Video Clip: Alichokisema Mhe. Joshua Nassari huko Kigoma

Uanagenzi.

Kitendo cha kuanza ku tout "rais wa Tanzania atatoka Kigoma" tayari ni kupanda mbegu ya mgawanyiko, regionalism.

Wa Tanga tukisikia hivyo hata kama hatukuwa na mawazo kama hayo tutaanza kufikiri "Eboo, kweli ee? Sisi wa Tanga hatujawahi kutoa rais Tanzania hivoo?". Tayari mgongano usio na haja.

Huyu ndiye yule dogo anayesemwa alitaka kuikata sehemu ya kaskazini Tanzania iwe nchi mpya? Maana kama ni hivyo inaonekana ana ki element cha kuibagua nchi kwa mikoa kwenye DNA inawezekana.

Kwa nini kiongozi yeyote aliyekomaa kupanda mbegu hii ambayo zao lake ni utata kama si sumu?

Rais wa Tanzania anatoka Tanzania, and that's what matters, huko kwingine tutaangalia uwezo, sio mkoa.

Hapa labda aniambie alikuwa anafanya show ya siasa rejareja na propaganda za ku connect na wananchi kwa kutumia least common denominator, sawasawa na walivyokuwa wana dansi pale.

Lakini ukitafuta kauli iliyokomaa kisiasa haipo.
kwa hiyo kigoma sio tanzania? na kigoma hawako wnye uwezo? tatizo liko wapi? kwa sababu lazima rais atoke sehemu mojawapo ya tanzania, inaweza ikawa iringa, singida, tabora, mjini magharibi..popote tanzania kuna kosa gani kutaja eneo wewe chura?
 
kwa hiyo kigoma sio tanzania? na kigoma hawako wnye uwezo? tatizo liko wapi? kwa sababu lazima rais atoke sehemu mojawapo ya tanzania, inaweza ikawa iringa, singida, tabora, mjini magharibi..popote tanzania kuna kosa gani kutaja eneo wewe chura?

Kigoma ni Tanzania, lakini hatuchagui rais kwa sababu katoka Kigoma au Morogoro. As far as geographical location is concerned, kinachomatter ni kwamba rais anatoka Tanzania.

Kiongozi wa kisiasa ukishaanza kusema "rais ajaye atatoka Kigoma" unakuwa ushaanza kupanda mbegu ya kuwatenga Watanzania kwa mikoa.

Watu wa mikoa mingine nao wataona "mbona na sie hatujapata nafasi hii?" inaanzisha zogo kama la Goodluck Jonathan alivyotaka kumrithi Yar'Dua huko Nigeria kwa sababu wana upumbavu huu wa "rais akitoka kaskazini, anayemfuatia atoke kusini"

Hii ni habari ya upumbavu wa regionalism, haiko mbali na ukabila.

Mtu makini hakutakiwa kufagilia kitu kinachowagawanya Watanzania, bali kinachowaunganisha.
 
Zito hana tofauti kubwa sana na Nape, Tena Nape amemzidi kwa mbali coz at least Nape anawaheshimu viongozi wake hasa pale kwenye maslahi ya chama!!!
 
Zito hana tofauti kubwa sana na Nape, Tena Nape amemzidi kwa mbali coz at least Nape anawaheshimu viongozi wake hasa pale kwenye maslahi ya chama!!!

Mkuu wapi zitto amewadharau hao viongozi wake? mbona hamtaki mawazo mbadala?
 
Hii mbona iko clear...

Kwani Kigoma yuko Zitto peke yake? Anaweza akawa Kafulila, Zitto au Eng Chiza.
Na inaweza nikawa mimi vilevile....kwani rahisi huyo si lazima awe miongoni mwa wanasihasa mnaowafahamu kwa sasa.
 
Hata mimi ningekuwa Zitto,ningefikiri hivyo hivyo kuwa ninafagiliwa kugombea urais.Hata yeye alishangazwa,na nimeona impression kama amesema "woow" Yani kwamba hata yeye alishtushwa na kauli ile.Pengine kosa liko kwa gazeti la mwananchi kumlisha maneno Mh Nassari.Hivyo hapa sioni kosa la mh Zitto hata kidogo.Issue ni kweli imekuzwa,lakini hakuianzisha yeye,unless tuhuma za yeye na Semtawa ni za ukweli.
 
