Barabara za Kenya Wakati huo huo, idara ya polisi nchini Kenya imetangaza ratiba ya usafiri wakati wa mkutano huo wa kimataifa.
Barabara kuu kati kati mwa mji mkuu wa Nairobi na zile zinazoelekea, katika makao makuu ya umoja wa mataifa mjini Nairobi zitafungwa wakati wa mkutano huo, na idara hiyo imetoa wito kwa Wakenya kujiepusha na shughuli katikati mwa mji na maeneo ya mkutano huo kuanzia siku ya ijumaa hadi siku ya jumapili.BBC