Katavi: Chongolo, amebaini kusimama Kwa mradi wa skimu ya umwagiliziaji kutokana na uchakavu wa miundombinu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,116
49,840
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ,(CCM), Daniel Chongolo, amebaini kusimama Kwa mradi wa skimu ya umwagiliziaji kutokana na uchakavu wa miundombinu uliokithiri, mradi huo upo katika Kata ya Ugalla Kijiji cha Katambike, mkoani Katavi.

Chongolo amesema mradi huo haufanyi kazi tangu mwaka 2007, hivyo ataongea na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu mradi huo ambao inatakiwa ufanyike usanifu wa kina unaoendana na mazingira husika ili upatikane mradi ambao utakua endelevu na wa uhakika.

Kwa hili Bw.Chongolo Katibu Mkuu wa CCM nakupa pongezi sana,umekuwa unaenda maeneo ambayo Mawaziri mnaowateua hata Wakuu wa Mikoa au DC Huwa hawafiki.

Tumewahi enda Chocho Fulani kwenye miradi ya Serikali ndani kabisa kwenye Wilaya yaani ndio ilikuwa mara ya kwanza Kwa DC kufika anashangaa harafu anaona ni mateso na kudai hatorudia tena maana mazingira ya kufikika sio salama.

Sasa viongozi wa dizaini hiyo ndio wamekaa Tzn ,kazi Yao kubwa na kuzunguka kwenye Bar Mjini lakini Huwa hawapendi maeneo yenye Changamoto kutatua kero.

Just imagine huko uliko ni ndani sana hata RC hajui na hana Mpango wowote wa ku push mradi ila wewe umefika.

My Take
Shida yenu huko ccm mnapeana madaraka Kwa kujuana sana ndio maana hakuna Cha maana wanafanya walio wengi kuanzia Mawaziri,RC na DC.
 
Kiukweli katibu mkuu wetu ni mchapa kazi sana na anajituma sana katika kazi. Naamini mwenyekiti wetu Taifa na Rais wetu atamuunga mkono katibu wetu kwa kuwachukulia hatua wale wote watakaoonekana kutoendana na kasi yake, pamoja na matarajio ya chama katika utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi ambayo ufanisi wa utekelezaji wake ndio upatikanaji wa maendeleo kwa Taifa letu na Tabasamu kwa watanzania.
 
Too late mkuu.

CCM imetufikisha hapa.

CCM haiwezi kutunasua kutoka kwenye mkwamo iliyoujenga na kuusimika na kuusimamia miaonvo yote hii.

Hizi cheap politics zinaenda kukwama
Kwa hiyo unataka nani atuvushe?
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Godfrey Chongolo leo Ijumaa Oktoba 6, 2023 amekagua Skimu ya Umwagiliaji ya Ugalla katika Kijiji cha Katambike, wilayani Mpanda, ili kuuwekea mpango wa kuukwamua, baada ya mradi huo kukwama tangu 2007.

Ndugu Chongolo amefanya ukaguzi wa skimu hiyo iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 800 wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika Halmashauri ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.

Akizungumza na wananchi wa maeneo ambao ndiyo walikuwa walengwa na wanufaikaji wa Skimu ya Umwagiliaji hiyo inayotegemea maji ya Mto Ugalla, amesisitiza kuwa mradi huo unapaswa kufanya kazi ili wakulima wa maeneo hayo waendelee kufanya kilimo na kuzalisha zaidi ya sasa, ambapo amesema atamuita Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ili kupata mpango wa wizara katika maeneo hayo ukoje, kwa ajili ya uukwamua mradi huo uliokwama kwa miaka 16 tangu uanzishwe.

"Mradi huu wa skimu ya umwagiliaji umekwama tangu mwaka 2007. Zinatajwa tu fedha hapa, ziliingia zikaingia, lakini watu wanawashangaa kuwa hizo fedha zilienda wapi? Nitakwenda kuzungumza na Waziri mwenye dhamana na Kilimo ili aone namna ya kuukwamua mradi huu ambao tija yake ni kubwa endapo utafanya kazi,

Akiwa katika eneo hilo Chongolo amesisitiza kuwa mradi huo inatakiwa ufanyike usanifu wa kina unaoendana na mazingira husika, ili upatikane mradi ambao utakua endelevu na wa uhakika.
 
Back
Top Bottom