Video Games zimeniathiri mahusiano yangu

The patriot man

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
968
1,064
Wakuu kwema

Mimi nimekua mhanga mkubwa saana wa kucheza video games kwenye computer na PlayStation kutokana Mimi nimejiajiri mwenyewe so nakua na mda mwingii Sasa hii imepelekea mahusiano yangu na baby mama kuzorota maana Mimi nikisahakaa kwenye PlayStation huwa sielewi Tena Jambo lolote naweza kulala saa 10 saa moja naaamka naenda kazini

Hili Jambo linamkera saana anaona Kama simjali kumbe nampenda saaana juzi tumeachana kisa videogames.

Wala sijamtafuta akanitumia text leo asubuhii saana akaniambia nichague kucheza games au yeye nikamuambia yeye Ila ukweli ni kwemba sitoweza kuacha kucheza game maana shaathirika kabisa

Wadau nampenda na sipendi nimkere Ila ndo hvo siwezi kuacha

Week moja iliyopita nimeagiza ps5 online soon inakujaa daah. Niko dilema naombeni ushauri ili niweze kutetea penzi langu
 
Umenikumbusha movie ya Ted,

Nampa pole huyo mpenzi wako kwa kudate na mvulana, wa kupewa ushauri ni yeye, aidha akuvumilie hadi ukue au akuache,

Kama akikubali kukuvumilia na wewe jaribu kumshawishi azipende hizo games kwa kucheza pamoja ili mje kua kama mazombie humo ndani.
 
eti mazombie,hamjui tu utamu wa Games nyie,yani sisi wacheza games tunavozipenda ni kama wanywaji wanavopenda beer.nikicheza Games nahisi furaha na amani sana
 
kuna jamaa alikutwa na boss wake ofisini anacheza video games kwenye pc ilikuwa ni Fifa ,boss akafoka sana ila jamaa akasema haachi
 
Huu uzi ukisoma comments tu unajua Born Town na wakuja yaani playstation kucheza na umri vina relate vipi?
IMG-20201003-WA0009.jpeg
IMG-20201003-WA0011.jpeg
 
mkuu kwanini mnaamini wanaocheza games ni watoto ? Mimi namfahamu mzee fulani alikuwa na cheo kikubwa serikali ya awamu ya nne na alikuwa anacheza games nyumbani kwake akitoka ofisini na kuna uwezekano hata ofisini alikuwa anacheza
Namaanisha kuachana na mpenz wako kisa game n utoto
 
eti mazombie,hamjui tu utamu wa Games nyie,yani sisi wacheza games tunavozipenda ni kama wanywaji wanavopenda beer.nikicheza Games nahisi furaha na amani sana
Hujajua kama games ni mpango maalumu wa kufanya watu wawe kama zombies,

Mimi mtu hawezi nishawishi hata kidogo, kitu cha kuumiza akili yangu halafu i gain nothing hua sikipi nafasi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom