Kieleweke,
Na kuajiriwa kwa Asha Rose Migiro UN ni kwa ajili ya automtic-favor?
Mkuu, soma post yangu vizuri. Kuna wakati nilipoituma network ilileta problem ikaja robo na hivyo nikaiedit. Pitia hapa upya hapa chini.
Hivi ni lini watanzania tutaonekana tunaweza kazi za competition za dunia hii katika international forum. Nina maana kwamba ni kazi zile ambazo mnagombea na wanadunia wenzenu halafu akaibuka mtanzania akawa-beat wote.
Mimi naamini hizo ndizo zitakazotuongezea sifa kwamba Tanzania kuna intelligent people na kuongeza sifa kama Taifa.
Mfano kile alichothubutu Salim Ahmed Salim kugombea ukatibu mkuu UN ile mwaka 1980. Baada ya hapo tungesiki mtanzania mwingine anashindana kutoa consultation katika masuala ya kisayansi, na mwingine jambo lolote.
Zaidi ya hapo unaweza kufarijika kidogo kwa post kama ya Dr. Asha Rozi Migiro na Proffessor Anna Tibaijuka. Ni kazi ambazo unaweza kukaa kwenye ndege unaelekea Japan unamsimulia aliye pembeni mwako kwa kutamba kwamba "ona watanzania tulivyo wataalamu"
Lakini ukiziangalia hizi kazi nyingine unagundua si kwamba watanzania tulionyesha u-genious fulani. Utaona kwamba ni kazi ambazo inahitajika mtu aongee kiswahili. Jambo unaloweza kufananisha na ubalozi wa Brazil ulipofunguliwa hapa nchini. Kabla ya hapo kama kuna m-mozambique aliishi hapa nchini kwa kubangaiaza basi siku ikitangazwa kwamba ubalozi wa Brazil unahitaji mtu anayejua kireno basi m-mozambique huyo moja kwa moja aweza kupata kazi ubalozini.
Kama kule Mozambique (Msumbiji) kuna JF kama hii watamshangilia kwamba jamaa yetu kaula huko Tanzania.
Niliwahi kuambiwa jamaa yetu anafanya kazi taasisi ya kitaalamu hapa nchini. Siku moja akaenda Korea na kutoa presentation nzuri. Mimi nikaitafuta ile presentation kwenye google na nikaipata, kwani namjua yule jamaa tangu chuoni anapenda kujulikana ni kipanga.
Nilipoisoma ile presentation yake nilisema Mungu wangu! Nilishtuka kuona kilichoandikwa. Nilitarajia kwamba jamaa kule ata-present material makali ili wakorea wajue Tanzania kuna vipanga. Lakini nilichokikuta niliona report imejaa jinsi nchi yetu ilivyo masikini na inavyohitaji kusaidiwa.
Sikatai concept ya kusaidiwa. Lakini hakuna sehemu ya report ile iliyoonyesha kwamba watanzania tukiingia kwenye internationa forum tunaweza ku-compete na wenzetu kwenye internation issues iwe ajira, consultation au kitu kama hicho.
Niliwahi kukaa jiji la Yorkshire nchini Uingereza na siku moja nikatembelea daraja refu liitwalo Humber Bridge lililo karibu na jiji hilo. Hakika kwangu lilikuwa daraja refu kuliona kwa macho yangu. Na wenyeji wakasema wakati linajengwa lilikuwa refu duniani kote.
Lakini nikaambiwa kwamba project ya daraja hii ilifanywa na mtu asiye raia wa Uingereza ni mholanzi. Lakini miaka ya badaye nikagundua hakuwa na uhakika maana serach yangu kwenye net inaonysha aliyelijenga ni muingereza.
Lakini kabla ya kugundua hili nilibaki kujiuliza kwamba hivi ni lini na sisi watanzana tutagombaniwa kwenye proffession project kama hizi kama waholanzi wanavyothubtu kuwajengea waingereza daraja kama lile.
Hapo ndipo ilipolala concept yangu. Na siku zote nikisikia mtanzania kaitwa kufanya kazi majuu kwanza naangalia ni post yenye sura ya global competition au ni aina fulani ya automatic-favor.
Automatic-favorkwa maana ya kwamba kama ni kazi ambayo inahitaji ujuzi kiswahili, je, hapo kuna competition gani wakati sisi watanzania ndiyo wataalamu wa kiswahili duniani.
Kama ni kazi inahusu haki za ma-albino duniani, Unategemea succesfull candidate atoke wapi wakati Tanzania kila leo unasikia maalbino wanauawa au wanakatwa mikono.
Hizo ndizo kazi tunazozipata huko majuu na sisi tunashangilia kwamba wameonyesha mfano.
Mimi naamini hata kwa utani ikianzishwa kampuni ya kimataifa ifanye kazi duniani ya kutengeneza vikao vya harusi na kitchen party basi nadhani watanzania tunajijua tulivyo wataalamu eneo hilo. Kampuni hiyo itajaa watanzania kibao. Wenye kutumia neno "wenzetu wameula" watalitumia na wengne watsema "tumepaisha chati" ya nchi yetu.
Hebu tukae tutulie. Sisi ni vipanga (brilliant) kama wengine duniani. Ifike mahala ikitangazwa proffessional tender kama consultation nchini Netherland basi uwakute watanzania tunagombea huko. Hata kama hatuna hela za project basi walau wajue kwamba kuna watanzania vipanga. Si unakumbuka tumesoma nao hao wazungu na darasani tulikuwa tunawa-beat. Leo iweje watushinde mtaani, akili mpya waliipata wapi.
Tusiishie kukimbilia kazi kwa sababu kuna kampuni inafanya research kuhusu umasikini ulivyo Tanzania tukabweteka kwamba tunakumbukwa katika international forum.