Vicky Kamata: Rais Samia hawezi kutibu majeraha, viongozi wa dini wagange mioyo ya watu, wamejeruhiwa

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,407
Amesema kiongozi wa awamu ya tano (jiwe) alikuwa mtu katili sana kiasi cha kumfanya apate taabu sana.

Amewasihi watanzania kuishi kwa kutenda mema maana duniani tunapita. Jiwe alilewa madaraka.

Amemaliza kwa kusema pamoja na kufuta andiko lake la kumshutumu jiwe ni kweli jiwe aliniumiza sana.

Source: StarTv (Medani za Siasa) muda huu.

==========

Mwandishi: Hujaeleza mheshimiwa Vicky Kamata, umezunguka sana. Swali la msingi, ni kitu gani kigumu ama ni jambo gani, wakati gani ambao ulikumbana na jambo gumu ambalo ukitafakari unaona kabisa kidogo likutoe kwenye reli?

Vicky Kamata: Unazungumza wakati tayari niko bungeni au wakati natamani kuwa kwenye siasa?

Mwandishi: Tayari uko kwenye siasa

Vicky Kamata: Nikiwa bungeni, labda kile kipindi ambacho awamu ya tano iliingia, mimi ilikuwa tayari ndio nimeolewa, nina ndoa changa tu ikatokea bahati mbaya, siwezi kusema bahati mbaya, mwenye ofisi yake akisema pumzika nataka huyu akae hapa utalalamika? Huwezi kulalamika.

Hicho kilitokea kwa mume wangu, alikipokea very positively, binafsi nilikipokea kawaida kabisa na maisha yakawa mazuri kabisa lakini sasa wenzangu pale bungeni wakaanza kama kunitenga.

Chochote ninachoshauri naonekana ninashauri kwa sasabu nina hasira, kitu ambacho sikuwa nacho wala sikiwazii kwasababu mhusika mwenyewe hajalalamika, walihusisha kazi ya mume wangu na kazi yangu.

Tena wanaCCM wenzangu mpaka walikuwa wanachangia wazi kabisa yaani flani, anakupiga kijembe cha wazi kabisa kwamba una hasira, mume wako ametumbuliwa.

Vicky Kamata Magufuli.jpg

Mwandishi: Umekuwa mbungewa viti maalum kwa miaka 10 mkoa wa Geita, kwanini ukaja huku(Dar-Kibamba) ambako hukufanya chochote kwa ajili yao? Hofu yako ilikuwa nini Geita?

Kamata: Sikuwa na hofu isipokuwa katika majimbo yote ya Geita, yote yalikuwa na wabunge ambao ni wazuri, kaka zangu na wanafanya kazi nzuri kiasi huoni sababu ya kwenda kusukumana na Dotto Biteko, Kanyasu au uende kwa Msukuma

Mwandishi: Kwa mantiki hiyo unataka kutuambia Kibamba hakukuwa na mbunge anayefanya vizuri?

Kamata: 'Exactly' mimi ni CCM mbunge aliyekuwepo wakati ule alikuwa ni wa upinzani na niliona ilikuwa ni wakati sahihi wa kurudisha jimbo letu kwenye chama cha mapinduzi, Kibamba nilienda kwasababu jimbo lilikuwa upinzani na kule kwetu hakuna jimbo lolote lilikuwa upinzani, majimbo yote yalikuwa ni CCM na yalikuwa na wabunge wanapendwa

Mwandishi: Unataka kuwaaminisha watanzania, majimbo ambayo yanaongozwa na wabunge wa CCM ndio yanayopofanya vizuri

Kamata: Sijasema hivyo, inawezekana yapo majimbo ya wabunge wa CCM na hayafanyi vizuri lakini kwa mkoa wangu wa Geita wana sifa nzuri na wanafanya kazi nzuri.

Mwandishi: Ni kweli kwamba wanawake wengi walioko kwenye siasa wanatumika kwenye rushwa ya ngono?

