Video: Abiria wataharuki angani wakati ndege ya etihad ilipopata hitilafu leo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
etihad1-723x334.jpg

Mapema asubuhi ya leo ndege ya Etihad namba EY 474 toka Abu Dhabi kwenda Jakarta Indonesia ilipata hitilafu angani. Abiria 31 wamejeruhiwa huku 9 kati yao wakiwa na hali mbaya zaidi. Chini ni video ya hali ilivyokuwa ndani ya ndege wakati wa dhahama hiyo.

Shuhudia mwenyewe kwenye video hii

My take: Sisi wanadamu tujifunze kukumbuka imani zetu kila siku sio mpaka ukutane na taharuki
 
Mkuu Malcolm05 nimekupata unamaanisha hawana matumaini mwisho wao ukifika?
Hii sehemu ya Indonesia,Malaysia,Thailand Ina dhoruba kali
sehemu nyingine yenye dhoruba kali Ni Atlantic maeneo ya kuanzia Brazil, Venezuela mpaka Bermuda tri angle
sehemu zote hizi ndio zimesababisha maafa mengi,ikiwamo air France,ndege za jeshi la marekani na Malaysian airlines.
Tukumbuke kumwomba Mungu ulinzi wake kabla,wakati na baada ya safari na tuwe na imani na kuomba sio kulia na kukosa matumaini.
ddhoruba Ni nguvu za giza ndio maana zinaleta maangamizi, ki geographic utaona Ni upepo au mawingu ya kawaida lakini Kuna zaidi.

Hiyo juu Ni clip ya British airways inatoka Buenos Aires(Argentina) inakwenda London.
wamekumbana na dhoruba ya atlantic
 
...
Hii sehemu ya Indonesia,Malaysia,Thailand Ina dhoruba kali
sehemu nyingine yenye dhoruba kali Ni Atlantic maeneo ya kuanzia Brazil, Venezuela mpaka Bermuda tri angle

....
ddhoruba Ni nguvu za giza ndio maana zinaleta maangamizi, ki geographic utaona Ni upepo au mawingu ya kawaida lakini Kuna zaidi.

Hapo kwenye green nakubaliana na wewe. Eneo lingine ambalo at least limewahi kunikumba nikiwa angani ni kuanzia India kuelekea mashariki hadi kuvuka mpaka kuingia China. Hilo eneo usiombe kusafiri nyakati za pepo na mvua za monsoon; ndege inaweza kurushwa juu halafu ikadondoka chini huku radi za ajabu zikinguruma na mwanga mkali wa radi ukitanda ndani ya ndege. Salama yenu ikutane na wingu zito la kuizuia isidondoke jumla. Pamoja na ukubwa wa lile "pipa" liligeuka kuwa particle mbele ya nguvu zile za asili.

Hapo kwenye red sijakusoma Mkuu. Nijuavyo "nguvu za giza" ni mambo yanayohusiana na uchawi, mashetani, ushirikina, kuzimu, n.k. Kwamba dhoruba ni mambo ya jinsi hiyo? Sivyo.
 
etihad1-723x334.jpg

Mapema asubuhi ya leo ndege ya Etihad namba EY 474 toka Abu Dhabi kwenda Jakarta Indonesia ilipata hitilafu angani. Abiria 31 wamejeruhiwa huku 9 kati yao wakiwa na hali mbaya zaidi. Chini ni video ya hali ilivyokuwa ndani ya ndege wakati wa dhahama hiyo.

Shuhudia mwenyewe kwenye video hii

My take: Sisi wanadamu tujifunze kukumbuka imani zetu kila siku sio mpaka ukutane na taharuki

Mkuu ilikuwa hitilafu au Ndege ilikumbana na hali mbaya ya hewa? (Turbulence)
 
etihad1-723x334.jpg

Mapema asubuhi ya leo ndege ya Etihad namba EY 474 toka Abu Dhabi kwenda Jakarta Indonesia ilipata hitilafu angani. Abiria 31 wamejeruhiwa huku 9 kati yao wakiwa na hali mbaya zaidi. Chini ni video ya hali ilivyokuwa ndani ya ndege wakati wa dhahama hiyo.

Shuhudia mwenyewe kwenye video hii

My take: Sisi wanadamu tujifunze kukumbuka imani zetu kila siku sio mpaka ukutane na taharuki

Itakuwa ni turbulence.......Hapa ndipo marubani hulipwa fedha nyingi....manake The second effect of control yaweza tokea pande .....ote..SALUTE to all pilots...mtu mmoja kakabidhiwa roho nyingi......pilots si viumbe wa kawaida.....
 
Ukiwa naimani sawasawa na kumtaja sana Mungu huwezi kuogopa kifo.... anaye ogopa kifo basi huyo hakujiandaa vya kutosha
 
turbulence ni ya kawaida tu hasa kwa long trip inaonekana kina mama wengi humo ndani wamepanic.issue hizo ni kukaa kimya kuomba mungu na kumsubiri pilot afanye yake.kupiga makelele namna hiyo ndio mnarisc kupata ajali kwani pilot anapoteza confidence.
 
Kama unaomba uingie peponi kwa nini uogope kifo? na huwezi ingia peponi ila kwa njia ya kifo.
 
Back
Top Bottom