VETA wagundua Dawa: Usipovaa Kofia ngumu Pikipiki haitawaka

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
pic+veta.jpg

Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka Mamlaka ya elimu na mafunzi ya ufundi (Veta) kituo cha Kipawa jijini dar es Salaam, Aneth Mganga, amegundua teknolojia mpya ambayo itakuwa mwarobaini kwamadereba pikipiki ambao hawapendi kuvaa kofia ngumu.

Kwa kutumia teknolojia hiyo, mwendesha poikipiki asipovaa kofia ngumu, basi pikipiki anayotaka kuiendesha haitawaka.

Kwa mujibu wa mwalimu huyo, teknolojia hiyo mpya haipatikani mahali pengine popote duniani.

Akizungumza katika banda la veta katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi, mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika utapunguza madhara yanayotokana na ajali za pikipiki.

“uzuri wa teknolojia hii ni kuwa hata anapokuwa katika mwendo, dereva akivua tu kofia ngumu, pikipiki inazima,” anafafanua mwalimu Aneth.

Amesema kwa upande mwingine teknolojia hiyo inazuia wizi wa pikipiki kwa sababu mwizi hatoweza kuiwasha pikipiki hiyo mpaka awe na kofua ngumu ambayo imeunganishwa kielektroniki na pikipiki husika.

Mwalimu Aneth ameiomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili kueneza teknolojia hiyo na kusaidia kampeni zirtakazoifanya ikubalike katika miongoni mwa waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini.

Akielezea juu ya gharama ya vifaa vinavyotumika kutengezeaa kifaa hicho, mwalimu Aneth alisema kuwa kwa sasa vifaa hivyo vinapatikana nje ya nchi na anatumia fedha nyingi kuviagiza kwa sababu huagiza vichache.

“Naamini kama utawekwa utaratibu utakaowezesha kuviagiza kwa wingi, bei yake itapungua sana,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
good, tunahitaji watu km nyie tz, sio wapiga kelele

Sent From Ikulu-Magogoni street
 
Saaaafii sana akitangaze clsuzi naamini watapata promoo

sent from my iPhone 6
 
Ili kuwa Na wanasayansi wengi zaid wazawa, inabidi tuendelee kwa miaka kumi zaidi kuwanyima mikopo wote wasiosoma sayansi.
 
Veta na watu wengine wanazindua na kutengeneza vitu vizuri sana ambavyo utaviona kwenye maonyesho tu baada ya hapo vinawekwa stoo.
Nakumbuka enzi za mkapa niliwahi shuhudia mashine za kukandamiza barabara zilizotengenezwa na kitengo cha uhandisi udsm zikiwa aina mbili Magufuri 1 na magufuri 2 lakinj baada ya hapo sikuwahi kusikia zimeishia wapi.
Tatizo serikali yenyewe haiamini katika kutumia vitu vilivyo tengenezwa nchini wao ndiyo wana discourage maendeleo ya science hapa maana wanaagiza kila kitu nje.
 
Biashara ya Helmet maalum hiyooo, inakuja.
Maana itabidi hiyo helmet iwe imeunganishwa na ignition system ya pikipiki. Ni kama ufunguo wa pili.
Helmet ikipotea, lazima ukanunue helmet yenye "connection" hiyo at specific outlets.
 
Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka Mamlaka ya elimu na mafunzi ya ufundi (Veta) kituo cha Kipawa jijini dar es Salaam, Aneth Mganga, amegundua teknolojia mpya ambayo itakuwa mwarobaini kwamadereba pikipiki ambao hawapendi kuvaa kofia ngumu.

Kwa kutumia teknolojia hiyo, mwendesha poikipiki asipovaa kofia ngumu, basi pikipiki anayotaka kuiendesha haitawaka.

Kwa mujibu wa mwalimu huyo, teknolojia hiyo mpya haipatikani mahali pengine popote duniani.

hongera huyo mwalimu asee

E bwana ee. Hii safi sana, ugunduzi mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app

good, tunahitaji watu km nyie tz, sio wapiga kelele

Sent From Ikulu-Magogoni street

Saaaafii sana akitangaze clsuzi naamini watapata promoo

sent from my iPhone 6

Huyu mwalimu kama hakunukuliwa vibaya hafai kabisa kwa mujibu wa maelezo yake. Sababu kubwa ni kwamba hiyo teknolojia ipo sehemu nyingine tayari, labda atuambie kuwa yeye ndio wamemuiga. Lakini kuna video zimekuwa published 2014.

Anashindwaje kusema kuwa waige hiyo teknolojia kutoka huko kwingine badala ya kusema yeye ndiye mgunduzi? Au ana maanisha yeye ndie wa kwanza kuleta hilo wazo au teknolojia nchini kutoka huko nje ya nchi.

Bila mtandao wa intaneti tulikuwa tumeingizwa mjini. Na kama amepata academic promotion kwa jambo hili, inabidi avuliwe wadhifa huo.

Tazama video clips hapa chini ili unielewe vizuri.





 
Back
Top Bottom