Habari za jioni wapendwa,
Huyu baba ni mzee wa 60+ lakini pesa imemtembelea, si pesa hii ya kubadilisha mboga tu, hapana ni pesa ndefu, kila mwaka birth day yake anajipa treat ya Range Rover mpya ni mfano tu wa maisha anayoishi. Baba ana mke, watoto na wajukuu, lakini si unajua adabu ya pesa ameama kuwa mzee kijana.
Baba amepata kitoto cha chuo kikuu, sikujui kitoto kile kimempa mahaba gani mzee ambayo hajawaji kuyapata, mzee amechanganyikiwa kabisa kwa katoto ambacho kanaweza kuwa kitoto chake cha mwisho au kijukuu.
Kila alichotaka mtoto alipewa, sasa bwana, weekend moja mzee ameshachukua chumba hotelini akapumzike na mtoto. Mama nyumbani ameambiwa ni business meeting. Mzee amenunua Viagra aweke heshima kwenye mechi.
Goli la kwanza halijafika, mzee mapigo ya moyo yamebadilika, mzee chali kitandani. Mtoto akaona hili soo, alivyokuwa jasiri, katoto kalichukua face towel na kuanza kumfanyia mzee towel bath ili kupoteza ushahidi wa DNA zake. Mzee amekata roho kitu kikiwa katika 45 degree angle. Mtoto amevaa nguo, amechukua kile ki face towel huyooo kapotea.
Nyumbani wanamtafuta lakini mama alijua business meetings nyingi za mzee zinafanyika hotelini na akichelewa analala huko. Mhudumu wa hoteli aje afanye usafi ndiyo anakutana na maiti. Kujulikana ni nani, familia kupigiwa simu. Mama hana hamu, anaonyeshwa maiti ya mumewe kwenye shuka bado kitu kiko 45 degree angle.
Mwangalie afya zenu kwanza kabla ya kumeza haya ma Viagra.