Nimeamua kuweka video hapa ili watanzania muweze kuamua kama kweli Mhe. Lema alihusika na mauwaji na kuchochea vurugu chuo cha uhasibu Arusha kama mkuu wa Mkoa wa Arusha (Mulongo) anavyodai.
Part I
[video=youtube_share;_z-Cl4nNva0]http://youtu.be/_z-Cl4nNva0[/video]
Part II
[video=youtube_share;Y1Zy44AokSw]http://youtu.be/Y1Zy44AokSw[/video]
Hii video imemuumbua Lema. Kwa hakika hapa Lema hakwepi. Ni wazi kwamba alichochea vurugu, na amemdharau mkuu wa mkoa.
Kwanini yeye asingeacha hayo maneno yasemwe na mkuu wa mkoa mwenyewe? Haya bwana ameyatafuta mwenyewe. Mwanzoni alifanya vizuri sana na ameongea maneno ya msingi sana. Lakini kuanzia baada ya mkuu wa mkoa kufika, Lema hakupaswa kuendelea kuwa msemaji tena.
Kwa busara za kawaida kabisa, alipaswa amuachie mkuu wa shule na mkuu wa mkoa waseme wanayotaka, lakini kitendo cha kusimama na kuwatangazia alichokisema mkuu wa mkoa na kuwatamkia wanafunzi kwamba hawa ndiyo aina ya viongozi tulionao na nini ambacho mkuu wa mkoa alipaswa kufanya hakikuwa sawa kabisa. Kwanza alipaswa aheshimu uamuzi wa mkuu wa mkoa kufika eneo la tukio.
Katika hili sitaweza kumtetea Lema. Amelikoroga.
Tukisema CCM ni wauwaji kuna punguwani wanakataa ona wameanza kujisahau.....Wampe kesi ya mauaji.chezea dola wewe!!,nanyinyi ambao muna kimbelembele cha maandamano endeleeni,si munakumbuka walikufa watatu mwanzo,wamesahaulika na maisha yanaendelea.kudadadadeki!!!,na kwa mungu virungu.
Ulukolokwitanga Sikatai Lema kwenda kama jirani ila kwenye maneno yake aliyowaambia wanafunzi baada ya mkuu wa mkoa kudai kipaza sauti ndipo aongee yalivuka mipaka na yaliwaongezea wanafunzi hasira na huo ndio unaitwa uchochezi; after all baada ya mkuu wa mkoa kufika pale chuoni; mwenyeji wake alistahili kuwa Mh. Lema au uongozi wa chuo? Pili, kueleza mambo ya michakato ya chaguzi za madiwani nayo yalikuwa ni mahali pake?
Mimi nasema ule tu mwitikio wa mkuu wa mkoa kwenye tukio hili ulikuwa ni ustaarabu tosha. Maana angetaka angegoma na kumtuma mkuu wa wilaya au afisa mwingine yeyote wa mkoa au wilaya. Lakini yeye alitoka mwenyewe ofisini kwenda kuonana na wanafunzi. Hilo pekee linastahili pongezi. Yaliyojiri hapo, haikuwa kazi ya Lema kuyaelezea.
Hitimisho: Mkuu wa Mkoa hafai, hana uwezo wa uongozi, hastahili kuwa hata Afis Mtendaji wa Kijiji. Is an exceptionally hopeless leader with no qualities.
Inafunguka vizuri sana. Jaribu kuangalia settings za computer yako huenda zina kasoro.Video haifunguki mbona?
Mkuu sikatai mawazo yako. Ila haikuwa kazi ya Lema tena kurudisha feedback kwa wanafunzi juu ya nini amesema mkuu wa mkoa. Ilikuwa ni kazi ya mkuu wa shule. Soma post ya Ulukolokwitanga. Lema hakuwa mwenyeji wa mkuu wa mkoa? Na kiprotacally, si Lema aliyepaswa kuwajibu wanafunzi. Na hata kama aliona ni vema kuwajibu kwa kuwa ndiye aliyewaahidi kwamba amemwita, basi angewaambia tu kwamba unafanyika utaratibu wa kupata mic ili aweze kuongea na ninyi. Au kauli zile za eti woga ndiyo adui mkubwa .... mara sijui hawa ndiyo aina ya viongozi tulionao na kuanza kuelezea namna kiongozi anavyopaswa kuwa.... blabla yalikuwa yanini? huko ndo kulikuwa ni kuwapandisha hasira wanafunzi. Na pia ilikuwa ni dharau kwa mkuu wa mkoa. Ni vizuri tuwe wakweli kwamba Lema alikosa hekima. Na inawezekana ana bifu binafsi na mkuu wa mkoa. Kama mkuu wa mkoa alikubali kuja basi ni dhahiri kwamba alikuwa na nia njema. Na ni kweli kwamba mic ilikuwa mhimu ili kuweza kuongea na ule umati. Na kwa kuwa mkuu wa mkoa alisema hayo na makamu mkuu wa shule, basi hakukuwa na sababu ya Lema kumsemea. Angemwachia makamu mkuu wa chuo kufanya hayo.Mkuu, hivi wewe ukiamka asubuhi kwenda shule unastahili kupongezwa? Yaani kazi ama shughuli ama wajibu wako mwenyewe bado unataka upongezwe, umeitoa wapi wewe hii? Mrejesho kwenye jambo lolote ni muhimu na ndo maana ni lazima wanachuo waambiwe kisa na mkasa cha mkuu wa mkoa kukataa kuongea nao, maana toka mwanzo aliwahakikishia kuwa ameshanogea naye na wavute subira, what else ulitaka?
