Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,507
Mkuu KK, nafikiri umemwelewesha vizuri kama alikuwa hajui ukaribu wa baba mkubwa na mdogo, unajua watu waliozaliwa kwenye flat za Upanga hawawezi kujua boma ni kitu gani, hawajui kuwa Wazanaki, Wasukuma, Wamasai, Wakurya na makabila mengi zamani walikuwa wanaishi pamoja wanajenga nyumba kwenye boma moja karibu familia nzima. Watoto wa flat wao wanajua familia ni Baba,mama na watoto tuwengine wote ni ma uncle na ma aunt awe dada yako au binamu wote ni ma aunt. Sijui kweli makabila ya kusini labda wana tabia hizo za kizungu hawana cha mjomba wala shangazi.Aliyeanza kuongea mambo ya kitoto ni yeye Mkapa na imetusikitisha wengi kauli kama ile. Haki ya yeye kupanda jukwaa la kumnadi mwana CCM anayo hata kama ni Rais mstaafu but kauli zake hazikuwa na mshiko. Bahati mbaya viongozi wengi waliopo wamechafuka hakuna anayeweza kupanda jukwaani akasikilizwa hata kwa wana CCM wenyewe waliogawanyika. Mkapa kwa record ya utendaji anakubalika sasa wenzie wanaweza mtuma tuma ili naye pia achafuke. Hii nasema hivi kwa kuwa hata Mwigulu kwa umri wake asikabidhiwa majukumu makubwa yale lakini naye hajachafuka ukiacha udhaifu mdogo ambao vijana wengi wanao hasa wanapopata mafanikio kiuongozi kama yeye. Hata kina Zito, Mnyika wana viudhaifu vya ujana. Hapa Mkapa kama mtu aliosoma arts alipaswa kuchuja ya kuzungumza bado angaisaidia CCM. Mkapa huwa ana maneno ya namna hiyo hata 2010 pale jangwani kufunga mkutano wa kampeni wa CCM alitukana na mi nilikuwa nawambia watu tulookaa nao kadri alivokuwa anaongea jazba ilikuwa inampanda nikawanong'oneza kuwa sasa hivi anatukana namalizia tu akashusha kitu. Hivo lazima ajidhibiti sana kwenye maneno na washauri wake pia wamsaidie.
Kuhusu udhaifu wa hayo mengine ya kifo cha mwalimu ukweli hizo speculation zilishakuwepo muda mrefu na wengine wanatuhumu hata kipindi akiwa sayansi ya teknolojia wakati katibu mkuu akiwa Ngororo alikuwa hatoi kibali cha scholarship kwenda nje hadi utoe kitu kidogo. Naamini wapo walioathirika na hili na wanaweza kuliweka pia hapa kuthibitisha. Nadhani haya mbeleni ndo yalileta kiwira, anben nk. Tusiseme vcent ataumbuka na eti mtoto wa baba mdogo au mkubwa hawezi mzungumzia baba mkubwa, kwa ambao hawajafika Butiama ni kuwa wale wameisha pamoja ukoo mzima wamejenga nyumba hapo hapo pamoja kama familia. Haya maisha ndo yalikuwepo zamani baba alikuwa na wake wengi na wanaishi hapo hapo wote kwa hiyo kina Kiboko, kina Julius wote watoto wa mmoja na walikuwa wanaishi hapo hapo na hata nyumba ya mwalimu ipo hapo tofauti ni kuwa nyumba ya mwl ina fence nyinge zipo kwa nje lkn compound moja, nadhani angalau litaeleweka but waswahili wanasema akuanzaye mmalize.