Vicent amlipua Tendwa, Mkapa aomba suluhu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vicent amlipua Tendwa, Mkapa aomba suluhu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Mar 17, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Vicent Nyerere amemlipua Msajili wa Vyama vyaSiasa, John Tendwa, kwa kimzuia kumzungumzia Hayati Mwalimu Nyerere.
  Amemshauri kuwa kama anahitji kuwa mmoja wa familia yao, anaruhusiwa kuandika barua kuomba kujiunga na ukoo wao kama alivyofanya Mkapa.

  Alisema anamshangaa Tendwa kumpiga marufuku kuongelea mambo ya baba yake na kulidanganya Taifa kuwa watahatarisha amani nakujenga chuki kwa Taifa kwa kumzungumzia Nyerere.

  "Mimi huyu ni baba yangu na kila siku lazima nimtaje na sisi wakatoliki tuna sala maalum ya kumwombea Nyerere na leo (jana) pia nimesali mara baada ya kuamka, sasa yeye ni nani anayenizuia kutaja jina lababa yangu, kama anataka ajiunge na ukoo wetu aombe kwa barua, kama alivyofanya mwenzake Mkapa, aliandika barua akaingizwa katika ukoo,"alisema Nyerere.

  Akimnadi Nassari katika mkutano wa hadhara wakampeni, Vincent Nyerere, ambaye ni Meneja wa kampeni za mgombea ubunge waChadema Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, jana alisema kuwa Mkapa amemfuata Joseph Butiku kuomba amuombea msamaha kwake (Vincent). Alisema kuwa Mkapa alimweleza Butiku kuwa alikuwa anamtania ingawa mbunge huyo aliichukulia kauli ya Rais huyo mstaafu kama ya kweli.

  "Huyu Butiku jana (juzi) alinipigia simu akiniomba tuachane na haya mambo ya malumbano kwa sababu Mkapa alikuwa ananitania na hakujua kama itakuwa hivyo, na mimi nimeendelea kulisema hadharani, sasa anaomba basi yaishe,"alisema Nyerere katika mkutano uliofanyika katikakijiji cha Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni.

  Alisema kuwa amekataa kuombwa radhi kupitia njia yasimu au kukutana wawili na kuongeza kuwa anachotaka ni Mkapa kwenda Arumeru kuomba radhi katika mkutano wa hadhara ambao aliuhutubia na kumchafua kuwa hanaundugu na Hayati Mwalimu Nyerere.
  Aidha, alisema Mkapa anapaswa kuwenda kumuomba radhi kwenye ukoo wao. "Mimi ni wa ukoo wa Nyerere atake asitake, Nyerere ni baba yangu na sitaacha kumtaja kamwe," alisema Vincent.

  Alisema kuwa Mkapa alikuwa anamheshimu sana kama Rais mstaafu na alifahamu anahitaji kupumzika, ila kwa kumgusa kwa hilo nakumchafua hadharani kuwa anajifanya mtoto wa Nyerere, wakati hamfahamu, kwa hilo aende katika ukoo kumsafisha.

  Gazeti la Nipashe
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,496
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Vicent my bro it's enough to him strategically! Go on kill them all!
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Yaani Mkapa aombe radhi kwa kumuua BABA WA TAIFA!! Adhabu pekee inayomfaa huyu UGLY CREATURE ni KUNYONGWA TU.
   
 4. S

  STIDE JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mh!!! Kumbe Bwana mdogo ni nomaee!!!??
  WBM hawezi kwenda kuwakutanisha wanaukoo maana anajua wanajua A-Z ya kifo cha JKN!! WATAMLIPUA!!
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo Vincent anaona ni kuzaliwa kwenye ukoo wa Nyerere ni kitu cha maana sana! Maana sioni kama anatoa hoja yeyote ya maana. Ingawaje watu wanachekelea domo lake linavyosema ovyo kumchafua Mkapa kwa hoja za kitoto, ajue anamchafua zaidi huyo Nyerere ambaye anamwita baba yake. Iko siku atajutia maneno yake na sidhani kuwa mtoto wa baba mdogo ana haki ya kumuongelea baba mkubwa kuliko wanaye wa damu.
   
