SoC02 Tatizo la VICOBA ni kuvunja ile miiko yake, VICOBA ni nzuri sana

Stories of Change - 2022 Competition

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Apr 14, 2022
389
753
Tanzania VICOBA inaogopwa sana kwa sasa, na kosa ni kuvunja miiko yake, VICOBA AU Saving group, Village Saving and Loan Associations(VSLAs) na kadhalika ni wazo ambalo malengo yake yalikuwa ni mazuri sana kwa walio asisi, VICOBA Kwanza tutambue haiko Tanzania pekee yake kwenye Bara la Africa zaidi ya nchi 30 zina practice VICOBA, Bara la Asia kuna VICOBA, America ya kati na kusini kuna VICOBA pia, ni Ulaya Magharibi na Marekani ndo hakuna VICOBA na sababu zinajulikana vyema.

Hizo tajwa hapo juu zote VICOBA vyao havina shida kabisa na wanaendele vizuri , shida kuu iko Tanzania, bongo land kwa wajanja ambako kila mtu anataka kutoka kwa kila mbinu zikiwemo chafu na kadhalika,hi indo inafanya VICOBA viogopwe sana kwa sasa na inaonekane ni kitu cha hatari sana ambacho kina filisi jamii hasa wanawake.

VICOBA ina miiko yake ambayo hizo nchi zingine nilizo taja hapo juu bado wanafuata ile miiko yake na wana endelea huwezi waambia chochote kuhusu VICOBA. Je miiko hio ni ipi hasa? Twende tukaingalie hio miiko ya VICOBA;

VICOBA inaundwa na watu wanao fahamiana- Hii ni mwiko wa kwanza wa VICOBA kama unaona ndani ya kikundi hamjuani basi toka nduki mapema sana, VICOBA lazima wanachama wote 30 muwe mnajuana sio mje kujuana kwenye kikundi hapana muwe mnajuana kabla, yaani kabla ya kuanza kikoba mnajuana, mnajua fulani anakaa wapi na ana maisha gani yaani mnajuana hadi kwa majina na tabia pia mnajuana sio majina pekee. Kama hamjauani basi kimbia make mwisho wake utakuwa mbaya sana kwako, utaenda kulilia chooni, utazika pesa zako.

WANACHAMA WANAISHI MTAA MMOJA- lazima wote muwe mnaishi eneo moja hiii inasaidia hata kuongozana vyema na ndo hata sababu ya kufahamiana inaingia hapa, lazima wote muwe eneo moja, hii itawasaidia sana hata kuendesha mikutano yenu ya kikundi, tofauti na hapo anaza kuhesabu hasara, sio mmoja mbezi mwingine gongo la mboto.

UPENDO KWA WANACHAMA WOTE-Hii inaweza kuwa ndio nguzo kuu ya kwanza ya Kikoba, je nyie mnapendana? Au mnapendana kinafiki? Ukiona mko ndani ya kikoba na hampendani basi ni swala la muda tu, upendo ni nguzo kuu kabisa ndani ya Kikoba, wanachama lazima wawe na upendo wad hat kabisa na hii inasaidia mambo mengi sana, kama hampendani hicho sio kikundi bali ni sehemu ya watu kutaka kupiga pesa za wenzao na walale mbele. Upnedo ni muhimu sana tena upendo wa kutoka moyoni kabisa.

UWAZI- Hii sasa ndo imeau VICOBA vyote ingawa hizo sabau za hapo juu zinawea kuwa ndio sababu ila swala la uwazi, bila uwazi hapo kimbia kabisa ndugu yangu na kama kuna mke wako anataka kujiunga mwambie aacha au ajitoe mapema, uwazi ni pamoja na kuendesha vikao kwa uwazi kabisa, kutanga mapato kila siku na kwa uwazi kabisa, yaani kila kitu ni kwa uwazi kabisa na hakuna kufichana kitu, tofauti na hapo anza kulia.

