Jamani WanaCCM na dola wasidandie ugomvi wa Vicent Nyerere na Mkapa hakika,yoyote atakaeingilia ugoomvi huo utammaliza vibaya sana,kwa watu wanaojua mila na desturi kwenye familia kama wote nyie ni watoto wa familia moja hata kama mmoja anamiaka hamsini na mwingine anaumri wa miaka kumi kwa kuwa wote ni wanafamilia basi wote wanahadhi ya kiti sawa ndani ya baraza la kifamilia.Wakiongozwa na kiongozi wa familia ambae daima uwa ndie mwakilishi wa familia.
Na kwa kuwa wote ni wakristu tena wa dhehebu moja la Roman Catholic,ili nalo ni jambo jingine jema,lakini ni baya sana kwa Mheshimiwa Mkapa ,kwa kuwa yeye na vicent ni mdogo na Mkapa ni Mtu mzima alipaswa kumuongoza mdogo wake vyema kiimani na kuwa wao kama wanafamilia mmoja akiwa ni aliyepokewa kama KAMBARAGE alivyoungana na BURITO basi kwa mmoja ametenda kosa kubwaa sana na msamaha wake si wa kupayuka mitaani au kutafuta watu wa kuzima mlipuko huo na mbaya mbaya sana Mzee tajwa yuko katika mchakato mgumu na wa muhimu sana kiimani katika maisha ya binadamu.
Sipati picha Vicent kapiga magoti chumbani kwake na rozari yake mkononi akimuombea baba yake mkubwa afanikiwe kupata daraja la kiimani katika dhehebu ambalo yeye Vicent na Mkapa ni waumini wake,uku akimuomba amuonyeshe majibu ya tamko la mkapa kumwambia yeye kuwa sio mwanafamilia wa Nyerere,wakati ni aibu sana kwa mtu ambae kidamu wana nasaba moja na Marehemu Baba wa Taifa.Kitu kizto ni kuwa Watanzania wote Millioni 45 ni WANAFAMILIA WA NYERERE kwa kuwa NI BABA WA TAIFA LA TANZANIA.Hivyo ndio kusema Vicent sio Mtanzania kwa kuwa kwa kuzaliwa tu mtanzania tayari umeshakuwa ni mwanafamilia wa Nyerere.Kwa kuwa Taifa uwa halina Baba wa Taifa wawili ni Baba wa Taifa mmoja tu nae ni BABA MKUBWA WA VICENT NYERERE.
Hakika hakuzaliwa kwenye ukoo huo wa Nyerere kwa bahati mbaya Mungu alkuwa na sababu zake [It happen for a reason].
Ushauri wangu kwa Mzee Mkapa atimize hizi njia TATU kuomba TOBA ya kweli
1: KUPITIA NJIA ZA KIIMANI [KANISANI]
Kutubu [Kitubio] kanisani mbele ya kiongozi wake wa kiimani kanisani kwake,kisha kukili kilichoko moyoni na dhamira yake ya kutamka hayo kwa nia ya dhati kusudio lake lilikua nini.Kupitia toba hiyo pia aombe kiongozi wake wa kiimani kuwaalika wnafamilia wa Mwalimu wote na kusali nae misa maalumu itakayompa mwafaka wa nafsi ya yale yaliyomo ndani ya mioyo ya wanafamilia wa Mwalimu.Lakini atoe toba halisi na kwa kuwa yeye ni muumini wa Roman Catholic, si wa kufundishwa toba ni nini.
2: KUSULUHISHA KIFAMILIA [NJIA ZA KIJADI MWITONGO]
Kutatua mgogoro wake huo kwa njia ya kifamilia [Ina maana jadi ya kizanaki lazima ifanyike kwa Mwanafamilia kumtamka Mwanafamilia Mwenzie kuwa sio Mwanafamilia Mwenzie mbele ya hadhara uku mwanafamilia aliyetamka hayo akiwa na hadhi ya utu uzima na mbaya zaidi alipata kuwa Rais wa Taifa.].Kupitia Chief wao watamuunganisha upya kwa kusudio la kumjenga kama binadamu na si kama Rais Mstaafu.Manake tunakoelekea yale ambayo yako mioyoni mwa Wanafamilia na baadhi ya Wananchi ni ishara kuwa sio shwari kwake.
3: KUOMBA MSAMAHA KWA UMMA
Baada ya kupitia hatua hizo tatu basi mzee huyo ajitokeze mbele ya umma hakika kwa toba ya kweli kanisani na kwenye familia umma utampokea na kukubali kuwa nae kama binadamu kuna matendo aliyoyatenda kwa wenzie yalikuwa ni kiovu mbele ya wanajamii pamoja na yeye kuwa Rais hakuwa Mungu wala Maraika.
Tatizo la Taifa letu ni pale viongozi wetu wanapotaka kuoenekana ni watakatifu na kuwa wao siku zote wako sawa na kuwa hawatende uovu na mabaya dhidi ya wengine hakika hilo kosa uwa ndio msaraba wao daima hawachelewi kuishia na skandal mbaya na za aibu zinazoziandama mpaka familia zao.
Inawezekana timiza wajibu.
Kwa wale wenye imani ya kikristu wanajua kuwa Yesu hakuja kwa wema.!!!!!!!!