Vetting ya viongozi sasa inatia mashaka!

Vetting ya viongozi sasa inatia mashaka!

Hakuna vetting nchi hii,zile teuzi za mkwere na teuzi ya huyu mchato zinafanana sana,teuzi ambazo hazina maslahi kwa umma,zimejaa ukabila,udini,ukanda tu. Teuzi za ovyo kabisa.
 
Kama ikidhibitika
Nadhani kuna haja kama taifa
Tuwe na mjadala mpana
Ya namna gani ya kufanya vetting ya kupata viongozi wetu
Nadhani kutakuwa na tatizo mahala


Possibly kuna genge la watu fulani wenye dhamira binafsi
 
Hili tatizo la vetting ni pans sana! Maana hata huko ukawa walimpokea mgombea urais aliyekatwa chama kingine kwa tuhuma mbali mbali! Kama hiyo hitoshi wakampokea na mwanachama mwingine mwenye tuhuma!
 
Sidhani kama kuna vetting siku hizi. Vetting ilikuwa inafanywa kipindi cha nyerere, sikuhizi ni ushkaji tu
 
Mwalimu alipokuwa anateuwa watu ilifanyika vetting ya kweli alizingatia regional balance na competence na hii ilisaidia na ndiyo maana aliweza kuwandaa vijana na wazee kwenye maaadili hakuwajali wa wale wa karibu yake lakini kwa vitendo aliwateu majasiri kutoka kila kona ya nchi kwa usafi wao na uadilifu wao.Turejee maandiko yote ya Mwalimu tuisome tujue kinacho hitajika tuzifahamu nyufa na tujisahihishe.. Viongozi akituhumiwa ajiuzulu apishe uchunguzi Mzee Mwinyi alifanya hivyo na leo hii ni kipenzi cha Watanzania. Tuwe fair tumpe kijana muda vyombo husika vifanye kazi tutajulishwa. Vita aliyovianzisha ni nzuri anastahili kuungwa mkono pengine alikosea kwenye njia lakini kila kitu kimesahihishwa.
We unaamini kuna vetting inafanyika Tanzania? Siamini hivyo. Kama ilipata kufanyika basi ni enzi za mwalimu huko labda na mwinyi. Vetting ya kitanzania ni ushkaji na kukisaidia chama.
 
Paul anaweza kuwa na vyeti fake sawa , lakini sio makosa yake..
wenye makosa ni wale walio mteua na kumfikisha hapo..

Kwa sasa hii hesabu kuisolve ni ngumu sana, wala tusifananishe na ile ya kitwanga.

akimtumbuliwa ni kumweka Paul katika hatari ya kuozea jela.

Ana kesi mbili zote anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya.

Kwa sasa anatetewa na serikali, nje ya serikali hataweza kulimaliza hili.

Paul bado ni kijana mdogo, angalia anavyo tapatapa kama mbwa aliyejiingiza kwenye zizi la simba kimakosa. Mara ananyenyekea akiwa ameshikwa mikono na baba mtakatifu wakati yeye alijiita Mungu, Mara kuna watu 12 wanataka kumroga kwa majini, hii yote ni dalili kuwa anajua makosa yake na anajutia.

Sipendi ni mhukumu Paul lakini naliona tatizo la kielimu pia, hapa ndio unaona umuhimu wa shule halali kwamba humsaidia MTU kuina vitu in 3D in advance. Sasa mambo ambayo yalitakiwa yafanywe na monita wa darasa LA pili yanakuja kufanywa na mkuu wa mkoa.

Nadhani hili ni somo kwa vijana wengine wanao pewa dhamana ambazo hawakustahili. Hapa ndipo utakapo mwona Nape kama bonge la kiongozi.. Gud morning
Morning sir, karibu supu mazee! Kuna mahali nimechangia maoni yangu kwamba: kwa namna ya utendaji wa Bashite suala la vielelezo kwa maana ya vyeti ni nyongeza tu, lakini ushahidi wa kwamba hamna kitu upstairs upo katika utendaji wake! Inashangaza kuona hata wateuzi wake eti wanamwona kuwa ni "jembe"!
 