Ni aibu sana kwa Zitto Kabwe ambaye ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni! Umethubutu kusema kuwa, kilichoandikwa na Mwananchi ndicho kilichosemwa na Nassari, ona sasa clip uliyosema itaeleza kila kitu, inavyokuumbua!


nilimwambia zitto kuwa anamtumia ramdhan semtawa katika kuandika makala za kichonganishi ..akaruka futi mia

zitto kabwe ndo kai upload youtube!!

Mkuu Edson, sasa naanza kuamini unachosema. Naona ni kama mwandishi alitaka kuona mtazamo wa watu na hivyo akatia nakshi hiyo habari (zile bahasha alizozielezea Pasco zinaweza kuhusishwa hapa)

Katika hili nina maswali:
Je, alitaka kuona mtazamo wa watu juu ya Zitto kuwa rais kwa manufaa ya nani?!
Na Zitto kwa nini aamue kuleta clip hii?! ina maana hakujua kuwa inapingana na yeye kuunga mkono walichoandika Mwananchi?!

Mawazo yangu:
Nadhani Zitto amekua na ujasiri wa kuweka hiyo clip ili watu waone kuwa hahusiki katika yaliyosemwa na mwananchi japo aliyasapot kunogesha mjadala ama aliyasapot kwa kulewa sifa (ile kuona japo amefikiriwa kuwa anafaa kuwa rais).
Ama labda hakuwa amelisoma hilo gazeti na akaunga mkono hoja kwa ule mtindo wa "wanaokubali waseme, 'ndiooooo?!' kutokana na kujivunia weledi na rekodi ya gazeti hilo?!
Either way, kwa kuwa wanasiasa wanapenda kufanya vichwa vya magazeti, so amepata alichotaka.


 
Zitto is very strategically ila kuna sehemu nyingine anakoroga hapo hamna uhusiano kabisa kati ya alichokisema Nassari na kilichoandikwa na gazeti la mwananchi. Zitto tuliza nyago uraisi siyo kirahisi hivyo jipange sawasawa ushauri wangu tu huo.

Unatudanganya na kucheza na vichwa vyetu kama sisi wendawazimu watu sasa hivi wako makini na tuna taarifa zote.moja tu nalolikumbuka ni wewe kuita press conference na kutangaza kugombania ubunge wa kinondoni uchaguzi ukliopita then ukaaacha ukaenda kigoma mbona hukusema kama hutagombania tena.

Jipange urahisi una uwezo mkubwa tu ila usipende sana kutumia vya habari kujikuza,fanya kazi kama tunayoiona mbona ukifika wakati wa urahisi utapita tu kumbuka Tanzania ya mwaka 2010 siyo hii ya 2012.M4C
 
Hivi inaingia akilini kwa wabunge wote hawa kuacha kushiriki kikao cha bunge, wakenda kujionyesha hadharani kwenye "promotion" ya Kigoma (kuwa hawana udhuru usioepukika), huku spika wa Bunge na Makatibu wake, wakijua?

Kweli sisi tuwazima?
 
Mi nafikiri Nasssar alichanganywa na ule umati na alikuwa anajua hadhira ya WanaKigoma inataka kusikia nini bila kujali walio nje ya Kigoma wangesemaje!! Si unajua Wanasiasa wengi wanabadilika kutokana na mazingira?? Kwa mfano msikilize Filikunjombe nae yeye ndio alimaliza kabisaaa!! www.chadema.tv
 
Kigoma ni Tanzania, lakini hatuchagui rais kwa sababu katoka Kigoma au Morogoro. As far as geographical location is concerned, kinachomatter ni kwamba rais anatoka Tanzania.

Kiongozi wa kisiasa ukishaanza kusema "rais ajaye atatoka Kigoma" unakuwa ushaanza kupanda mbegu ya kuwatenga Watanzania kwa mikoa.

