Ukiweza punguza au acha kabisa matumizi ya vyakula vya kuchoma na kukaanga

Wakuu kwanza kabisa niwe wazi mimi sio daktari wala sipo kabisa kwenye eneo la afya.

Habari hii ni kwa hisani ya vyanzo mbalimbali vya taarifa nilizosoma na kusikia.

Matumizi ya vitu hivyo ni mojawapo ya vichocheo vya ugonjwa wa kansa.
Kwa hivyo, Wamasai, Wamang'ati, Wachagga, Wakurya, wote wanakabiliwa na ugonjwa wa kansa?
 
Maana kuna mtu alisema tupunguze matumizi ya nyama (kula nyama). Sasa ukiangalia Watanzania wenyewe nyama wanazokula, mishikaki miwili, nusu kilo ya ng'ombe tunakula familia nzima tena siku 2.

On average mtu anatakiwa ale atleast kilo 75 ya nyama kwa mwaka. Ni kama wastani wa kilo moja na nusu kwa week. Ukizidisha hapo zaidi ndio unaweza pata shida kutoka kwa bwana nyama.

So na mtoa mada ungeweka vizuri kwamba chips kula kiasi iki, pizza kiasi hiki, etc kwa week au mwaka
 
Ulaji mbovu unapingwa kiafya sababu madhara utayaona umri ukishaanza gonga 45+
Ukiwa kijana system bado inachakata.
Hitimisho: Unapoishi upigie mahesabu uzeeni!
 
Ni kweli kabisa, saratani ya utumbo na puru (colorectal cancer).
 
Wakuu kwanza kabisa niwe wazi mimi sio daktari wala sipo kabisa kwenye eneo la afya.

Habari hii ni kwa hisani ya vyanzo mbalimbali vya taarifa nilizosoma na kusikia.

Matumizi ya vitu hivyo ni mojawapo ya vichocheo vya ugonjwa wa kansa.
Binafsi niliwahi kupata shida hiyo nikaelezwa smoked food inasababisha cancer nikiwa katika matibabu hapo HCG Mumbi- India.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom