Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amevunja ndoa ya kinyemela ya kimila iliyokuwa imefungwa baina ya "Muddy Muuza Urembo" wa Tunduru Mjini na Binti aliyechaguliwa kujiunga na elimu ya Kidato cha Tano katika Shule ya Wasichana ya Masasi.
DC Mtatiro ameongoza vyombo vya usalama kuwakamata wazazi waliomuoza binti huyo pamoja na washenga waliohusika na akafanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa Muddy Muuza Urembo majira ya saa 6 usiku akiwa anaishi na binti huyu wa shule kinyumba kwenye Kijiji cha Muungano, Tunduru Mjini.
Mzazi wa binti amekiri kumuoza binti huyo kwa mahari ya shilingi 30,000 kwa madai kuwa binti hakuwa tayari kuendelea na kidato cha tano.
Hata hivyo, DC Mtatiro alivyomuhoji binti huyo, binti alikiri kutaka na kupenda kuendelea na masomo yake ikiwa atapewa nafasi hiyo.
Mtatiro amemkabidhi binti huyo kwa taasisi inayolea na kufadhili wanafunzi wilayani Tunduru iitwayo KALAMU EDUCATION FOUNDATION (KEF) ili ihakikishe msichana huyo anaendelea na masomo.
Makamu Mwenyekiti wa KEF ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Masonya Wilaya ya Tunduru, Bwanali amekiri kupata taarifa kuhusu binti huyo na kuahidi kuwa taasisi yao itamsimamia.
Mtatiro amesisitiza binti huyo atasimamiwa aendelee na masomo yake na kuendeleza ndoto yake na amewaasa Wazazi wa Tunduru kuachana na mambo ya zamani ya kuoza mabinti ambao wana nafasi ya kuwa na mchango mkubwa zaidi kwa Taifa.
Watuhumiwa watano kwa jumla wanashikiliwa na Polisi wilayani Tunduru wakiendelea kuhojiwa juu ya kula njama na kumuoza binti huyo.
Pia soma Ruvuma: Wazazi waliomuozesha mwanafunzi kwa Tsh. 30,000 waomba radhi