Wakuu heshima mbele
Nilikua napita tu ila nimeona si vibaya tukawekana sawa kwenye hili swala na sio kulaumu tu. Tatizo sio mkongo wa taifa wala infrastructure ya smartcard, unayesema hivyo nadhani hujui hivyo vitambulisho vinafanyaje kazi. Kimsingi ni kuwa huo utaratibu ulishaanza katika hatua ya awali ambayo ni ya kutengeneza database kwanza na mikoa ya Dar na Moro(Nadhani Kilombero peke yake) walishaanza kuandikisha na uandikishaji unafuata utraratibu huu
1.Unaandikishwa makazi(Daftari la makazi la mataa limerudishwa kama miaka ile yetu)
2.Baada ya hapo wanachukua taarifa zako nyingine pamoja na supporting information kwa ajili ya verification
3.Then after verification kwenye database nyingine zilizopo tayari wanarudi kuchukua fingerprints
4.Inatengenezwa database ya taifa zima
5.Ndio unapewa kitambulisho(Kikadi) kwahiyo ishu ya muhimu sio kile kikadi bali ni taarifa za ujumla za muombaji na hii inachukua muda kuthibitisha
Kwa mkoa wa Dsm watu waliandikishwa kwa hatua ya kwanza walikua 7m kwa kupita kwenye makazi ila katika hatua ya pili kwasababbu ya mapuuza ya waTanzania kama kawaida yetu walikwenda watu millioni 2 tu mpaka muda ulipokwisha.
Muda utaongezwa tena ila kwa sasa walisimamisha kupisha zoezi la sensa kwakua NIDA nao ni washiriki na baadhi ya data zitatumika.
Muda sio mrefu uandikishaji utaendelea Dar kwa wale waliokosa
Lokissa nimejaribu kuelezea kwa kifupi hapo na teknolojia ya smartcard inayoongelewa sio complicated ni kama lesseni mpya za magari tu zilivyo. Ishu ni registration yani kwenye jina pamoja na fingerprints.Nadhani kama ni mfanyabiashara utakua umegundua lesseni mpya za biashara kuandikisha ni mpaka uweke fingerprints pia hiyo ni sehemu ya huu mradi wa NIDA pia. Logic ni kuwa na uwezo wa kuonganisha idara hizi kwa pamoja..TRA,,NEC,NECTA,NACTE,Immigration, Bureau of Statistics pamoja na wale wazee wa mitaa/wanaitwa wenyeviti nadhani na hiyo database ndio itakua controled na NIDA kwahiyo ni mradi mkubwa kuliko watu wengi wanavyofikiri na wanakomaa na Dar wakifanikiwa hapo wanajua watafanikiwa Tz nzima