VIDEO: Hotuba ya M/Kiti wa CHADEMA Taifa wakati akifungua Kikao cha Dharura cha Kamati Kuu

Wewe ndio unaumwa kweli, na wewe pia mbona ni kipeperushi cha CCM. Kwani hao tbc wasipotangaza habari za CHADEMA ndio kitakufa? tena ndio kitapanda chat, kabla ya kuchangia uwe unafikiria kwa kutumia akili, lakini kwa kuwa nawe ni kipeperushi sikushangai. Toka lini ukaona tbc inatangaza mazuri ya chadema? na hicho ulichoita kituo cha habari cha taifa kina msaada gani kwa taifa? kuonyesha ccm tu? wanashindwa kuonyesha matukio muhimu ya hapa tz wanaonyesha upuuzi mtupu. kakoje ulale:bange::bange::bange:
Mkuu, kukomboa nchi siyo lelemama. Aina ya watu kama hao unaosema wakakojoe walale ni wengi sana hapa nchini. Kazi ya cdm ni kuwaelimisha watu wa namna hiyo ili wafunguke.
 
Kwa kweli ITV,Star tv,Channel ten zitaisaidia sana CDM kwenye upande wa habari kwa kipindi hichi ambapo TBC imekuwa ya CCM swali ni kwamba ikitokea CDM ikashika serikali je TBC itaendelea kuwepo?
 
Amechemka sana. Kiongozi wa siasa lazima uwe mvumilivu na mwenye kuchagua maneno ya kuongea. Kitendo cha kukiita kituo cha habari cha taifa ''kipeperushi cha CCM'' kinaonyesha dhahiri kuwa mheshimiwa huyu hana busara wala uvumilivu wa kisiasa. Sasa TBC wakigomea kutangaza habari za CHADEMA atamlilia nani sijui? Watu wengine bwana.

busara ipi ? Kama unasema Tbccm walishagoma kitambo na mbio zao zitaishia sakafuni,ITV,STAR TV watarusha na CDM inasonga mbele,tbccm nawachukia kutoka moyoni mwangu,na nikikuta mtu anatazama nahis kichefuchefu,poor tbc poor ccm.
 
Hotuba ya nani huyo? Mbowe au Dr. Slaa manake hapo ndipo CDM inatengeneza mgombea Urais!
mkuu umesahau mbowe alishasema aongozi genge la watafuta urais sasa watawezaje kutengeneza mgombea msibani? hata hivyo sijaiona wala kusikia ya dr babu wa ukweli
 
Kwa kweli ITV,Star tv,Channel ten zitaisaidia sana CDM kwenye upande wa habari kwa kipindi hichi ambapo TBC imekuwa ya CCM swali ni kwamba ikitokea CDM ikashika serikali je TBC itaendelea kuwepo?

Itaendelea sana kuwepo na itakuwa inapiga filimbi za CDM! Unadhani itafutwa? Hakuna kitu kama hicho hivi vyombo vya habari vya umma katika nchi zetu hizo vyote viko hivyo hivyo. Hukumbuki TV za Libya na Misri wakati wa michakato ya kuwahujumu akina Qadaf (RIP) na Mubarak. Kabla ya tawala zile hazijaanguka walikuwa sambamba na viongozi hao lakini zilipoanguka wakawa wa walioitwa wanamapinduzi. Huwa viko very strategic na vinabadilika kama vinyonga.
 
mkuu umesahau mbowe alishasema aongozi genge la watafuta urais sasa watawezaje kutengeneza mgombea msibani? hata hivyo sijaiona wala kusikia ya dr babu wa ukweli

Mkuu hayo ni maneno ya majukwaani tu. Kwa hiyo hakutakuwa na mgombea mwaka 2015? Kama atakuwepo atakuwa ametengenezwa lini? Kuna siasa za ndani na siasa za majukwaa.
 
Ni kituko kwa chama kinachojiita makini kuruhusu mwenyekiti msanii msanii kama huyu mbowe na hotuba ya ajabuajabu iliyorushwa leo kwenye hii jamii forum. Inawezekanaje chama kumlalamikia rais kikwete eti kwa nini aliamua kwenda kampala kuhudhuria usuluhishi wa kongo na kuacha kwenda kumzika mwangosi. Lakini chama hicho hicho kililazimisha kwenda kwenye msiba na kukutana na professor mark mwandosya ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya rais. Kama chadema haaminiani ndo maana katibu wa chama anakwenda kufungua matawi vijijini tena kwa kulazimisha na kukataa kutii sheria pasipo shuruti. Halafu kamati inakaa kusikiliza porojo za kufungiwa mwanahalisi, ulimboka kutekwa nyara. Haya yoote kwa jamii ni historia. Watanzania tunamambo mengi ya kufanya kuliko haya ambayo chadema wanajidanganya kuwa ni matatizo. Inatia shaka kama hawana mkono kwenye hizi makala za mwanahalisi na migomo ya madaktari. Tunapata funzo gani kuhusu umakini wa hikichama?

