Vichwa viwili na Sanaa ya Bongo

Landrover 109

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
366
565
Habari za week end wadau!

Katika tafakuri zangu kuhusu Sanaa yetu ya bongo, nimeona niandike Uzi mfupi kuhusu artists hasa wale wenye vichwa viwili( mabeberu wenzangu). Mwenyezi Mungu ametujalia vichwa viwili, Cha juu na Cha chini. Ukweli ni kwamba vyote viwili vinatakiwa kufanya kazi, lakini sio katika uwiano wa 50/50, Bali Cha juu kinatakiwa kutumika Zaid kuliko Cha chini.

Cha juu kikitumika sana kuliko Cha chini, kama msanii utajikuta unafanya kazi zenye ubunifu mkubwa na zinazoishi milele. Kwa wasanii wetu wa bongo inaonekana wazi mambo ni kinyume, wanaumiza sana Cha chini kuliko Cha juu, matokeo yake wanatulisha big G kila Ngoma na walaji tumekubali hasa ukizingatia ndio muziki ambao unasapotiwa na mfumo.

Utasikia pachika nitereze kama nyoka pangoni ,shemeji nakulaga, mwajuma mbona siku hizi hueleweki, nk. Wanajikuta inabidi wafanye matukio hasa na celebrities wa kike kutumia brands zao ili kutulisha udaku na big G.

Ushauri wangu Kwa wasanii wetu wa bongo, tumieni sana Cha juu kuliko Cha chini( kumbuka Cha chini hakina ubongo), Kwa kukilisha knowledge na wisdom, Kwa kusoma vitabu mbalimbali vinavyogusu dini, falsafa, siasa ,ujasiriamali, nk na Kisha myatumie maarifa hayo kutunga nyimbo zinazoishi.

Pia mashabiki wenu tunahitaji tusome vitabu vyenu, documentaries, vinavyogusu historia za kweli mlizopitia na kufika hapo mlipo, tunahitaji kuwaona mkicheza movies, Tv series, nk. Kwa wale wanaoona wanaweza kufanya Sanaa ya uigizaji.

Mwisho niwatakie wasanii wote baraka tele, Nina Imani 2023, mtakuja kivingine, ili walaji tupate chakula Cha ubongo.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Back
Top Bottom