Watu wa mikoa mingine nao wataona "mbona na sie hatujapata nafasi hii?" inaanzisha zogo kama la Goodluck Jonathan alivyotaka kumrithi Yar'Dua huko Nigeria kwa sababu wana upumbavu huu wa "rais akitoka kaskazini, anayemfuatia atoke kusini"

Hii ni habari ya upumbavu wa regionalism, haiko mbali na ukabila.

Mtu makini hakutakiwa kufagilia kitu kinachowagawanya Watanzania, bali kinachowaunganisha.
hao wa mikoa mingine unayosema ndio wamekutuma uwasemee? jisemee wewe na hisia zako za ubaguzi, unaposema atatoka tanzania tanzania inaundwaje kimaeneo? na hasa tukiwa tunaongea sisi kwa sisi nchini mwetu..uwezi sema atatoka tanzania wakati wewe ni mtanzania na unajua tanzania inaundwa na mikoa,wilaya,tarafa,kata na vijiji rais lazima atoke moja ya eneo la tanzania tena kwa jina la eneo, acha kishi kwa hisia tena zile potofu, all the time unahisi mabaya tu, kwanini usihisi kuwa wapo watanzania wengi tu watafuahi kam rais atatoka moja ya vijiji vya wilaya ya mkalamo, singida?
 
Mi nafikiri Nasssar alichanganywa na ule umati na alikuwa anajua hadhira ya WanaKigoma inataka kusikia nini bila kujali walio nje ya Kigoma wangesemaje!! Si unajua Wanasiasa wengi wanabadilika kutokana na mazingira?? Kwa mfano msikilize Filikunjombe nae yeye ndio alimaliza kabisaaa!! www.chadema.tv

Hili ni tatizo kubwa sana, kuanzia rais, PM mpaka wabunge.

Yaani mtu anakuwa kama anajisahau kwamba hapa naongea na hawa watu lakini kuna mi camera na wanahabari watani quote na kuandika magazetini.

Inakuwa kama mtu anaongea na watu wa pale tu.

Very myopic.
 
Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015
Monday, 23 July 2012 08:18
digg

0000000kabwe.jpg
Mbunge Zitto Kabwe


NI JOSHUA NASSARI WA CHADEMA, DEO FILIKUNJOMBE WA CCM, WASEMA KIGOMA WAJIANDAE KUTOA RAIS

Anthony Kayanda, Kigoma na Fred Azzah Dar

IKIWA imebaki miaka mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini mwaka 2015, wabunge wawili vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo.

Kauli za Wabunge hao zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea huku kukiwa na uwezekano wa umri wakugombea urais kushuka hivyo kuwawezesha wanasiasa wengi vijana akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo.

Wakizungumza katika tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma, Deo Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua Nasari wa Arumeru Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema), walisema wanaamini Rais wa 2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na ambaye ni mzaliwa wa mkoa huo.

Katika kauli yao hiyo, wabunge hao walisema Mbunge huyo ameonyesha umahiri mkubwa katika kusimamia mambo ya kitaifa bila upendeleo, jambo linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hivyo kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa hili.

Akimzungumzia kuhusu rais ajaye kutoka Kigoma, Filikunjombe alisema kundi la vijana lazima liungane kuhakikisha kuwa linatoa viongozi watakaopigania maslahi yao na Taifa kwa jumla ili kuleta ukombozi wa kifikra na kimaendeleo kwa maslahi ya jamii.

"Lazima mtambue kuwa, Tanzania ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba tunaweza kufanya makubwa katika kuleta maendeleo ya jamii katika nchi yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:

"Vijana wa Kigoma mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka michache ijayo lazima mkoa huu utoe Rais wa Tanzania."

Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini hapa kuhudhuria tamasha hilo lililopambwa na wasanii nyota wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma, Filikunjombe alisema; "Zitto anastahili kuwa rais".

Mbunge huyo wa CCM ambaye katika siku za karibuni ameonekana kuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa Zitto na Chadema, alisema Zitto anafaa kuwa Rais kwani amefanikiwa kuwaunganisha watu na kuleta umoja miongoni mwao, jambo ambalo linadumisha umoja wa kitaifa.

Kauli ya Nassari
Kwa upande wake Nasari, alisema Mkoa wa Kigoma umejitokeza wazi kuwa na wanasiasa mahiri na wenye vipaji vya hali ya juu katika kupigania maslahi ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi unaodidimiza uchumi wa taifa letu na kuwanufaisha wachache kwa kutumia nafasi zao.

