VIDEO: Hotuba ya M/Kiti wa CHADEMA Taifa wakati akifungua Kikao cha Dharura cha Kamati Kuu

Mkuu heshima yako,
Naomba uwe specific ili tuweze kuchangia hoja yako kuhusu uelewa wa Mbowe. Inawezekana una point ila sisi hatujaelewa. Kumbuka mambo yafuatayo.
Mbowe hatoi kichwani peke yake ndo maana alitoa baada ya kikao, lakini hata hivyo yeye huwa anachanganya na zake pia.
Mafanikio ya Chadema yamepatikana ikiwepo kuzinduliwa kwa M4C yeye akiwa mkiti na katibu wake Dr Slaa.
Nina mengi ya kueleza lakini hebu fafanua hoja yako kwanza.
Heshima yako Aweda,
kwanza nikupongeze kuwa muungwana wa kwanza tangu CDM ianzishwe kwa umakini,hekima na busara ya hali ya juu uliyojaaliwa.Nadhani utakuwa ukishuhudia siasa za jazba zikichukua nafasi katika chama chenu iwe katika kutetea hoja,kuwasilisha ujumbe hata mikutano na wahandishi wa habari au ya hadhara kwa kisingizio kwamba wana uchungu.Kama utafuatilia kwa makini aliyoyasema Mh Mbowe inaonekana alikuwa anaongea hisia zake binafsi na hakuwa anakiwakilisha chama (au labda itakuwa hivyo kwa kofia ya uenyekiti) na hapo ndipo utakapogundua udhaifu wake katika kujieleza hususani pale watu wenye uelewa wa mambo ya siasa na uongozi wanapomsiliza kwani hajui wapi aongee nini na kwa mantiki ipi.Hakuna ubishi Mh mbowe anaweza kuwa mwanasiasa mzuri katika majukwaa na kupiga kelele lakini akawa anapwaya upande mwengine.Hivi kwa mfano suala la rais kutoa pole kwenye msiba nayo ni agenda ya kikao cha chama? au utaona jinsi anavyoshindwa kupanga maelezo yake ukajua ameanzia kwenye agenda gani na kumalizia vipi kama hitimisho au msimamo wa chama chake.Hivi labda nikuulize Aweda kama nje ya vikao udhaifu wake unakuwa hivi ndani ya vikao inakuwaje? Ushauri wa bure kwa CDM si kila suala la chama liongelewe na mwenyekiti ama katibu,chama kimeshakuwa kikubwa safu ya uongozi ipangwe na kufuata taratibu za kimamlaka na utendaji.Ukilaza wa Mh Mbowe haujifichi mbele ya kadamnasi ondoeni aibu hii.

Nawasilisha.
 
Mkuu hayo ni maneno ya majukwaani tu. Kwa hiyo hakutakuwa na mgombea mwaka 2015? Kama atakuwepo atakuwa ametengenezwa lini? Kuna siasa za ndani na siasa za majukwaa.
mkuu maneno ya majukwaani yapo ccm chadema vitendo ukiwa na ya majukwaani nje si umeona madiwani 2 wa mwanza hiyo ndio cdm
 
Back
Top Bottom