VICOBA ni idea nzuri, Ila kwa Tanzania haitekelezeki

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,915
VICOBA ina histora ndefu sana, ikiwa ni wazo lilio anzia hasa India, miaka ya 80 mwishoni kwenye jamii ya watu masikini kule India ambao walikuwa wakati wa uchaguzi wanaomba omba pesa sana kwa wanasiasa ndio watu wakakaa chini na kubuni saving group.

Miaka ya 90 mwishoni ikaingia Afrika hasa West Africa kwenye nchi ya Niger, na baadae ikaenea hadi Tanzania miaka ya 2000.

VICOBA ukienda kwenye nchi tu za EAC kama Uganda, Kenya, Rwanda zina perform well sana, Zambia, Malawi, Zimbabwe, South Africa Botswana kote huko hakuna changamoto, West Africa Cameroon, Ghana, Nigeria kote huko hakuna Changamoto.

Shida iko Tanzania ambako ujanja ujanja ni mwingi sana, na VICOBA haitaki ujanja ujanja, kabisa. Kwa Tanzania VICOBA inaonekana haifai kabisa, na sababu kubwa ni Tamaaa na ujanja ujanja wa wanavikundi.

VICOBA ina misingi yake ambayo ni;
  • Upendo kwa wana vikundi
  • Uwazi
  • Umoja
  • Kuwa levo sawa ya maisha
  • Wanachama wote kufahamiana, kujua tabia za kila mwana kikundi.
Sasa Vicoba vya Bongo, unakuta Wanachama wenyewe hawajuani, hawajuani tabia, hakuna uwazi kabisa.Wanashangaana kwenye kikundi make hakuna anayejua mwenzie anaishi wapi.

Hio misingi ikikiukwa tegemea Vilio vya kupigwa, na hapo ndio viongozi unakuta wanalala mbele na pesa sa wanakikundi, mara wachore ramani ya kuibiwa pesa yaani ilimuradi wapige pesa.

Kama Ndugu yako yuko au anataka kujiunga kwenye kikoba muulize maswahi haya;
1. Mnajuana wote? Mnafahamiana kwa tabia? Mnajya kila mmoja wenu anaishi wqpi na levo yake ya maisha ikoje?
 
Mwaka jana nilipata wazo la kutengeneza App ya Vicoba ila nikaja kugundua kumbe washirika mpaka mkutane mkae chini? Na hakuna kinachoendelea zaidi ya Umbea tuu mwanzo mwisho.
 
Vikoba vimeingiza Dada zetu kuwa na wanaume wengi sna Ili wafanye marejesho hadi huruma
 
Nchi zingine kinachowasaidia ni kufuata utaratibu wa kisheria kwenye kuendesha vikundi vyao. Bongo vikundi vingi havina usajili kisheria kiasi kwamba hata pesa hukaa nazo kiongozi nyumbani kwake badala ya benki. Na vikundi vingi vinaundwa na watu wajanja wajanja wenye njaa kali. Vikundi vya wenye nazo hufanya vizuri hadi kuwa taasisi kubwa... mfano hai ni kikundi cha matajiri wa Arusha kilichokuja kuzaa Arusha Club SACCOSS ambayo ina mwelekeo wa kuja kuwa benki kabisa.

Mimi mtazamo wangu kuhusu utajiri na mafanikio ni kwamba hakunaga utajiri wa kikundi. Kama unataka kuwa tajiri lazima uwe mbinafsi.. hata ukiwa kwenye kikundi hakikisha kinakunufaisha zaidi. Usiwe kama wale wanakikundi wa kuvaa tshirts na kujionyesha wapo kwenye kikundi. Wewe angalia maslahi tu
 
Back
Top Bottom