WANACHAMA LAZIMA WAKUTANE WOTE-Hapa ndio upigaji unapo anzia, moja ya miiko ya VICOBA ni kwa wanachama kukutana , sasa VICOBA vingi eti wanatumana pesa, hahaha kanichezee kikoba, niko busy, kama unaona huna muda na kikoba wacha kujiunga, achana na habari za kutumana pesa, VICOBA kuhudhuria kwa wanachama ni muhimu kuliko hata kununua hisa, bora uhudhurie na ukose pesa ya kununua hisa au kuchea kama wanacyo ita, ila kama mko 30 na wanahudhuria 12 basi jiandaeni, na msije laumu mtu, kama uko kwenye vicoba na huna muda wa kuhudhuria unatuma pesa basi jilaumu mwenyewe na wala usije mlaumu mtu mwingine kabisa.

KUWA NA VIWANGO SAWA VYA MAISHA- ni muhimu wanachama wakawa na levo sawa ya maisha na sio tajiri kwa masikini, mnapo kuwa na kiwango sawa inasaidia sana make tofauti nan hapo unakiuta kikundi kinatekwa na wenye pesa, na nyie wengine mnabakia kama misukule tu ndani ya kikundi, hivyo hakikisha wote mana kiwango sawa cha maisha, msizidiane sana.

MFUMO WA KUKAA – Kuna ule mfumo wa kukaa wa kama Raisi anaendesha kikao cha Baraza la mawaziri, ule ndio mka na lengo sana ni kuhakikisha uwazi, hii inasaidia kuona pesa zinavyo hesabiwa, na lazima wanachama wakague vitabu vya wanachama wenzano ili kuhakikisha hakuna alie wekewa vigure kimakosa, sasa mkiwa mnakaa tu kama mko kwenye kikao cha famillia hii ni makosa sana kwenye miiko ya VICOBA.

HAKUNA UTITIRI WA VIONGOZI- VICOBA ina viongozi Mwenyekiti, Mweka hazina, Katibu na wahesabu pesa basi, ukianza kuona Kikoba kina kamati kamati basi anza kuhesabu maumivu ni swala la muda, VICOBA inatakiwa kuwa rahisi sana kuendesha na uongozi simple.

VICOBA HAKUNA ALIE NA MAMLAKA KUPITA MWEZAKE- Wanachama wote 30 wana haki sawa wana kura ya VETO, kwenye kikoba hakuna alie juu na wala hakuna kamati imeamua, Mwenyekiti ameamua, mambo yote ndani ya kikoba ni kwa democrasia ni kwa kupiga kura tu, hakuna cha kamati imeamua bali ni kura zimeamua.

MIKOPO WANAO AMUA MTU AKOPE NI WANACHAAMA WOTE 30- Sasa vicoba vya mtaani unakuta kuna kamati ya mikopo hii ni kosa kubwa sana ukiona kamati ya mikopo kimbia sana hapo utalia muda sio mrefu, wanao amua Fulani akope ni wanachama wote tena wanaulizwa na mwenyekiti wa kikundi kwamba je Fulani akope au asikope? Wanachama wanajadili, ila kama kuna kamati ya Mikopo basi kimbia kabisa hapo, ni upigaji kwend mbele hapo utalia muda sio mrefu.

VIONGOZI WA VICOBA LAZIMA WAWE WATU WA HEKIMA SANA- Kwenye kuchagua viongozi wa VICOBA kuna hitaji umakini sana na ndio maana swala la kufahamiana lina sisitiziwa na swala la wote kuishi eneo moja.

VICOBA vingi wamevunja hii miiko kwa sababi inawabana na wanachama wanaingia kichwa kichwa tu kwa kufuata mkumbo ndo maana wanalia, VICOBA zimejaa wajanja wajanja ambao ndo hao wanajipa vyeo mara mwenyekiti wa mikopo, mwenyekiti wa marejesho na kadhalika, kwenye miiko ya VICOBA hakuna kitu kama hicho, nenda nchi zingine nenda Rwanda, nenda Uganda, nenda Kenya , nenda Zambia, Malawi, South Africa na kwingineko, wana fanya vyema kabisa VICOBA vyao , tatizo liko Tanzania ambako ni ujanja ujanaja ni mwingi sana na upigaji.

Malengo ya VICOBA ni mazuri shida miiko imevunjwa na wajanja wamekuwa ndo wakuu wa VICOBA.

images%20-%202022-08-14T101221.063.jpg
 
Back
Top Bottom