‘Leo, ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona mpangilio mzuri wa shughuli hii,
naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nasari.

Huku akishangiliwa na mamia hayo ya wakazi wa Kigoma, alifafanua kwamba wanasiasa vijana wamejipanga kuwatetea wananchi na hususani kundi la vijana katika kuondoa matatizo mbalimbali yanayowasibu katika maisha kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao za uzalishaji mali.


Mdee amliza Zitto
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) alimliza Zitto jukwaani baada ya kumuelezea kuwa ni ‘jembe' katika mambo mbalimbali na mtu mwenye uchungu na maendeleo ya taifa.

Mdee aliyepewa nafasi ya kuwasalimia Wananchi alisema amekuwa na Zitto tangu Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kwamba kutokana na ujasiri na umahiri wake katuika kutetea masilahi ya wanyonge na taifa, anafaa kuwa mmoja wa viongozi wa juu katika Taifa.

‘Ndugu zangu watu wa Kigoma, kwa kweli mna bahati sana, achilia mbali kuwa na vipaji katika sanaa ya muziki na michezo hasa mpira wa miguu, lakini mna wanasiasa wakali ambao ni tishio hapa nchini. Mimi namkubali sana Zitto Kabwe na ninaamini kuna siku atakuwa kiongozi wa juu katika nchi yetu," alisema Mdee.

Mdee alipongeza ushirikiano wa wananchi wa Kigoma na kusisitiza kuwa unatakiwa kuenziwa na kuigwa na mikoa mingine.

Zitto akiri kutoa machozi

Zitto alipulizwa na gazeti hili alikiri kudondosha machozi jukwaani kutokana na Mdee kuzungumza kwa hisia kali na hivyo maneno yake kumchoma na kushindwa kujizuia jukwaani.

" Kwa weli Halima Mdee aluzumgumza maneno mazito sana na alinikumbusha mbali enzi za Chuo kikuu tukiwa kwenye harakati za kutetea maslahi ya wanachuo na pia nimekuwa naye kwenye harakati za kisiasa ndani ya Chadema, ndiyo maana nilishindwa kujizuia na kuanza kutoa machozi," alisema Zitto.

Alisema amefarijika kuwaona wabunge wenzake kutoka vyama vya CCM, NCCR Mageuzi, Chadema na CUF wamefika Kigoma kumuunga mkono katika uzinduzi wa wimbo wa 'Leka dutigite' ulioimbwa kwa pamoja na wasanii wa muziki wenye asili ya Kigoma.

Zitto alisema Mkoa wa Kigoma kwa muda mrefu umekuwa nyuma kimaendeleo hivyo, kuufanya kudharauliwa na watu wengi hata kama hawajui lolote juu ya eneo hilo.

‘Wapo watu wanaotubeza kwamba mkoa wetu ni masikini na haufai kuishi, na kasumba hii imejengeka hadi kwa baadhi ya watumishi wa Serikali. Ndiyo maana sishangai ninaposikia kwamba kuna watumishi wa Serikali wanakataa kuhamia Kigoma. Lakini hii dhana sasa itaisha," alifafanua Zitto.

Wabunge waliohudhuria

Wabunge waliofika Kigoma kwenye hafla hiyo ni Mdee , Amina Mwidau wa viti maalumu (CUF), Esta Bulaya ( Viti maalumu (CCM), Filikunjombe (CCM), Kangi Lugola wa Mwibara, David Kafulila (Kigoma Kusini, NCCR-Mageuzi), Nasari (Arumeru Mashariki Chadema) na Raya Ibrahim Khamis wa viti maalumu kutoka Pemba.

Kauli ya Nape
Alipoulizwa Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye kuhusu Filikunjombe kumtabiria Zitto kuwa Rais wakati anatoka upinzani, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hajasikia wala kulisoma popote.

"Nyie andikeni kwanza halafu ndiyo nitaweza kusema, kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu sijasikia kitu chochote ama kusoma popote pale jambo hilo," alisema Nape.
 
Back
Top Bottom