Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,139
Leah Cambridge

CHANZO CHA PICHA,SCOTT FRANKS
Maelezo ya picha,
Leah Cambridge alikumbwa na mshtuko wa moyo mara tatu alipokuwa amedungwa sindano ya ganzi katika kliniki ya Uturuki.

Mwanamke wa miaka 23 amefariki baada ya kuripotiwa kuelekea Uturuki kwa aina ya upasuaji kwa jina Brazilian Butt Lift [uongezaji wa makalio}.
Ni kwa nini upasuaji huu ni maarufu mbali na kwamba ni hatari kufanywa ughaibuni.
Leah Cambridge kutoka Leeds alipatikana na mishtuko mitatu ya moyo baada ya kudungwa sindano ya ganzi katika kliniki moja katika mji wa Izmir, mwenzake Scott Franks aliambia gazeti la the sun.

Anaeleweka kufanyiwa BBL ama upasuaji wa kuongeza makalio ambapo mafuta kutoka katika tumbo hutiwa katika makalio.
'Mrembo huyo alikubali kufanya upasuaji ughaibuni ambapo ni bei nafuu ikilinganishwa na Uingereza baada ya kukerwa na mafuta mengi katika sehemu yake ya tumbo baada ya kupata watoto', alisema bwana Frank.
Kim Kardashian

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Nyota wa kipindi cha runinga nchini Marekani Kim Kardashian

Majirani wake wamemtaja kuwa mtu anayevutia, wakiongezea kuwa wanaamini alielekea kufanyiwa upasuaji huo mwezi uliopita bila kumshauri mpenziwe.
Na bi Cambridge sio mwanamke wa kwanza Muingereza ambaye hamu yake ya kuwa na makalio ya kuvutia yalimwangamiza akiwa ughaibuni.
Joy Williams alifanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio yake mjini Bangkon nchini Thailand mnamo mwezi Octoba 2014.

Vidonda vyake vilipata maambukizi na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka mjini London , alifariki akidungwa sindano ya ganzi.
Miaka mitatu kabla , Claudia Aderotimi mwenye umri wa miaka 20 , kutoka Hackney , mashariki mwa London alifariki kutokana na matibabu ya kujiongeza makalio yake katika hoteli moja nchini Marekani.
Upasuaji wa kuongeza makalio hauonekani kuwa hatari zaidi ya aina nyengine zozote za upasuaji, kulingana na daktari wa upasuaji wa urembo Bryan Mayou.
Scott Franks and Leah Cambridge

CHANZO CHA PICHA,SCOTT FRANKS/FACEBOOK
Maelezo ya picha,
Scott Franks said he had been left a "broken man" after the death of his partner and warned others to think about the risks of cosmetic surgery

'Hatari yake ni upasuaji huo kufanywa na madaktari ambao hawajahitimu, nje ya kliniki bila kuwa na maelezo ya jinsi ya kujichunga baada ya matibabu hayo kufanywa', anasema bwana Mayou, mwanachama wa muungano wa madaktari wa upasuaji nchini Uingereza.
Iwapo mafuta yataingizwa katika tishu ya sehemu ya makalio kuna hatari ya kuingiza mafuta hayo katika mishipa mikubwa ya damu.

Mafuta hayo yanaweza kupita katika mishipa ya damu , kuingia katika mapafu kabla ya kusababisha kifo.
Claudia Aderotimi

Maelezo ya picha,
Claudia Aderotimi died after an injected substance spread to her organs

Bwana Frank aliambia gazeti la The sun : Leah alikuwa amedungwa sindano ya ganzi akakumbwa na matatizo baada ya mafuta kuingia katika mishipa yake ya damu hatua iliofanya viwango vyake vya oxygen katika damu kushuka .
Hali yake iliimarishwa lakini alikumbwa na mishtuko mitatu ya moyo na hawakuwa na la kufanya.
'Madaktari wa upasuaji kutoka jamii za kimataifa wameunda jopo kuchunguza kuripoti kuhusu utaratibu huo'', anasema Mayou.

'Viwango vya vifo vinavyotokana na utaratibu huo ni kisa kimoja kati ya 3000 huku vifo vyote vilivyochunguzwa vikihusisha mafuta yaliopatikana ndani ya mishipa ya misuli ya makalio', anasema.
Kylie Jenner

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Nyota huyo wa kipindi cha Keeping Up with the Kardashians Kylie Jenner amekana kufanya upasuaji wa makaliuo.