Hili sakata la vyeti vya Paul Makonda linatia mashaka kwa sisi tunaoiunga mkono serikali ya awamu ya tano.

Mtu unajiuliza amepita pitaje vikwazo vya vetting.
Tunajua fika kuwa hata kama kiongozi hakupikwa chamani, lakini anachunguzwa sana maisha yake kiujumla.
Tusipokuwa careful tutapata viongozi si wasiostahili tu, bali majambazi.

Mbya zaidi hili suala la vyeti vya Makonda hakuna aliyelitolea maelezo ya maana, ukitilia maanani kampeni ambayo haijaisha ya vyeti feki.
Hakuna cha Vetting ni kujipendekeza tu unakula shavu.... ikiwemo kufunga viatu vya wakubwa
 
...ndio sababu tulisema tangu mwanzo kwamba ule uhakiki wa vyeti ungeanza na viongozi... Ili wawe mfano...

...sasa ona watumishi walio wengi wasio na shida na vyeti wamesimamishiwa stahiki zao wakati kuna viongozi kama hawa kina bashite wamefoji cheti na wanafurahia huduma za serikali na kuleta shida kubwa kwa watu kupitia ujinga na jeuri yao...

...nchi bado sana hakika....hatutafika kwa mtindo huu....ambapo waliofoji vyeti wanapewa dhamana ya kuwaongoza wenye elimu na vyeti halali...


...hizi double standards zinaiua hii nchi Walah....
 
Mwalimu alipokuwa anateuwa watu ilifanyika vetting ya kweli alizingatia regional balance na competence na hii ilisaidia na ndiyo maana aliweza kuwandaa vijana na wazee kwenye maaadili hakuwajali wa wale wa karibu yake lakini kwa vitendo aliwateu majasiri kutoka kila kona ya nchi kwa usafi wao na uadilifu wao.Turejee maandiko yote ya Mwalimu tuisome tujue kinacho hitajika tuzifahamu nyufa na tujisahihishe.. Viongozi akituhumiwa ajiuzulu apishe uchunguzi Mzee Mwinyi alifanya hivyo na leo hii ni kipenzi cha Watanzania. Tuwe fair tumpe kijana muda vyombo husika vifanye kazi tutajulishwa. Vita aliyovianzisha ni nzuri anastahili kuungwa mkono pengine alikosea kwenye njia lakini kila kitu kimesahihishwa.
Mkuu nakubaliana kabisa na wewe.
Wakati wa Mwalimu kuna kada Fulani ya viongozi ambao ukiwatazama usoni, unaamini kile wanachokuambia.
 
Aliemuingiza kwenye system ni JK,uyu wa sasa kampandisha cheo tu bila ya kuhakiki historia ya uyu jamaa.
dada06efe8a94ae0b0852c34597ab5ef.jpg
 
Mwalimu alipokuwa anateuwa watu ilifanyika vetting ya kweli alizingatia regional balance na competence na hii ilisaidia na ndiyo maana aliweza kuwandaa vijana na wazee kwenye maaadili hakuwajali wa wale wa karibu yake lakini kwa vitendo aliwateu majasiri kutoka kila kona ya nchi kwa usafi wao na uadilifu wao.Turejee maandiko yote ya Mwalimu tuisome tujue kinacho hitajika tuzifahamu nyufa na tujisahihishe.. Viongozi akituhumiwa ajiuzulu apishe uchunguzi Mzee Mwinyi alifanya hivyo na leo hii ni kipenzi cha Watanzania. Tuwe fair tumpe kijana muda vyombo husika vifanye kazi tutajulishwa. Vita aliyovianzisha ni nzuri anastahili kuungwa mkono pengine alikosea kwenye njia lakini kila kitu kimesahihishwa.
Kna haja ya kuanza kuwa na Public Hearings kwa wateule walio kwenye nafasi nyeti.
Utaratibu kama ule wa Marekani ni mzuri sana, mtu naye anajipima na kuona kama anatosha.
Akiona viwango havifikii matarajio, mtu anajiengua mwenyewe kwa manufaa ya umma.
 
