Kuepuka kuonekana kama mmoja alisafiria nyota ya mwenzake ni vema zile taarifa za kila mwezi ziendelee kutolewa bila kujali kushuka ama kupanda kwa idadi
-Taarifa za kuvunja makusanyo ya kodi
-Taarifa za wafanyakazi hewa kwa kila mkoa na kila idara
-Taarifa za waliohakikiwa mpaka sasa
-Kazi zilizo kwisha fanyika at least kwa mwaka huu wa kwanza wa awamu ya tano
Gavana wa benki kuu Prof. Ben Ndullu alitoa takwimu za uchumi kukua kwa kiwango cha 5.5! Huu ni mweleka kwakuwa kipindi cha mwisho wa utawala wa awamu ya nne takwimu zilionyesha kuwa uchumi unakua kwa asilimia 5.7
Kuna kitu cha kutisha zaidi kimeanza kujitokeza, ile tofauti kati ya matajiri na walalahoi tuliyoaminishwa itaondoshwa ni kama imekufa kifo cha asili
Kinachoonekana sasa ni matajiri wale wale waliokumbatiwa na serikali zilizopita ndio hao hao wanazidi kupewa kipaumbele huku walalahoi wakiwekewa vizingiti vya kila aina... Ni kama Mkapa anarudi kimyakimya
Kwasasa zinazotamba ni kampuni nyingi za kigeni kwenye kila sekta huku za walalahoi zikizidi kudhoofika! Na mgeni akilipwa chake hakilali hapa nchini kinapelekwa kwao
Vyovyote iwavyo basi endeleeni tu kutupatia takwimu ili tujue tulikotoka tulipo na tuendako
Hapo umewapendelea ma elite wa uchambuzi tu, je wanaosoma jf kijijini unafikiri wanataka kusikia nini? Million 50 kila kijiji na vijiji vilivyoishanufaika. Matenki ya maji yaliyofunguliwa siku ya mwenge vijijini na hayajatoa maji hadi leo wakati ukame umetamaraki vijijini. Majumuisho ya makusanyo ya wahanga wa tetemeko na walioishapata misaada kutoa wale ambao waipata baada ya mtangazaji wa iTV kuwekwa lupango na kuachiwa.