Uaminifu ni bidhaa adimu sana Tanzania

kahtaan

JF-Expert Member
Jul 11, 2009
18,713
11,274
Wanabodi,

Suala la uaminifu hapa Nchini kwetu limekuwa ni Changamoto kubwa sana kiasi kwamba mpaka nchi za nje watanzania tunajulikana kwa sifa za UONGO, UJANJA, UTAPELI NA WIZI.

Nimejaaliwa kutembea nchi nyingi tu za Nje zikiwemo katika mabara ya ASIA, EUROPE, USA na AFRICA na kila niendapo watanzania tunasifiwa kwa Amani na utulivu lkn always zinafuatana na hizo sifa hizi mbaya.

Upande wa utalii vijana wetu wanawapiga sana watalii kwenye kila nyanja. Kuanzia upandishaji wa bei za nauli, huduma mbalimbali mpaka Bei ya Mkate mtalii anapewa tofauti na Mtanzania. Na WATALII WOTE wanaokuja kwetu SIO WAJINGA.

We unampa bei ya juu unapata buku la ziada yeye kumbe anakucheki tu akijua "huyu kijana njaa yake hatari" kaiba buku? (senti 35 dollar) ambayo kwao hata ukidondosha hamna atakaeokota.)

Wengine wanaibiwa sana kwenye mabasi ya abiria. Nimekutana na wageni wanadai mizigo yao yote iliibiwa waliposimama na BUS kwenye zile Hoteli za vyakula Njiani.

Wakati mwingi Makondakta wanakula na WIZI njama za kuiba mizigo ya watalii manake abiria wengi wanashuka kwenye Bus. Inakuwaje Mwizi achukue Bila Konda kufahamu?

Hapa Nchini leo ukitaka kutafuta kijana wa kumuajiri awe dereva, karani, mhasibu, Shop salesmen hata house girl au house boy kuweza kupata muaminifu asilimia 100 hiyo sahau.

Huko mashambani vijana wanaiba mpaka vifaa vya kazi.
Kwenye Workshops, magereji vijana wanaondoka na Spana na kila kinachoweza kubebwa Fasta.

Swali nauliza. Kama kuiba kunaletwa na NJAA ina maana Tanzania wana shida kuliko Rwanda, Burundi na Zambia? Mbona sisi tumezidisha wizi kuliko hizi nchi za jirani.

Kwanini Ukienda Dubai kuna maduka ya Dhahabu lakini hukuti Nondo wala Mageti ya chuma na saa ya swala IKIFIKA wenye mali wanawacha wazi maduka. Na hakuna anaeiba?

Dubai maskin wengi tu kutoka India na kwengine. Kama ni kuogopa kukatwa mkono mbona Bongo vibaka wanapigwa mpaka Kufa lakini wizi unaendelea tena mchana?

Wabongo tuna sifa mbaya sana nje ya nchi..

Someni Website za serikali ya USA, UK, FRANCE na Nchi nyingine nyingi . Wameweka angalizo kwa watalii wao wanaotaka kuja TANZANIA kuwa wajichunge na MATAPELI NA WEZI WA MIFUKONI na MAJAMBAZI WAKABAJI.

SERIKALI haina budi kusimamia sheria kwa ukali sana otherwise itakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.
Serikali inapiga promo za utalii. Vijana wanaibia watalii.

Wakirudi kwao wanatoa onyo kwa wengine kuwa Tanzania nuksi. Na wanajaza kashfa kwenye blog zao kupeana tahadhari kuwa Tanzania vijana WEZI, MATAPELI, WAONGO NA MAJAMBAZI

Nawasilisha.
 
Kuna miaka flani niliwahi kufanya kazi flani isio rasmi kwa uaminifu mkubwa sana.

Aiseeeee! That time nilipata pesa sana ambayo sikuitegemea, nikanunua kiwanja na nikajenga nusu nyumba hadi wife alishangaa sana.

Mimi napenda kuwaambia watoto wangu kwamba, uaminifu na nidhamu ni mambo ya muhimu sana katika ustawi wa maisha ya mwanadam.
 
Kuna miaka flani niliwahi kufanya kazi flani isio rasmi kwa uaminifu mkubwa sana.
Aiseeeee....
That time nilipata pesa sana ambayo sikuitegemea, nikanunua kiwanja na nikajenga nusu nyumba hadi wife alishangaa sana.
Mimi napenda kuwaambia watoto wangu kwamba, uaminifu na nidhamu ni mambo ya muhimu sana katika ustawi wa maisha ya mwanadam.
Siku zote uaminifu unalipa.