Hivi mkuu unasikiliza na kutazama kwa kutumia nini?? Hakuna sehemu yoyote ya hotuba ya Mbowe inayomtaka rais kwenda kumzika Mwangosi ila kuna sehemu inayohoji ukimya wake juu ya jambo kubwa kama hili.

Ya mwanahalisi na Ulimboka sio historia maana mpaka sasa tunaumia sana na impact yake bado ni kubwa sana kwetu sisi watu wa kawaida. Madaktari wanazidi kukimbia nchi, madawa, vifaa tiba bado yanatutesa-Hivyo haiwezi kuwa HISTORIA.

Hivi ni baadhi tu ya mambo ambavyo hamtaki kuvisikia ila mtaendelea kuvisikia tu maana vinatutesa wengi.
 
Wakuu kwa uzoefu wangu huu mtandao wa YouTube unazingua sana; ukiangalia video kila baada ya sekunde kama 10 hivi inasimama kwa ajili ya "buffering" mpaka inaboa. Video ya dk. 15 itakuchukua hadi dk. 60.

Chadema watafute site nyingine kwa ajili ya ku-host hiyo online TV yao waachane na YouTube. Zipo site kibao za kulipia hela kidogo tu kwa mwaka.

Mkuu acha kutumia network zenye speed ya Kobe, Nina muda sana tangu Mara ya mwisho Kuona YouTube ikibuffer, upgrade bandwidth yako au tafuta provide wa ukweli.
 
Amechemka sana. Kiongozi wa siasa lazima uwe mvumilivu na mwenye kuchagua maneno ya kuongea. Kitendo cha kukiita kituo cha habari cha taifa ''kipeperushi cha CCM'' kinaonyesha dhahiri kuwa mheshimiwa huyu hana busara wala uvumilivu wa kisiasa. Sasa TBC wakigomea kutangaza habari za CHADEMA atamlilia nani sijui? Watu wengine bwana.

lool ...Nani alikuambia kuwa unahitaji TBC ili kutangaza sera za CDM, CDM ni self selling product huhitaji TBC kuuza product hii inajiuza yeyenywe mitaani na kila corner ya nchi, Fanya research ni watu wangapi wanaangalia TBC siku hizi then rudi hapa na bandiko lingine
 
kwa hivo kama chombo cha habari cha serikali kinapendelea kisiambiwe ukweli?
hajakosea kasema sahihi kabisa TBC haipo kwa ajili ya umama bali kwa ajili ya CCM huku wakitumia kodi zetu
mda wa kubembelezana umekwisha na hizi ni zama za ukweli
mm sio mwanasiasa na huwa sitazami wala kutembelea site ya TBC
hata TBC wasipotangaza na kwa vile wanapendelea zipo ITV,CHn ten na startv
usitake kutupeleka katika zama za ujamaa za kunyenyekea ili upate haki sasa ni wakati wa kudai haki

Amechemka sana. Kiongozi wa siasa lazima uwe mvumilivu na mwenye kuchagua maneno ya kuongea. Kitendo cha kukiita kituo cha habari cha taifa ''kipeperushi cha CCM'' kinaonyesha dhahiri kuwa mheshimiwa huyu hana busara wala uvumilivu wa kisiasa. Sasa TBC wakigomea kutangaza habari za CHADEMA atamlilia nani sijui? Watu wengine bwana.
 
