VIDEO: DC Mtatiro aanza kwa kishindo. Apiga marufuku unyago, atakayekaidi kukiona

Hiki ndio kipaumbele cha kwanza kukishughulikia , hakuna mchezo hata kidogo !
Umeandika kutaka kuonyesha kuwa amekosea lakini hujui tu... amefanya vizuri sana. Sijui uelewa wako kwenye haya mambo ya unyago kwa watoto lakini nikuambie tu ni utamaduni mbaya na uliopitwa na wakati na unatakiwa ukomeshwe kama ile tabia ya kukeketa.
 
DC kachemka

Alipaswa kusaidia kuboresha Elimu inayotolewa kwny Unyago sio kupiga Marufuku

Sio kila tulichorithi ni cha kupiga Marufuku, kuna vingine tunapaswa kuboresha kiendane na mazingira ya leo

Maendeleo sio lazima kuzika utamaduni wa Mwafrika completeley

Sasa hivi kuna Kampeni kubwa ya kuelimisha Watoto wetu Masuala ya Mahusiano kitu ambacho kingeweza kufanywa kupitia Unyago

Kuna Janga la Mapenzi ya jinsia moja, ubakaji, ulawiti n.k yote haya yameibuka zama hizi jee chanzo ni unyago?
 
Unyago ungeboreshwa ,nafundusho yaendane na wakati na sio kupiga marufuku, sijawahi pitia unyago lakini najua kuna mambo mazuri pia wanayofundushwa huko kama kufanya kazi, usafi,kupika,heshima nk
Yale yasiyofaa yafutwe na makungwi waelimishwe mm nadhani si utamaduni mbaya
Watu waliokuwa wanapitia unyago zamani walikuwa na umri mkubwa na wakitoka huko wanaolewa tofauti na sasa ni watoto wanaoenda unyago,
 
Mkuu kwenye swala la unyago nakupinga ni tamaduni safi ndo maana sikuhizi vijana wengi ndoa zao zinavunjika mapema kukosa elimu ya unyago afu unakuta binti mzuri anafanya mambo ya hovyo kwa kukosa elimu hiyo...kama hujui pia huko wanafunzwa kujistiri,kuongoza familia nk
Umeandika kutaka kuonyesha kuwa amekosea lakini hujui tu... amefanya vizuri sana. Sijui uelewa wako kwenye haya mambo ya unyago kwa watoto lakini nikuambie tu ni utamaduni mbaya na uliopitwa na wakati na unatakiwa ukomeshwe kama ile tabia ya kukeketa.
 
Back
Top Bottom