Video: Angalia Bodaboda alivyogongwa na Mwendokasi

Umetumia hisia hapa,ila ukweli ni kwamba dereva wa mwendokasi hapo hana makosa
mkuu hisia gani kwani ile intersection anatakiwa aiheshimu bodaboda peke ake na ndicho wanachofundisha driving school, bodaboda wana hatia kila ajali ikitokea na mbele pale uelekeo wa mwendokasi pana pundamilia kivuko cha watembea kwa miguu unataka unambie yule mwendokasi alipaheshimu, sawa mimi nimesema madereva wa mwendo kasi bila kutumia utu hadi anastaafu ashaua bodaboda 20, miundombinu yetu sio salama.
 
Mwendo Kasi Hana kosa Wala hastahili lawama!.
Huyo bodaboda ni kama kajiua mwenyewe!
Tatizo la bodaboda wengi hawajaenda driving schools kwahiyo wanachojua ni kuvuta moto na kupangua gia tu kama vile wapo majangwani ambapo hakuna watumiaji wengine wa Barbara. Sheria za usalama barabarani zinakataza mtu kuendesha chombo Cha moto akiwa amelewa au akiwa na uchovu mwingi unaoweza kumsababishia usingizi akiwa barabarani lakini naamini wapo bodaboda wanaokunywa hizo K Vanti na vilevi vingine wakiwa kazini hapo wanaweza gongwa hata na malori sio lazima mwendo Kasi.
bosi nani kamalaumu dereva wa mwendokasi nimesema watumie busara na utu, sababu hii miundombinu ya treni za mataili ina mapungufu usiiishie kumsema bodaboda utakuta huyo boda siku nzima anafanya kazi akili inachoka msiishie kuwalaumu hawa watu ni ndugu zetu wametoka kwenye familia zetu eti pombe, nani hanywi pombe madaktari au kwani hawafanyi upasuaji.
 
Hawa ndugu zetu boda boda
🤔🤔🤔🤔🤔🤔
Boda ni watanzania Wenzetu, baadhi yao, na wenzao bajaji, sioni kama ni wakuhurumia, wao wanajari kuwahi kuliko Usalama wao na wa wenzao barabarani.
.
.Juzi nipo kwenye kigari changu, kwenye kituo cha daladala nimepungaza mwendo, akaja kukivaa kigari changu, nyuma, gari imebondeka sana bampa na shavu la kushoto, maana alipoanguka pikipiki iliilaria gari.

.Ila kwa saidiwa na boda wenzi, walinyua pikipiki chapu akakimbia, bodaboda wengine wakabaki wanacheka na kebehi, hii haina kesi hii. Nikaona uzuri wa kutotembea na silaha mda mwingine, maana shetani alishanituma vibaya pale.
.
.
 
Bodaboda ni risk, lakini kuna maeneo ambayo risk zaidi kuliko maeneo mengine.

Mfano mjini kati(kariakoo, Posta) ndio balaa sana.

Juzi nilipanda Boda hapo mataa ya Gerezani anitoe Argentina, Daah alivyowasha moto akapita njia ya mwendokasi mimi rohoni nikawa najisemea leo nimepanda mtumbwi wa vimbwengo. Nashukuru alinifikisha salama, ila ile speed sio poa
Kwanini usimwambie apunguze speed au alikupa lift ukaogopa kusema??
 
SIa
-hawa madereva wa mwendokasi wanahitaji busara na utu sana wakiwa city center
-hawa bodaboda nao wanafamilia wanapigania mkate viongozi wetu wakuweka sawa haya mambo wao full ac huko
-miundombinu yetu sio ya kueleweka sisi tuliobadilisha vichochoro kua barabara tunatesana tu
-ila nchi hii laana tu yani kama tumeshindwa kuweka vizuizi kwenye railway itakua mwendokasi mbona kama najitesa kutoa ushauri mlaaniwe wenye mamlaka pateni utajiri lakini mlaaniwe kuku nyie

MADEREVA WA MWENDOKASI ACHENI UHURU KUJIONA MKO NDANI YA TRENI MIUNDOMBINU YETU INAINGILIANA SANA BILA VIZUIZI VYOVYOTE SERIKALI ACHENI KULALA KUNGEKUA NA KIZUIZI PALE TENA CHA GATE BODABODA ANGESIMAMA MNANUNUA MAGARI YA KIFAHARI TU NYAU NYIE

-NAAMINI KUIBADILISHA NCHI HII KAMWE USITEGEMEE CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA NI LAZIMA ITOKE NDANI YA MTU MMOJA AJITOLEE MAISHA YAKE KWAAJILI YA NCHI HAWA MAFISADI HAWA KUPITIA VYAMA HAMNA KITU
SIJAKUELEWA KOSA LA MWENDO KASI NI LIPI HAPO, HILI NENO TUAACHE WANATAFUTA MKATE, TUAACHE NI WAPIGA KURA, NDILO LINALOHARIBU MAMBO MENGI.
KUTOKANA NA TABIA HII, NDIYO MAANA WATU WANAFANYIA BIASHARA BARABARANI, BODA BODA WENYEWE NA WENZAO BAJAJI, KUNA MAENEO WANASUBIRIA ABIRIA NDANI YA BARABARA.
MFANO: UKITOKA UBUNGO KWENDA KIBAHA, STOP OVER, KIMARA SUKA. TEMBONI, OFISI ZA MKUU WILAYA UBONGO, NIMEPASAHAU JINA, KIBAMBA CHAMA.

HIVYO VITUO DALADALA ILA BODA NA HASA BAJAJI HUFANYA VITUO VYA KUANZIA KAZI.

UKIJA MBAGALA PALE ZEIKEM KIMEKUA KITUO CHA BAJAJI, MBAGARA HAPO HAPO UKITOKEA KONGOWE, PALE DARAJANI BIASHARA ZINAPANGWA BARABARANI KABISAA, NI BARABARA YA NJIA MBILI ILA INATUMIKA MOJA, NYINGINE INAPANGWA BIASHARA.
WAACHWE SABABU WANATAFUTA MKATE, WAACHWE SABABU NI WAPIGA KURA, SIKU AJALI IKITOKEA TUWALAUMU MADEREVA.
 
Mwenyewe nilikuwa naangalia hali ya usalama mbele, endapo ningeona hali ya hatari ningemshtua fast.

Pia nilitaka kufika mapema nilikokuwa naenda
Kwa scenario kama ya hiyo ajali unadhani abiria na dereva wake hawakua wanaangalia hali ya usalama??

Ajali mara nyingi huwa haionekani ni vuup chuma iko down watu mshafikia tamati ya maisha yenu.

Sasa wewe hiyo kusubiri uone hatari ndo umstue na ukimstua na yeye akubali au akate huo ushauri wao si tayari mko mochwari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom