Video: Angalia jinsi huyu askari alivyokosa utu

Hizo bidhaa anazozipiga mateke,wahusika watazikusanya na kuwauzia wateja wao,hatari sana kiafya,
Hii ni kufuru kubwa sana anayoifanya huyo Askari hata kama hao kina Mama wamekosea kwa kuuzia hapo.
 
Maskini huwa tuna lawama sana. Tunalazimisha kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa tukiambiwa tuondoke hatutaki. Mabadiliko hayaji kwa kubembelezana
 
Kuna baadhi ya maaskari ni miyeyusho, yani ameshindwa kutumia busara kuwaambia waondoke kweli?

View attachment 2926351

SIJUI NI NCHI GANI HII.
Kuna mambo mengine tusilaumu tu kabla hatujayajua kiundani,
Hapo huenda haparuhusiwi biashara, huenda na tangazo kabisa lipo hapohapo lakini utakuta watu wanajifanya kichwa ngumu wanaenda kufanya biashara hapo alafu yakitokea hayo wanaanza kulalamika hawana utu.

Ukija leo ukawaambia kwa upole, kesho yake wanarudi tena wakiamini hawezi kutufanya kitu.
Kuna mambo mengine ukifuata sheria haya mambo hutakumbana nayo.

Shida watu ni wakaidi sana, mpaka utumie nguvu ndio wanaelewa.
 
Kuna jirani yangu kila mwaka TANROADS wanamwambia usilime kwenye hifadhi ya barabara. Jamaa hasikii, mwaka hu wamesubiri mahindi yamekuwa vizuri wakafyeka shamba zima. Akaja kutoa dukuduku kwangu nikamchana, hayo ni ya kujitakia
 
Siyo poa kwa uoga walio nao hao wamama kiasi cha kuharibu bidhaa zao na hawamshambulii angesema tu waondoke nafikiri wangeondoka
 
Kuna mambo mengine tusilaumu tu kabla hatujayajua kiundani,
Hapo huenda haparuhusiwi biashara, huenda na tangazo kabisa lipo hapohapo lakini utakuta watu wanajifanya kichwa ngumu wanaenda kufanya biashara hapo alafu yakitokea hayo wanaanza kulalamika hawana utu.

Ukija leo ukawaambia kwa upole, kesho yake wanarudi tena wakiamini hawezi kutufanya kitu.
Kuna mambo mengine ukifuata sheria haya mambo hutakumbana nayo.

Shida watu ni wakaidi sana, mpaka utumie nguvu ndio wanaelewa.
Mkuu hapa issue sio kwamba tunalaumu kwa Askari kucwachukulia hatua hao wafanya biashara bali lawama ni kwa aina ya hatua aliyoichukua ya kupiga mateke hayo matunda,unaona hivyo ni sahihi? hakukua na njia nyingine ya kiutu zaidi ya hiyo?
 
Kuna kipindi sisi tulikua tunafanyia kazi maeneo yasio ruhusiwa na halmashauri kwa kuweka meza ndogo za uwakala, jamaa walikua wakija tunakimbia na meza zetu ukiacha wanaivunja.

Lkn tulikua hatulalamiki maana tunajua haya mazingira hayaruhusiwi ila tunaforce kwa sababu ya maisha
 
Mkuu hapa issue sio kwamba tunalaumu kwa Askari kucwachukulia hatua hao wafanya biashara bali lawama ni kwa aina ya hatua aliyoichukua ya kupiga mateke hayo matunda,unaona hivyo ni sahihi? hakukua na njia nyingine ya kiutu zaidi ya hiyo?
njia sahihi kuchukua hatua ni kuwahimiza wabebe bidhaa zao na kuondoka.

hatujui waliishaelezwa hilo kwa muda gani.
 
Back
Top Bottom