Daktari wa upasuaji anasema kuwa amegundua viwango vya upasuaji wa kuongeza makalio katika kliniki yake ya Cadogan mjini Chelsea , magharibi mwa London katika kipindi cha miaka minne.
Ni mtindo wa kisasa, miaka kadhaa iliopita kila mtu alipendelea kuwa mwembamba na walikuwa wakisema kuwa wanataka kufanyiwa upasuji ili kufanya makalio yao kuwa madogo.
'Na hiyo ndio mbinu ambayo inaweza kutumika iwapo mtindo mpya wa kuongeza makalio utakwisha na mwathiriwa anataka makalio yake kurudishwa yalivyokuwa', anasema.

Kwa nini watu wanapendelea sana kuwa na makalio makubwa ? ni kutokana na utamaduni maarufu wa kushabikia maungo yanayovutia.
Watu maarufu kama vile Kim Kardashian , Kylie Jenner na Cardi B wana umaarufu mkubwa katika mitandao ya kijmaii ambapo huchapisha picha zao wakionyesha makalio yao yalio mviringo.
Cardi B

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Mwanamuziki wa mtindo wa Rap Cardi B amekuwa wazi kuhusu kuongezwa makalio yake

Presentational white space

Jenner alichapisha katika blogi yake ambapo alisifu maumbile yake na uzani ulioongezeka.
''Sijaongezewa makalio. Unajua, nilikuwa na uzani wa 120 [lbs]. Nilikuwa mwembamba sana. Sasa nianelekea 136Ibs , lakini ni sawa napendelea uzani nilionao''.
Hatahivyo, Cardi B amefichua kwamba kabla ya kuingia katika fani ya muziki aliongezewa makalio huko mjini New York na kifaa alichowekewa ndani kilivuja kwa siku tano baadaye.
Katika mahojiano alisema kuwa alilipa takriban $800 (£564) kwa upasuaji huo baada ya kuwaona wachezaji densi wanzake walio uchi katika vilabu vya burudani walio na makalio makubwa wakipata fedha nyingi kumliko.

Chloe Simms, ambaye ni nyota wa kipindi cha runinga cha The Only Way Is Essex, amekuwa wazi kuhusu makalio yake aliyoongezewa baada ya kulalamika katika kipindi hicho kwamba alikuwa hana makalio.
Chapisho hili la Instagram la mwaka 2013 linamuonyesha alivyokuwa.
Ruka Instagram ujumbe, 1

Mwisho wa Instagram ujumbe, 1
Presentational white space

Anaonekana kuwa na maumbile ya kuvutia katika nguo yake ya kuogelea Julai 2018.
Ruka Instagram ujumbe, 2

Mwisho wa Instagram ujumbe, 2
Presentational white space

Je upasuaji wa kuongeza makalio unahusisha nini?​

  • Utaratibu huo unatumika kuongeza makalio , kuwa mviringo na kuinuka
  • Madaktari wa upasuaji huingiza Silicone ama mafuta yaliotolewa katika eneo jingine la mwili
  • Nchini Uingereza utagharamika kati ya £2,000 na £7,000, ikitegemea kliniki na iwapo kuna kazi ya ziada inayohitajika
  • Baada ya upasuaji , wagonjwa hupata maumivu machache, katika eneo lililofanyiwa upasuaji kwa muda wa wiki chache na hushauriwa kutoketi chini kwa kutumia makalio kwa kipindi cha wiki tatu.
  • Madhara yake yanaweza kushirikisha maambukizi ya vidonda, kupasuka ama mafuta hayo kuingia katika mishipa ya damu.
Presentational grey line

Upasuaji wa kuongeza makalio unagharimu £8,000 nchini Uingereza. Kulingana na baadhi ya ripoti Bi Cambridge alilipa £3,000 kufanyiwa upasuaji.
"lakini tuna watu wanaosafiri kutoka ughaibuni kuelekea katika kliniki mjini London kwa sababu wapasuaji uhitimu, kudhibitiwa na kliniki ni salama . chanzo. Uongezaji wa makalio: Je ni hatari inayopuuzwa? - BBC News Swahili
 
wanawake hawaweze kuelewa chochote, kila mmoja anataka awe na mzigo nyuma wakiamini maisha yatarahisika wakishakua na kiunokikubwa. Japokua imani ya ina ukweli ndani yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom