VETA Mwanza mmelala,kuna vyuo uchwara pale mjini kati

VETA Mwanza mmelala,kuna vyuo uchwara pale mjini kati

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,731
Reaction score
8,835
Taarifa ziwafikie VETA Mwanza

Mnalala sana kuna vyuo pale mjini ni vya kishenzi havizingatii mitaala,hawajali walimu wao kuwalipa ni kwa Shida,chuo kinajua kukusanya ada ila kuzingatia mfumo bora wa elimu hakuna

Mfano Mimi nafundisha chuo flani na ni professional natunga mtihani jinsi inavyotakiwa mwanafunzi akipata alama ya chini mwisho wa siku unakuta mkuu wa chuo kamwongezea alama za juu

Huku ni kuzalisha kizazi cha ovyo katika fani za ufundi VETA mwanza igeni mfano wa wenzenu wa NACTE kwenda kukagua vyuo vilivyopo maeneo yenu sio mnakaa hapo maofisini na kupiga soga,vyuo vingi vya mwanza havina walimu wataalam,wakuu wa chuo hawawajali walimu wao na kuwalipa ni kwa Shida, jitahidi mtembelee kufanya ukaguzi na muongee na wakufunzi

Mkiendelea kukaa ofisini na kunywa chai mjue mtajijengea sifa mbaya kupitia vyuo mlivyowapa usajili.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom