eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,235
- 16,205
Vatican ni dola mji
Hivyo ni nchi ndogo duniani kuliko zote
Ni nchi ya papa ambae ni askofu wa roma na mkuu wa kanisa katoliki duniani
Iko ndani ya jiji la roma upande wa mangaribi
Jina limetokana na mlima vatikan au mons vaticanus
Pamoja na basilika la mt. Petro ambalo ndilo kanisa kubwa kuliko yote duniani
Vatikani ina makanisa mengine 7
Vatikani pia ina makumbusho ya sanaa kubwa ya hazina kiasi kwamba inahesabiwa na UNESCO kua ni urithi wa dunia tangu mwaka 1984
Mji wa vatican ni mabaki ya dola la papa lililotawala sehemu kubwa ya italia ya kati kwa karne nyingi hadi mwaka 1870
Tangu mwaka wa 1860 baadhi ya maeneo hayo yalitawaliwa na ufalme mpya wa italia uliolenga kuunganisha sehemu zote za peninsula ya italia
Utawala wa papa juu ya mji na mkoa wa roma ulilindwa na ufaransa hadi mwaka 1870
Vita ya mwaka 1870 kati ya ujerumani na ufaransa kuliifanya ufaransa kuondoa jeshi lake roma hivyo mji huo kutekwa na jeshi la italy tarehe 20/9/1870
Wakati huo serikali ya italia ilitaka kumuachia papa pius sehemu ya mji wa roma lakini papa pius alikataa akitumaini wakatoliki wa italia na sehemu nyingine duniani watalazimisha serikali ya italy kumrudishia mji wote wa roma
Kwa hali hiyo mapapa walijifungia ndani ya jumba la vatikani kwa miaka 57 bila kutoka
Mwaka 1929 serikali ya benito musolini ilitafuta amani na papa pius aliekua tayar kwa makubaliano
Hivyo vatikani kua nchi huru kuanzia wakati huo
Mji mkuu- vatican
Wimbo wa taifa- ino e marcia pontificale
Katbu wa dola - pietro parolini
Vatican ina uhusiano za kibalozi na nchi 180 duniani kupitia ikulu ya vatikani
Vatican ina posta pia ikitoa stempu na hata sarafu za euro
Vaticani ina jeshi dogo kabisa duniani lakini lenye historia ndefu kabisa duniani
Ni kikosi cha walinzi waswisi ambacho kipo tangu mwaka 1, 506 na kina wanajeshi 100 tu
Wote ni wakatoliki raia wa uswisi kwa kuzaliwa
Je unaielewa vipi vaticani
Karibu kwa kuongezea zaidi ili wengine waelewe