 6. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Hii akili au matope, eti alikuwa anatania, anatania yupo jukwaani akiongelea mambo serious kama yale?
  Hapa nina wasiwasi isijekuwa hata hizo ahadi zao kwenye kampeni zao nazo ni utani mtupu..
  Mtu mzima hofyoo kabisaa.. Alaaah
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkapa aombe RADHI kwa kumtuma mkutano wa hadhara kama alivyofanya yeye kumchafua kamanda Vicent, tena iwe pale pale Arumeru.
   
 8. M

  MACHUPA Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aliyeanza kusema maneno ni bwm sasa vincent anajibu
   
 9. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hot issue JF kwa sasa ni ufisadi ndani ya CDM, haya mengine hayana mashiko kwa sasa
   
 10. s

  selopheady Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama zege kalikologa Mkapa kwa kuongelea mambo ya ukoo kwenye siasa. Sasa inabidi zege isilale mpaka kieleweke.
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mtoto wa baba mdogo haruhusiwi kumuongelea ba mkubwa ila litoto lililoomba undugu linaweza kuongelea baba asiyemuhusu
   
 12. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Jana nilisema Tendwa siingilie asije akawa victim, Tendwa anazidi kumwagia petrol kwenye moto tena kwenye upepo mkali anajua watu wako kwenye kampeni wakati huu kuna platform la nguvu la kusambaza ujumbe, yeye anainglia kama nani aache wana ukoo watayamaliza wenyewe.
   
 13. F

  Froida JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kwa ni yeye amewahi kutangaza au kujigamba kwamba ni mwanafamilia ya Nyerere : huyo baba yenu Mkapa aliyetaka kumshusha hadhi kumfanya mwanaharamu mumuonye kama alikwenda huko akampa ubani wakati wa kifo cha baba yake ambaye alikuwa rafiki Mkapa mwenyewe atafanyaje swala la ukoo wa Vicent kuwa ni hadidu rejea za Kampeni CCM wote ni matahira tuu ndio maana nchi inauzwa kama njugu upuuuzi mtupu kwa raisi kujishusha kiasi hicho
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkapa anasema alikuwa anatania pale aliposema kuwa Vicent sio mwanafamilia ya Mwl Nyerere. Kwa maana hiyo yale mengine aliyowaahidi wana Arumeru Mashariki nayo ni utani? Ni hivi;
  1. Mkapa alisema kuwa tatizo la ardhi Arumeru analifahamu na atamweleza rais Kikwete - huo ulikuwa ni utani?
  2. Mkapa alikataa kuwa hamiliki ardhi huko Arumeru - nalo ni utani?

  Arumeru miaka 50 ya utani mmeona matokeo yake, uchaguzi ni wenu, ama kuendelea na utani au kufanya kweli na kuinua maisha yenu.
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hivi Benki kuu wamesema mfumuko wa bei ni asilimia ngapi hebu Kamuulize Jakaya Mrisho Kikwete anafanya nini pale magogoni kuuza kila kitu bado kuuza hewa ya Tanzania tuu ,hazina chapa haina kitu
   
 16. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hizo ni hot issue kwa nyie mliopo ndani ya box ambapo fikra zenu hutegemea ukubwa wa box lenyewe.
   
 17. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Usilazimishe issue watu wana uhuru kwenda jukwaa au thread wanayotaka kuchangia au kusoma.
   
 18. c

  collezione JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kumbe kampeni zote ni utani???
  Duh,
   
 19. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeamini kuwa Ulimi ulimponza kichwa.
   
 20. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #20
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Acha umasaburi kama hujui maana ya ukoo omba watu wakupe semina elekezi. Lakini naona tatizo baba yako alitengwa na familia yake ndo maana akakurithisha chuki ya kutokuwapenda wakubwa na madogo zake (shangazi na baba zako). Pole ndugu kwa kukosa uanafamilia.
   
Loading...