Hii video imemuumbua Lema. Kwa hakika hapa Lema hakwepi. Ni wazi kwamba alichochea vurugu, na amemdharau mkuu wa mkoa.
Kwanini yeye asingeacha hayo maneno yasemwe na mkuu wa mkoa mwenyewe? Haya bwana ameyatafuta mwenyewe. Mwanzoni alifanya vizuri sana na ameongea maneno ya msingi sana. Lakini kuanzia baada ya mkuu wa mkoa kufika, Lema hakupaswa kuendelea kuwa msemaji tena.
Kwa busara za kawaida kabisa, alipaswa amuachie mkuu wa shule na mkuu wa mkoa waseme wanayotaka, lakini kitendo cha kusimama na kuwatangazia alichokisema mkuu wa mkoa na kuwatamkia wanafunzi kwamba hawa ndiyo aina ya viongozi tulionao na nini ambacho mkuu wa mkoa alipaswa kufanya hakikuwa sawa kabisa. Kwanza alipaswa aheshimu uamuzi wa mkuu wa mkoa kufika eneo la tukio.
Katika hili sitaweza kumtetea Lema. Amelikoroga.
Wakuu wa Mikoa ni janga la Taifa. Mbona mwenzie Kandoro hakupanic wana Mbeya walipotulizwa na Sugu na kusukuma gari lake hadi nyumbani kwake na kumwita Rais wa Mbeya? Naomba mwenye kumfahamu vizuri huyu Magesa Mulongo ni nani na kabla ya hapo alikuwa wapi na shule yake ikoje ili tuweze kumjadili vizuri hapa
Nashangazwa na watanzania walivyokuwa walalamikaji, kwamba wanahitaji ukombozi wakati huohuo wanadai nchi hii ilikombolewa. Yote sawa, lakini sikumbuki katika historia kama kweli tulipata ukombozi kama ujinga, umaskini na maradhi ndiyo waliokuwa maadui toka uhuru na baada ya uhuru, basi ukombozi na Uhuru haukuwa wa kweli ni kiini macho. Hakuna cha Mwalim wala mwanafunzi tusidanganyane hapa. Nilitarajia waliokuwepo wangeweka misingi imara ya kiuchumi, kijamii, kielimu na hata kisaikolojia. Msingi haukuwa imara, nyufa kibao ndiyo maana sasa watu wanagombea fito. Eti leo ndiyo babara zajengwa, mipango miji haikuwepo, alifanya ninin huyo anayesemwa alitengeneza kama siyo kuharibu, dhulma za mali za watu akidai kutaifisha mali za umma, mashule taasisi za kijamii, mashamba na alishindwa kuendeleza kama rafiki yake Mugabe. HE was a messed up Conspirator. Uhuru kwa heri Ukoloni karibu.Mkuu video haifunguki, nilishaanza kupiga makofi wa wa wa !!!
CC: Kwa wale wakipendao chama chao hata kama hakina mashiko kwa maskini wa tanzania!!! Imagine over 60% are poor!! And few in heaven!! To hell!! Kweli haya ndiyo maisha na ukombozi aliopigania marehemu baba wa Taifa hili? Sitakusahamu mwalim, kama si wewe nisingesoma mama yule mjane asingeweza kunisomesha!!
Nimeangalia weee video zote mbili, sijaona kosa la Lema wala wanafunzi!! Yule mkuu wa mkoa anaonekana hana akili kabisa, alishindwa kabisa kusama upepo wa wanafunzi kwa wakati ule walitakiwa waambiwe nini!!!!!!!