Chuo cha Uhasibu Arusha chatoa neno kwa wanafunzi wake kuandamana

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Chuo cha Uhasibu cha Arusha,IAA kimetoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizo sambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba wanafunzi wa chuo hicho wameandamana usiku wakidai fedha za mikopo kutoka bodi ya Mikopo na kudai kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote ni za kupuuzwa.

Akiongea na vyombo vya habari chuoni hapo ,kaimu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Epaphra Manamba alidai kwamba wanafunzo 801 kati ya 4700 wa chuo hicho ambao ni wanufaika wa bodi ya mkopo ya elimu ya juu walifanya kikao na mdhamini wao majira ya jioni kwa lengo la kupata ufafanuzi juu ya madai yao ya mkopo na sio maandamano kama ilivyoandikwa.

Prof. Manamba alisema kuwa wanafunzi hao wakikutana kwa lengo la kutaka kujua hatma ya fedha zao za mkopo ambazo zilitumwa na bodi ya mikopo kabla ya serikali kufunga vyuo kutokana na janga la Korona.

Hata hivyo Profesa Manamba alisema kuwa uongozi wa chuo hicho ,Bodi ya Mikopo ,wanachuo na ofisi ya Mkuu wa wilaya ulikutana na kujadiliana jambo hilo na kufikia mwafaka kwamba chuo kuiomba bodi ya mikopo itoe fedha za nyongeza kwa wanafunzi hao kwa sababu kipindi cha janga la Korona walikuwa wanasoma kwa njia ya mtandao.

"Wanafunzi walipokea pesa ya Miezi miwili toka bodi ya mikopo na fedha hizo zilitumiakabkwa siku 9 tu kabla serikali haijafunga shule na Vyuo tarehe 18/3/2020 kwa sababu ya Korona ,na mategemeo ya wanafunzi ni kupewa fedha za siku 60 na sio siku 20 kwa sababu IAA walikuwa wakiendesha masomo kwa njia ya Mtandao wakati vyo vimefungwa"

"Pia tumeiomba bodi ya mikopo kuwaongeza fedha za siku sita baada ya ratiba ya mitihani kubadilika kutoka Agosti 7 ,2020 na kuwa agosti 13 mwaka huu" Alisema

Aidha Prof Manamba alikiri kwamba chuo kiliomba fedha kipindi cha masomo tu bila kujumlisha muda ambao wanachuo walikuwa wanasoma kwa njia ya mtandao katika kipindi serikali ilifunga shule na vyuo .

Kwa upande wake Rais wa serikali ya wanafunzi (IAA),Michael Munish alisema kuwa wanafunzi hao hawana mgogoro wowote na chuo na kwamba taarifa kwamba walifanya maandamano hazina ukweli wowote na zimelenga kuwachonganisha wanafunzi na chuo chao.

"Kilichotokea ni kutoelewana kuhusu taarifa ya bodi ya mikopo (Long Board)na wanafunzi baada ya bodi ya mikopo kuleta fedha kiasi cha sh,170,000 kwa wanafunzi kama fedha za kujikimu kinyume na mahitaji ya wanafunzi" Alisema Munish.

Aliongeza kuwa uongozi wa chuo, wanafunzi ,mwakikishi wa bodi ya Mikopo na Mkuu wa wilaya walikaa kikao Jana na kukubaliana kwamba suala hilo Lima shughilikiwa.

"Tunashukuru kwamba chuo kimewaruhusu wanafunzi kufanya mitihani kuanzia wiki ijayo hata kama hawajamaliza ada wakati wakisuburi nyongeza ya fedha za mikopo kupoka bodi ya Mikopo" Alisema Munish.

Rais huyo wa serikali ya wanavyuo alisema kuwa picha za jengo zilizotumika kuonyesha wanafunzi wakiwa juu ya jengo hilo wakiwa wamejikusanya wakiandama hazina ukweli wowote kwani ni picha za zamani.

IMG-20200726-WA0008.jpg
IMG-20200726-WA0007.jpg
IMG-20200726-WA0009.jpg
 
'Kilichotokea ni kutoelewana kuhusu taarifa ya bodi ya mikopo (Long Board)na wanafunzi baada ya bodi ya mikopo kuleta fedha kiasi cha sh,170,000 kwa wanafunzi kama fedha za kujikimu kinyume na mahitaji ya wanafunzi" Alisema Munish.'

'Long board' ni noma sana.
 
'Kilichotokea ni kutoelewana kuhusu taarifa ya bodi ya mikopo (Long Board)na wanafunzi baada ya bodi ya mikopo kuleta fedha kiasi cha sh,170,000 kwa wanafunzi kama fedha za kujikimu kinyume na mahitaji ya wanafunzi" Alisema Munish.'

'Long board' ni noma sana.
Long board ni ile kamati ya kupambana na viba100? Lol!
 
Nimesoma maelezo yote, lakini nimeshindwa kuona mantiki nzima ya huo ufafanuzi. Kwa mfano....

-Kuna dhambi gani kama kweli hao wanafunzi waliandamana? Mbona maandamano vyuoni ni jambo la kawaida sana.

-Hivi uongozi wa Chuo unawezaje kufanya kikao na wanafunzi 800, siku ya jumamosi, jioni bila kuwepo na shinikizo la maandamano, mgomo nk hapo chuoni?

-Uongozi wa ofisi ya mkuu wa mkoa inahusikaje kwenye mambo ya chuo na bodi ya mkopo?

-Kama wanafunzi walisoma kwa njia ya mtandao wakiwa nyumbani, ni vipi udai wapewe pesa za kujikimu kutoka bodi ya mikopo as if walikuwa chuoni?
 
Back
Top Bottom