Van Dame(Sinza), Yesu (Mbeya) kati ya Wababe waliowahi tikisa Tanzania

Wababe wa Arusha
Saba Sita (Alikuwa ni ndata)
Somba
Idd Nkurlu
King Kola(Mpiga vichwa)
Babaa
Papaa(Alikufa akiwa anamkimbiza aliyemchoma kisu)
Fred Gebby

Makundi ya wababe
SUA SIDE
NAKO 2 NAKO
FIRE

Hapo sijawataja watumia pipe(Bastola)
bou nako naye amewahi kusumbua??vipi fido vato?
 
enzi zetu kijana bila "kupiga chuma" ilikuwa ni ngumu sana ku-survive mtaani. ilikuwa ni lazima uwe na mwili mkakamavu uliojazia ili uweze kumuogopesha mtu kabla hajakuchokoza.

vijana wa kizazi hiki cha social media wanaenda gym ili wawe na miili ya kuwavutia wasichana kimapenzi.
mzee wewe ulikuwa unapiga gym?
 
mkoani kwetu kuna jamaa aliitwa kinjikitili ngware jamaa alikua noma wajeruman walijua kama mfalme wa maji
 
😂😂😄😄 huyu zebedayo ni nouma kuliko wote!

Miaka ya kuanzia 2004 au 2005 km sikosei nikiwa primary alitokea jamaa mmoja maarufu Mbeya aliitwa zebedayo huyu jamaa alikuwa ni balaa kwenye kufukuza upepo achana na ubabe wa kupigana
Kuna mbwa aliiba samaki kwake bwana huyu alimfukuza mbwa yule na hakutaka kumkamata ni swala la kwenda nae sambamba tu. Mbwa yule alikufa kwa kukosa pumzi ligi ilikuwa kubwa
Bwana huyu pia alishawahi kukimbia kutoka town mpaka tukuyu kwenye msiba na wale walipanda magari kutoka town walishangaa kumkuta zebedayo ameshafika eneo la msiba na gari hakupanda
 
Ayubu Van Damme amepitia visa vingi sana maisha yake so unachokisikia kibaya cha hovyo jua ni kweli... yule alishapewa pambano na Askari makaburini alipigwa for the first time akienda chini akainuka akatengeneza stamina so yule Askari akawa anampiga Damme haendi chini anapangua na alipoanza kupiga yeye Askari alianguka chini na polisi wengine wakamchangia kwa vitako vya bunduki akatulia akatiwa pingu lumande.. kesi zilizomaliza baada ya kuchomekewa silaha baada ya kuiba akatiwa ndani muda mrefu sijui walimpiga sindano za kupunguza nguvu aliopotoka akawa sio yule but hakuacha kuiba akasekwa tena babake akafa aliyekuwa akimtetea nyumba yao ikauzwa mamake alihamia mwana nyamala alipotoka akahamia huko kwa maza ake akaendeleza ukabaji.

Tatizo anakupa ukimtizama tu kosa anakupa na kukusachi na watu huwa wanamtizama lilivyo na mimacho yake mibaya anawaumiza sana... anavisa zaidi ya milioni
Van damme jina lake ni ayoub mkobo
 
Dame wa sinza ukuta wa posta, aka mawasikiano, ukikutana nae anakwambia leta simu hyo unatoa bila kupenda,
Ila nishawahi kumchakaza kumtapisha maukoko boya yule
 
Mbona abdallah kuveta hamjamuweka huyu bwana habari zake zinahitaji jamvi.. Mburahati moja hiyo
 
Miaka ya kuanzia 2004 au 2005 km sikosei nikiwa primary alitokea jamaa mmoja maarufu Mbeya aliitwa zebedayo huyu jamaa alikuwa ni balaa kwenye kufukuza upepo achana na ubabe wa kupigana

Kuna mbwa aliiba samaki kwake bwana huyu alimfukuza mbwa yule na hakutaka kumkamata ni swala la kwenda nae sambamba tu. Mbwa yule alikufa kwa kukosa pumzi ligi ilikuwa kubwa

Bwana huyu pia alishawahi kukimbia kutoka town mpaka tukuyu kwenye msiba na wale walipanda magari kutoka town walishangaa kumkuta zebedayo ameshafika eneo la msiba na gari hakupanda
We jamaa nishushe kwenye Tuta please
 
Back
Top Bottom