Kamata: Mimi kama mbunge wa viti maalum nilipigiwa kura na wanawake wenzangu, sasa ukiniambia kuna rushwa ya ngono sijui hata inakuwaje lakini sidhani, siwezi kulijibia hilo.

Mwandishi: Hivi karibuni tulishuhudia andiko lako katika mitandao ya kijamii ambalo liliibua hisia za watanzania na nikiona kila mmoja akiipost kwa walichodai umetoa povu, nini ilikuwa dhamira ya andiko lako?

Kamata: Ningeshangaa usingeniuliza hilo swali, dhamira ya andiko langu ilikuwa ni kukumbusha watanzania wenzangu au mtu yoyote ambae angepita kwenye 'page' yangu kwamba hapa duniani sio mahali petu pa kudumu, tujitahidi kusihi vizuri ili tutakapoondoka tuache historia nzuri kwasababu hakuna atakaebaki hapa, hapa tumepewa muda mchache tu lakini katika muda huu mchache tuyafanye yale mzee Mwinyi amekuwa akituambia, kwamba maisha ni hadithi tu.

Mwandishi: Kwanini viongozi wengi wanatumia nafasi zao vibaya kama ulivyosema?

Vicky Kamata: Nadhani ni hulka ya mtu mwenyewe, walikuwepo viongozi ambao wapo kwa ajili ya kutesa watu wa Mungu na Mungu alijua jinsi ya kushughulika nao leo tunawasoma kama historia.

Mwingine anapambana apate madaraka fulani ili amkomeshe fulani.

Mwandishi: Athari yake katika taifa ni nini?

Vicky Kamata: Athari yake ni kutengeneza Taifa la watu wanafki, waongo, wavivu wasiojiamini na madhara yake pia ni makubwa sana kwasababu hakuna kitakachoendelea, nchi itasimama.

Juzi nimemuona askofu Arusha akimwambia mama, mama tibu majeraha, kwanini amesema hivyo? Ina maana kuna waliojeruhiwa, mimi nataka kuongezea hapo kwa askofu, sio mama atibu majeraha ila ninawaomba viongozi wa dini wagange mioyo ya watu wamejeruhiwa kwasababu ile post yangu imenipa vitu vya ajabu, nimepigiwa simu nyingi sana, kila mtu anaelezea maumivu aliyopitia katika kipindi fulani.

Kwa hiyo nataka kusema kwamba, sio mama Samia, mama Samia hawezi kutibu majeraha lakini viongozi wa dini wanaweza kutibu majeraha ya watu walioumizwa.
 
Amesema kiongozi wa awamu ya tano (jiwe) alikuwa mtu katili sana kiasi cha kumfanya apate taabu sana.

Amewasihi watanzania kuishi kwa kutenda mema maana duniani tunapita. Jiwe alilewa madaraka.

Amemaliza kwa kusema pamoja na kufuta andiko lake la kumshutumu jiwe ni kweli jiwe aliniumiza sana.

Source: StarTv (Medani za Siasa) muda huu.
Wataendelea kufunguka tu
 
Huyu naye au alikuwa miongoni mwa wanufaika wa Kikwete?
Mbona hamusahau Jiwe?
Swala kufa kila mtu atakufa,mbona kifo Cha Magufuli anakiona Kama adhabu?
Mbona mme wake alishakufa naye alionea watu ndo maana alikufa?
Hovyo kabisa.
upo sahihi,mi naona huu msemo wa duniani tunapita 7unatumiwa vibaya,jiwe alikuwa katili ndio na alijua atapita tu so kifo kisitumiwe kama kumsimanga mtu
ya jiwe yameisha watu wamuache tuendelee na mengine hata wakisema the Guy is no more na hasikii chochote
bora Lissu na kina Lema na Mbowe walimpa za uso akiwa hai na alizisikia,kusema mtu hayupo hakubadili chochote
 
Back
Top Bottom