KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 26,215
- 56,855
Ni dhahiri kabisa pasipo uhai hakuna maisha!,kwa maana maisha ni uhai.
Lakini lipo jambo moja tata kuhusu uhai!. Nalo ni kusudio la uhai.
Tukijaribu kuangalia mfano wa vitu vidogo ambavyo vimetengenezwa na binadamu bila kusita vitu hivyo utapata kusudio lake.. lkn jambo lakushangaza kitu ambacho ni maana nzima ya uukiumbe hai kusudio lake bado ni mtambuka!.
Nafahamu yameandikwa mengi juu ya kusudio la uhai wetu lkn hata hivyo bado yamekuwa si majibu yenye uthibitisho wa kutosha!.. kukosa kwangu kwa majibu hayo kumenifanya kila siku kufikiri juu ya kusudio la uhai,lakini napo bado sijapata jibu la uhakika.
Leo nimeangazia vichocheo tulivyonavyo labda vinaweza Kuwa kielelezo au njia ya kufumbua swali hili tata!.. si kwamba ninalo jibu, hapana Sina hata punje lkn itafaa zaidi Kama tukiunga fikra zetu labda tunaweza pata kitu kipya zaidi!.
Uhai wetu umeegemezwa na vichocheo mbalimbali,navyo ndio vimekuwa nguvu ya msukumo ktk maisha yetu,Ni ukweli ulio dhahiri vichocheo hivyo ndio chachu ya uhai wetu!. Kama kutakuwa hakuna vichocheo basi hata uhai unakuwa ni sawa na gari lililokosa njia au uelekeo wa kwenda!.. kwa ambao bado hawajajua nazungumzia nini ni Kuwa nazungumzia hamu ama hisia tulizonazo ndio vichocheo vya maisha.
Kama tusingekuwa tunahamu ya kufanya mapenzi basi kusingekuwa na uzalianaji!,Kama kula kusingekuwa na hamu au kuhisi njaa basi uhai ungetetereka na ama usingekuwepo kabisa!. hata wewe unafanya kazi ili upate hela ilikusudi utimize malengo yako na hayo malengo ndio tageti yako na hiyo tageti basi nyuma yake kuna kichocheo na nyuma ya kichocheo Kuna uhai!..
Sasa swali la msingi ni kwanini uhai uwe na matamanio(vichocheo) ili uzidi kukua(kwa maana ya kuzaliana)..?
Ukifikiri kiundani unaona kabisa mienendo yetu imekuwa coded!,juu ya swala la nani katufanya Kuwa hivyo (Kuwa coded) kila mtu anamajibu yake ambapo wengi wao huishia kusema Kuwa ni Mungu.. okay ni vizuri hata mimi ntaishia hapo lkn tutatofautiana ni Mungu yupi!! (Nimegusia tu hapo).
Kama vichocheo hivyo vyote vimesimikwa kwa misingi ya kuutetea uhai sasa kwa kuviangalia vyenyewe je,tunaweza kupata kusudio la uhai..?
Kwa kupitia vichocheo hivyo binadamu amekuwa ktk maendeleo ya vitu vingi,mfano teknolojia n.k hayo ni matokeo ya vichocheo lkn bado haileti picha ya kusudio la uhai wetu!.
Labda niandike hivi kama tupo ili tufaidishe kitu fulani basi kitu hicho ni kipi..?
Kama tupo kwaajili ya maendeleo basi maendeleo hayo anayafaidi nani ikiwa tunakufa..? Au hakuna msamiati faida ktk ulimwengu..?
Au ndo tuseme Kuwa kilichoumbwa ama kutengenezwa hakipaswi kujua kusudio la chenyewe kuwepo,isipokuwa alietengeneza akijua basi inatosha..?😅
Namaanisha kikombe hakijui kusudio lake kwanini kipo lkn binadamu akijua kusudio lake la hicho kikombe basi ndo inatosha..?
Kama ni hivyo Basi kwanini tuwe na kimuhemuhe cha kujua kusudio letu..?
Najaribu kuweka maswali ili kuleta utafakari lkn swali kuu ni kichwa cha mada hivyo haya mengine ni vichokozi tu ili kufikiri kwa upana..
Nimejaribu kuchokoza kwa upana wake na hayo ndio yangu machache,so karibuni kwa mjadala na majibu.