Van Dame(Sinza), Yesu (Mbeya) kati ya Wababe waliowahi tikisa Tanzania

Kalapina aliishia kuwa mbabe wa wasanii tu. Kamwe asingeweza kugusa himaya ya wababe halisi. Yeye alikua mbabe wa akina Juma nature, Mwana FA na wengineo
Hahahaha ,hata huko alikua anaforce u ,namjua toka enzi za ' Indiana police' maskan ,nyuma ya makumbusho school
 
Kweli hiyo miaka ya zamani..hivi kweli kipindi hiki unaweza mfanyia ubabe mtu kweli??Kwanza nahisi watu wengi wamestaarabika...
 
Ww Mbeya nyamaza,hujawakuta kina Jombi,Kina Ambangisye "El Kibo"Chanda, Jared,Simion ama Semeni,Frank kulikua na timu pale nzovwe tu inatosha kutawala Mbeya nzima. Hujaja mabatini,majengo,mwanjelwa,hao kina yesu na shetani wakikutana na hizi jamaa wanaomba wenyewe likizo bila malipo.
Halafu kuna jamaa alikua na mashetani nimemsahau,siku hiyo akilivuta bangi lake yakapanda basi anachomoka na panga,mtaa mzima mnatafutana ni mbio tu.
Ajabu hajawai kumkata nalo mtu.😂😂😂
 
damme nakumbuka alikuwa anaagiza watoto wa shule chipsi na hawapi pesa na anawaambia mwambie akupeni na chenji mwambie damme kanituma na ukienda kwenye kibanda cha chipsi ukitoa tu hayo maelekezo huyo muuza chipsi hana jinsi lazima atoe chipsi na chenji ndio ilikuwa ponea yake japo hajapewa hata mia!
 
Miaka ya kuanzia 2004 au 2005 km sikosei nikiwa primary alitokea jamaa mmoja maarufu Mbeya aliitwa zebedayo huyu jamaa alikuwa ni balaa kwenye kufukuza upepo achana na ubabe wa kupigana

Kuna mbwa aliiba samaki kwake bwana huyu alimfukuza mbwa yule na hakutaka kumkamata ni swala la kwenda nae sambamba tu. Mbwa yule alikufa kwa kukosa pumzi ligi ilikuwa kubwa

Bwana huyu pia alishawahi kukimbia kutoka town mpaka tukuyu kwenye msiba na wale walipanda magari kutoka town walishangaa kumkuta zebedayo ameshafika eneo la msiba na gari hakupanda
Kaka hapa umetulisha matango pori 😂😂😂😂
 
Umenikumbusha mbali sana enzi hizo mbeya. Umemsau mwasimba wa nonde. Alikuwepo mwakayugu kipindi hicho stand ya chunya ilikuwa chini hapo karibu na rift Varey hotel. Kipindi hicho dhahabu inatema mbaya chunya,wasukuma walikuwa wanapolwa balaaaa pale stand na akina mwakayugu. Alikuwa anawapora milioni 20,50 kipindi hicho au dhahabu za kiwango hicho ilikuwa kitu cha kawaida. Alikuwa anachomeka nato refu kuanzia kuanzia kwenye buti lake refu,kuja juu kwenye ka-jeans kake ka kubana. Siku moja ilikuwa inapigwa gemu (kamali)kule nyuma mtoni sinde. Mwakayugu akaliwa hela yote,mpaka buti,nguo,akabakiwa na chupi tu. Sasa kulikuwa na mtindo wa aliye-win siku hiyo anawapa arifu aliowala,hiyo arifu ilikuwa kama nauli ya kwendea home. Sasa mwakayugu alipewa arifu ya kwanza akaliwa nayo. Jamaa alie win siku hiyo akamwambia kula mjusi yule nitakupa arifu nyingine. Duuh...! Lile lijamaa mwakayugu lilikuwa kama mnyama hivi. Likaurukia ule mjusi na kuukata na meno,likaanza kuutafuna mjusi bwana. Basi pale karibu wote tulistuka tukataka kukimbia,yule jamaa aliemwambia ale mjusi,akamwambia acha acha acha,chukua hela arifu hii hapa. Aaah...! Wapi jamaa likaendelea tu kuutafuna ule mjusi,likaumaliza. Likainama chini mtoni pale likachota maji na viganja vyake likanywa maji,likachota likanywa,hapo limeliwa kila kitu mpaka nato(kisu kikubwa) lake limebakiwa na njupi tu. Jamaa lilikuwa hatari balaa. Lilipanda juu hivi,bingwa lililojizira zira hivi,likimya,linaongea kwa vitendo tu. Nasikia liko south Africa now
Hahahaha we jamaa sio kwa usimuliaji huu we ni Comedian nn? 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 dah hizi story zinachekesha sana.....Huyo jamaa hafai 😁😁
 
Kwetu Ilala tulikuwa na Maksudi Mbwaa mechi za FC Boom na Ashanti United ilikuwa noma uwanja wa Karume. R I P Kaka Mkubwa Maksudi Mbwaa...
 
Mnyama alikuwa anaenda kawetere mara tatu kwa siku kubeba mabanzi....wakati watu wengine wakienda saa kumi na mbili wanarudi jion saa kumi
Mkuu mfugale naona wengi wanaona eti ni chai hiii bila shaka mbeya wew ni mwenyeji waambie zebedayo is real bila shaka utakuwa mtu wa ilemi, ilolo, isanga ya kati na mitaa ya karibu hapo....
 
Uzi murua sana huu, ila binafsi Shuleni kwetu hakuna aliyeniweza, kuanzia darasa la 1 mpaka la 7. Miaka ya 1985 huko, ngumi ilikuwa jiwe kweli.
 
Yaani nimecheka Sana Hadi machozi

Kuna vituko jamaniii

Hakushiriki mashindano ya olimpic?? Kumbe nasi tunao wenye vipaji ila hatujawatafuta.
Kuna watu hawaamini hii kitu jaribu kwenda ilemi darajani pale au ilolo utapewa story ya huyu jamaa
 
Kuna mwaka mmoja dar walikusanywa wababe na mabaunsa wengi ili Waende kuwahamisha watu wanaosemekana wamevamia kwenye eneo la mtu Mmoja na kujenga na kufanya makazi
Kilicho wakuta wababe hao wengi wao walipoteza maisha wengine hadi leo wamepatwa na vilema
Huko walikutana na nguvu ya raia waliyokuwa na mishale,mapanga etc

Ova
 
Mwanzinga namfahamu alikua kiboko na matukio ya hatari utadhani sio binadamu wale jamaa walikua wanaiba hawadhuru watu wao ni kuiba tuu bila nondo wala panga...
Kulikuwa na mbabe mwingine anaitwa "KAMBASON" wa Meta MBEYA. A. K. A. pengo miaka ya 1990s Sijajua Yuko wapi siku hizi.
 
Back
Top Bottom