Mungu anatia baraka kwenye kipato chako. Na anakulinda na balaa nyingi.
 
Tatizo letu kubwa ni:

 

Attachments

  • IMG_20240113_003425.jpg
    IMG_20240113_003425.jpg
    31 KB · Views: 2
Suala linaanzia level ya familia, ndio maana viongozi wengi ni wezi halafu waongo, kwa mikoa Dar inaongoza kwa watu wasio waaminifu, unakutana na dogo miaka 10 anapiga sound za kitapeli hadi unashangaa.

Malezi bora ya familia yanajenga taifa lililo bora.
 
Hii balaa imeanzia kwa watawala wetu. Ukipata nafasi halafu usipige jangusho, unaonekana zobanangai mtaani watasema huyu alikuwa fulani lakini cheki alivyochoka na hao wapigao jangusho malipo yao ni hapa hapa pesa itaishia kwenye matibabu na kulipia watoto wao sober houses 👍
 
Suala linaanzia level ya familia, ndio maana viongozi wengi ni wezi halafu waongo, kwa mikoa Dar inaongoza kwa watu wasio waaminifu, unakutana na dogo miaka 10 anapiga sound za kitapeli hadi unashangaa.

Malezi bora ya familia yanajenga taifa lililo bora.
Kuna watoto wawili km miaka 8 au 9. mtaani walioniomba kuwanunulia madaftari na vifaa vya shule
Wakadai wao ndio shida yao kubwa manake wakiomba pesa wataonekana wezi.

Nikaenda nao dukani tukanunua begi za shule 2 madaftari kadhaa , pencil case, rulers Pens na mazaga mengine.

Nimeachana nao hapo baadae naambiwa na mama lishe wa pale mtaani kwetu kuwa wale madogo wamekuja wanatangaza biashara ya vifaa vya shule kwa Nusu ya Bei.

Toka siku ile nikiona mtoto mtaani anaomba daftari nachafuka nafsi.
 
Hii balaa imeanzia kwa watawala wetu....ukipata nafasi halafu usipige jangusho....unaonekana zobanangai...mtaani watasema huyu alikuwa fulani lakini cheki alivyochoka....na hao wapigao jangusho malipo yao ni hapa hapa...... pesa itaishia kwenye matibabu na kulipia watoto wao sober houses
Watu wana laana ya wizi.
Kuna watu nimekutana nao wako serikali rushwa hapokei
Lkn zawadi hakatai.
Na usipoleta zawadi anakununia.

Serikali lzm iingilie kati suala la WIZI la sivyo nchi yetu itaendela kuogopwa mpk tubaki na MAJIZI KAMA SISI ndio tutawezana.

Ndo maana Wazungu na wawekezaji wakija hapa NI KUIBA TU manake SISI WENYEWE WEZI.

Mtu anaiba Dhahabu ya billion 20 anampa mtanzania million 200 akae kimya .

Na yeye anaona sawa. Bora serikali ikose mapato yeye apate hio pesa akajenge kwao
Serikali iweke sheria kali na iisimamie mwaka mzima uone km na sisi hatujafikia Dubai au Zaidi.
 
Kuna watoto wawili km miaka 8 au 9. mtaani walioniomba kuwanunulia madaftari na vifaa vya shule
Wakadai wao ndio shida yao kubwa manake wakiomba pesa wataonekana wezi.

Nikaenda nao dukani tukanunua begi za shule 2 madaftari kadhaa , pencil case, rulers Pens na mazaga mengine.

Nimeachana nao hapo baadae naambiwa na mama lishe wa pale mtaani kwetu kuwa wale madogo wamekuja wanatangaza biashara ya vifaa vya shule kwa Nusu ya Bei.

Toka siku ile nikiona mtoto mtaani anaomba daftari nachafuka nafsi.
Miaka 8 huyo, akifika 20 atakuwaje.
 
Suala la uaminifu hapa Nchini kwetu limekuwa ni Changamoto kubwa sana kiasi kwamba mpk nchi za nje watanzania tunajulikana kwa sifa za UONGO, UJANJA, UTAPELI NA WIZI.
TZ Bara kizaidiiiiiiii sanaaaa

****

Mojawapo ambayo huwa sielewi hadi kesho ni hili

Kitu mfano huduma fulani, kinaandikwa bei
Mtanzania Tshs 30,000/-
Mtalii asiye Mtanzania 30usd (75,000/-)

Yaani ikiwa 70,000/-
Mtalii unaona 70usd

Kwanini hivi?
 
Back
Top Bottom