inabidi tu leo niseme mwanamke mimi! eti mimi nimewabatiza wanawake wote wanotembea na waume wa wenzao na kuwaita vibaka wa ndoa! is it a very negative name au ni sawa? kwa nini hatwtulii nao wakapata waume zao, kutwa kucha kuleta mpasuko kwenye ndoa za wenzao? na walio wengi, hata ukiondoka ukawaachia, they cant even make a wife and a home!du!
Ni vibaka tu, na wataishia kuwa vibaka wasipomkubali Mungu, hawajitambua wanajidanganya mioyo yao, kwa ujinga wao, na hao waume wasiojitambua wasiojua kupenda na kujali familia zao. Wanawake wanaotembea na waume za watu na hata wengine kuwa wake wadogo wanajidanganya na kufa kwa mawazo kwa sababu siku zote wanaishi kwa mashaka, wanahitaji maombi, tembea na mume wa mtu,zaa nae hata ukiweza olewa kabisa lakini ukweli ni kwamba hutakaa uwe na amani, hutakaa uwe mke mkubwa,haijalishi mke anamatatizo gani hawatakaa wafanane nae ndo maana mara zote wamejaa stress kwa kuiba waume za watu.
Na nikweli ukimwachia hata akidumu lakini anaishi kwa kukosa amani na kutojiamini kwa sababu mwanamke anayejitambua hawezi kuhangaika na waume za watu ni kibaka tu mpaka Neema ya Mungu ikimpitia ndo afunguke. Mimi nawahurumia hao vibaka wa ndoa wa kike kwa wakiume, ukiona m-baba anavyohangaika na vidumu kwa upendo wa kinafki wanahitaji maombi kwa kweli waondokane na ukibaka.
Na huwa nashangaa wanawake kujitesa kuhangaika na mume wa mtu mwisho unaumia mwenyewe. wanazalishwa na kuanza kulilia haki za mke mkubwa nawapa pole sana. Ni aibu mpaka watoto wao wakikuwa wanaelewa mama alikuwa hajatulia, mama alinizaa kwa mume wa mtu.sijui huwa wanawaambia nini watoto wao, Raha ya mume awe wa kwako mwenyewe, hakuna mwanamke anayependa kushare. Na waume vibaka mjue hakuna mwanamke anayependa kushare, hata kama wako na wewe moyoni na machoni hata hao vidumu huwa wanawadharau, na wake zenu pia hata akiendelea kuwa na wewe anakudharau, ndo maana wanaume wengi wanakufa ovyo kwa presha walizojitafutia wenyewe. na mara zote mwisho wa hao vibaka unakuwa mbaya sana.
Na wanaume vibaka wa ndoa zenu wenyewe,mnaotesa wake zenu na kuvunja maagano mliyotamka na kukiri mbele za Mungu, mpaka maofisini na mtaani mlikubali kuwa huyu ni mke wangu tena uka sign ndoa ya mke mmoja leo mnahangaika na wanawake wengine mtubu mumrudie Mungu.
Mwisho nawapa pole manawake wote walioolewa na wanaume wanaotoka nje ya ndoa. Mtumaini Mungu siku zote atakuinua.simama katika nafasi yako kama ikupavyo si kushindana na vibaka, mume anayetoka nje ya ndoa yake hiyo aibu itabaki kwake na hao vibaka wenzie. waombeeni hao vibaka ushetani uwatoke. Hata mume akikuacha kwa ajili ya kidumu, we mtumaini Mungu akikupa amani ya kweli simama lea watoto usisononeke kwa dhambi ya wengine.