Halafu kamati inakaa kusikiliza porojo za kufungiwa mwanahalisi, ulimboka kutekwa nyara. Haya yoote kwa jamii ni historia.
Hapo umesahau masuala ya walimu, askari kuua migodini na serikali kupewa asilimia 3 ya mapato ya madini, wizi wa mawaziri na watendaji wakuu wa serikali, pesa zilizofichwa kwene mabenki ya nje, kujilimbikizia ardhi na kuigawa kwa wawekezaji kama njugu, matatizo sugu ya maji na umeme, mfumko wa bei...na mengine mengi. Hayo unayoyaita historia kwa jamii, Mhe. Kikwete alishatangulia kusema kuwa Ni upepo tu, utapita.`

Ninachokuambia wewe ni kuwa hii si historia. Hawezi kuwa historia kwa mtu anayetafuta tonge ya ugali asiyo na uhakika nayo kutokana na mfumko wa bei na maisha magumu, haiwezi kuwa historia kwa mtu amabaye mgonjwa wake anakufa akijiona kwa sababu madaktari ama wamefukuzwa au hospitali hazina dawa na vifaa, haiwezi kuwa historia kwa yule ambaye ameweka kilo yake ya nyama kwenye jokofu baadaye inaoza kwa kukosekana umeme, haiwezi kuwa historia kwa kulala gizani siku na kutembea kilomita kadhaa kutafuta maji, haiwezi kuwa historia kwa mamaia kwa maelfu ya vijana waliobahatika kusoma na kuhitimu lakaini hawana ajira, wala haiwezi kuwa historia kwa mzazi ambaye mwanawe amefukuzwa shule kwa sababu hakulipa ada. Haya yote sio historia, ni maisha ya kila sekunde, dakika, saa, wiki, siku, miezi, miaka.... ndio maisha yetu kwa miaka 51 sasa, sio historia mkuu.

Hapana Mkuu wangu mmwaisoba, haya sio historia wala upepo wa kupita, ni upepo wa mabadiliko. Ushauri wa bure, sitokutoza hata senti moja: kama wewe umekalia tawi jembamba, shikilia vizuri, upepo unavuma kwa kasi.
 
Hotuba nzuri yenye uchambuzi wa kina juu ya udhaifu wa viongozi wa CCM na serikali yake.

Tunaomba CHADEMA wakiwa na vikao vya Kamati Kuu ku-posti video clips maana CHADEMA inasemea wananchi wanyonge na inaonyesha kuwa tayari kuchukua nchi 2015 na kuleta matumaini mema.
 
Ni kituko kwa chama kinachojiita makini kuruhusu mwenyekiti msanii msanii kama huyu mbowe na hotuba ya ajabuajabu iliyorushwa leo kwenye hii jamii forum. Inawezekanaje chama kumlalamikia rais kikwete eti kwa nini aliamua kwenda kampala kuhudhuria usuluhishi wa kongo na kuacha kwenda kumzika mwangosi. Lakini chama hicho hicho kililazimisha kwenda kwenye msiba na kukutana na professor mark mwandosya ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya rais. Kama chadema haaminiani ndo maana katibu wa chama anakwenda kufungua matawi vijijini tena kwa kulazimisha na kukataa kutii sheria pasipo shuruti. Halafu kamati inakaa kusikiliza porojo za kufungiwa mwanahalisi, ulimboka kutekwa nyara. Haya yoote kwa jamii ni historia. Watanzania tunamambo mengi ya kufanya kuliko haya ambayo chadema wanajidanganya kuwa ni matatizo. Inatia shaka kama hawana mkono kwenye hizi makala za mwanahalisi na migomo ya madaktari. Tunapata funzo gani kuhusu umakini wa hikichama?

Red: Sheria ipi? Hebu tuwekee hicho kifungu cha sheria hapa tuone kinasemaje?

Blue: Porojo? Una maana mwanahalisi halijafungiwa? Na Ulimboka hakutekwa wala kuteswa? Na unaposema hayo ni historia una maana gani? If you are brave enough nenda kamwambie baba mzazi wa Ulimboka (face to face) kuwa kutokwa kuteswa na mwanawe ni historia!

Purple: Mambo mengi muhimu kuliko uhai? Watanzania wanaishi kwa hofu, tena hofu kubwa ya kupigwa risasi/mabomu na polisi. Kahubiri hizi habari za mambo mengi muhimu kule Nyamongo, watakupa defination sahihi ya neno 'muhimu'.
 
Wakuu kwa uzoefu wangu huu mtandao wa YouTube unazingua sana; ukiangalia video kila baada ya sekunde kama 10 hivi inasimama kwa ajili ya "buffering" mpaka inaboa. Video ya dk. 15 itakuchukua hadi dk. 60.

Chadema watafute site nyingine kwa ajili ya ku-host hiyo online TV yao waachane na YouTube. Zipo site kibao za kulipia hela kidogo tu kwa mwaka.

Mkuu ndio kwanza nakusikia unasema kwamba youtube inasumbua, youtube ipo powa kabisaaa sema tu labda ni network zenu zipo slow me nimefungua bila tatizo kabisaa
 
Back
Top Bottom