subiri CWT walipwe fidia zao wanadai pesa nyingi serikalini......kwenye kampeni za Tanzania ya viwanda 2lisema hakutakuwa na migomo na si hilo 2 pia wanafunzi wa vyuo vikuu wangepata mikopo bila kubagua kwa hiyo 2mesikia kuna waliobaguliwa sasa nao 2nataka 2cwabague......haaaaahaaah!nmekumbuka,pia 2liahidi milion 50 kila kijiji 2nafanya utaratibu iwe kila kaya.....2mewaahidi ndugu zetu watanzania hatutawaangusha.....haiwezekani kabisa mwekezaji anapewa kiwanda anafugia mbuzi na kondoo lazima wavirudishe haraka......Ila subirini kwanza 2malize kuhamia dodoma serakali mathalani 2megundua kitu wizara zetu zinabidi zikasome pale yudom na bodi ya chuo ime2kabidhi baadhi ya majengo km hosteli za wizara.
 
Hili sakata la vyeti vya Paul Makonda linatia mashaka kwa sisi tunaoiunga mkono serikali ya awamu ya tano.

Mtu unajiuliza amepita pitaje vikwazo vya vetting.
Tunajua fika kuwa hata kama kiongozi hakupikwa chamani, lakini anachunguzwa sana maisha yake kiujumla.
Tusipokuwa careful tutapata viongozi si wasiostahili tu, bali majambazi.

Mbya zaidi hili suala la vyeti vya Makonda hakuna aliyelitolea maelezo ya maana, ukitilia maanani kampeni ambayo haijaisha ya vyeti feki.
Kwani hawako hao viongozi majambazi!
 
Hii ni kuonyesha kuwa ndani ya serikali ya Rais Magufuli kuna watendaji wanaompiga vita sana Rais kwa kutowajibika, wanampa wrong information knowingly else hii ya Makonda ingejulikana mapema wakati wa vetting!!! Rais Magufuli take care umezungukwa na maadui wengi kwa kazi nzuri unayoifanyia Watanzania.
Makonda aliteuliwa na Rais Kikwete!
 
Kama ikidhibitika
Nadhani kuna haja kama taifa
Tuwe na mjadala mpana
Ya namna gani ya kufanya vetting ya kupata viongozi wetu
Nadhani kutakuwa na tatizo mahala
Hayo mambo ya mijadala rasmi inatupotezea tu muda, sisi tunapiga hapahapa...tukimalizana na bashite mdogo tutaelekeza nguvu kwa bashite mkubwa nae atueleze phd yake ya chemistry aliipatajepataje pasipo kuingia maabara!
 
hata elimu ya boss wake haipo straight sana, ya kupinda pinda sana....

pia tujiulize, huyo ni Daudi wa dar, vip wale waliopewa nyazifa za ndani huko vijijin, na kwenye halmashauri zilizo ndani huko, ambako wananchi hawajui A wala Be....

ni hatar sana, alafu tunakuja kuambiwa kuwa alichukua muda mrefu kufuatilia na kwa umakini kufuatilia weled wa wateule wake
 
Unajua wapigaji kazi wapo sehemu nyingi sana,linalo wakwamisha ni vyeti.Sasa isiwe kwa fulani iwe sawa kisa kafichua madawa ya kulevya.Sisi tunataka mtuelewe Makonda siyo Mkuu wa mkoa,alie mkuu wa mkoa ni Bashite.Na bashite alifeli,na mamlaka hazipaswi kuwa na kiongozi muongo,katudanganya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom