imechakachuliwa?!hata sikuamini wewe una lako jambo siku hizi kwenye video unaweza fanya lolote lile,ukabadili ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli.
 
Watanzania wanaona........................ ni wangapi watakaounga mkono RC kushindwa kuongea na wanafunzi kwa kukosa kipaza sauti?
Kwanza isitoshe RC ndiyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, alitakiwa kuwa wa kwanza kupata taarifa ya kifo kama kile kwenye mkoa wake. Bado amesaidiwa na lakini chakushangaza anaigeuza swala la mauaji kisiasa.
Tutaandaa maandamano ya kumwondoa RC feki namna hii.
Mulongo tokea aje amekuwa anafanya kazi ya ukatibu mwenezi wa ccm!!!!!!!!!!
Poor Mulongo!
 
Hujaichakachua na kuweka yale ambayo roho yako inataka?!,mbona walipoweka ile ya Lwakatare mliwahi kusema imechakachuliwa?!hata sikuamini wewe una lako jambo siku hizi kwenye video unaweza fanya lolote lile,ukabadili ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli.

Kiongozi hii video ipo live zaidi, inaonekana kama ilivyo. ile ya lwakatare ilikuwa on Skype
 
Nadhani Lema anajua Nini Maana ya Uongozi, uongozi ni utumishi Na si ubabe Kama serikali yetu inavyotaka.. Ni kweli, Kiongozi lazima uwe mnyenyekevu Na si mbabe Kwa unaowatumikia, tumezoea kuwaabudu sana VIONGOZI nao wanajiona kwelikweli ni LAANA gani hii..
 
CCM wasahau Arusha kabisa..

Kuanzia Lolliondo Mpaka Arusha mjini fujo tupo.
Na yote ni ajili ya utendajo mmbovu wa kazi.
 
Back
Top Bottom