Vazi la CHADEMA!! Vazi la Ukombozi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vazi la CHADEMA!! Vazi la Ukombozi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELNIN0, Feb 28, 2011.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Vazi la CHADEMA linanivutia sana, limebuniwa vizuri kwa matumizi sahihi hasa kuonyesha ujasiri na upiganaji ili kuikomboa nchi hii, linaonyesha uzalendo na ari ya kuondoa kwa nguvu zote aina za unyonyaji na ufisadi katika nchi yetu.

  Ili chama chochote kikue lazima kiwafikie wananchi wengi na ndiyo hivyo CHADEMA inafanya hivyo kwa sasa, kwa mantiki hiyo na mimi nakuja na wazo langu ili kufanikisha njia mojawapo ya kukiwezesha CHADEMA kuwafikia watu wengi zaidi.

  Mimi nipo ki ujasiliamali zaidi kwamba tuboreshe vazi hili liuzwe sokoni, nina imani ni wengi sana wantakaopenda kulivaa hasa kipindi hiki cha vuguvugu la mabadiliko ili kuonyesha ukeleketwa wetu.

  Napendeleza vazi hili lifanyiwe marekebisho liwe kwenye international standard na liuzwe na CHADEMA kote Tanzania ili kuinua kipato cha CHAMA.

  Designers waangalie quality, fashion ili kuendana na wakati kwa mfano mavazi yawe kwenye rika:-
  a) Kwa watoto chini ya miaka 12
  b) Kwa wasichana na wavulana 13 - 18
  c) Vijana wa kike na kiume kati ya 19 - 35
  d) Watu wazima wake kwa waume 36 na kuendelea.

  Mnaonaje wana CHADEMA? kwa mfano maandamano ya kanda ya ziwa nina uhakika copy zaidi ya 10,000 zingeuzwa na kipato hicho kingetumika moja kwa moja kukitangaza chama vijijini na kufungua matawi zaidi.

  Ni hoja tu ndugu zangu sababu naona CHADEMA ndicho chama kinachoonyesha moyo wa dhati wa kutupatia maendeleo na wananchi wengi mno kwa sasa wanakiunga mkono, sote tunapenda kisonge mbele na kukua kwa haraka lakini kumbukeni bila Fedha kasi ya ukuaji inapungua.
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  VAZI LA CHADEMA NI VAZI LA MBOWE. kwani yeye na mwenzake Ndesa na Mtei ndio wanahisa wakuu wa CHADEMA.

  Poleni sana
   
 3. S

  SeanJR Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli ndugu yangu ww *****!! Huelewi hata unachoandika ''vazi la CHADEMA nivazi Mbowe na Ndesa na Mtei'' ushasema vazi la CHADEMA,kwa uelewa wako finyu unaendelea nivazi la Mbowe ,ndesa na Mtei ,hao wengine wanaovaa huwaoni! Namueshmu sana Mzee wetu Mtei naweza sema muasisi na mpambanaji wa ukweli,hababaishi! Vazi la ukombozi la wanaCDM wala c la mtu mmoja ndo maana wanalivaa akina Tundulisu,Mbowe,Ndesa,Dr.(wa ukweli) Slaa,na wanaharakati kbao! Ww utaishia apo tu,badilika! eeh, kalagabaho..
   
 4. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kizuri zaidi linaendana na hali hii ya mgao si lazima ulipige pasi CDM waliona mbali sana.
   
Loading...