Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vichwa Vya Nguruwe Vatundikwa Msikitini

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Aug 3, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 38,760
  Likes Received: 3,107
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  <tbody>[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG]
  Damu ya nguruwe kwenye sakafu ya eneo la msikiti[/TD]
  [TD]Thursday, August 02, 2012 5:50 AM
  Wakati waislamu wakiendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani, waislamu nchini Ufaransa wameelezea kusikitishwa na vichwa viwili vya nguruwe vilivyotundikwa kwenye geti la kuingia msikitini huku damu ya nguruwe ikitawanywa kwenye sakafu.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Umoja wa wanafunzi wa Kiyahudi nchini Ufaransa wameungana na jumuiya ya kiislamu nchini Ufaransa kulaani kitendo cha vichwa viwili vya nguruwe kutundikwa kwenye geti la kuingilia msikitini.

  Tukio hilo limetokea kwenye mji wa Montauban ambako mwezi machi mwaka huu mwanaume aliyejitangaza kuwa yeye ni gaidi wa Al-Qaeda, Mohamed Merah aliwaua wanajeshi wawili wa Ufaransa.

  Vichwa viwili vya nguruwe vilining'inizwa kwenye geti la kuingilia msikitini huku kiasi kikubwa cha damu ya nguruwe kilimwagwa kwenye sakafu ya kuingia msikitini.

  Waislamu walioenda msikitini kusali sala ya alfajiri jana jumatano walikumbana na vichwa hivyo vya nguruwe vikiwa tayari vimeishatundikwa kwenye geti la kuingia msikitini.

  Rais wa msikiti huo uliopo kwenye kitongoji cha Tarn-et-Garonne, Hajii Mohamed alilaani tukio hilo akisema haamini kama mtu mwenye akili zake anaweza akafanya kitendo cha kuishambulia dini ya kiislamu tena katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

  "Tukio kama hili kutokea ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kusema kweli halielezeki, ni tukio la kueneza chuki", aliongeza.

  Umoja wa wanafunzi wa Kiyahudi nchini Ufaransa nao umeungana na waislamu kulaani tukio hilo.

  Ufaransa ndio nchi yenye waislamu wengi kuliko zote barani Ulaya ikiwa na jumla ya waislamu zaidi ya milioni 4.[/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]

  [​IMG]  Vichwa Vya Nguruwe Vatundikwa Msikitini
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,896
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Duh, its too bad! matendo mengine bwana, si bora angeenda kumtafuta huyo aliyejiita al-qaed kuliiko kuwaharibia wenzke swaumu. Anyway, labda kuna kitu nyuma ya pazia.
   
 3. b

  bdo JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,211
  Likes Received: 1,176
  Trophy Points: 280
  Nina laani kitendo hicho walichofanyiwa waislaam wa Ufaransa, pia nina laani kitendo cha SMZ kuzuia waumini wa ndini zingine kutokuonekana wanakula katika mitaa ya Zanzibar na Pemba katika kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani
   
 4. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,571
  Likes Received: 269
  Trophy Points: 180
  Bora kutundika vichwa kuliko kujilipua na kuua watu kule Nigeria. Kichwa kimetundikwa tu kwenye geti hakijamgusa mtu ila wao wanajilipua wanaua watu wasiohusika. Madhara pekee yanayoonekana hapo ni kulazimishwa kuona nguruwe tena msikitini wakati wako kwenye mfungo na kusababisha wale walafi watamani kula ilihali muda bado
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,873
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ndhani aliyefanya hivyo hakuwa na akili timamu.
  Waislamu wamsamehe tuu.
   
 6. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,808
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 145
  Astaghfirullah
   
 7. Hansy wa East

  Hansy wa East JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 317
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  wanajaribu kupinga dini ya haki ila daima watashindwa na dini inaendelea kukua tena hukohuko Ulaya.
   
Loading...