Ilumine
Senior Member
- Dec 27, 2008
- 196
- 4
Leo hii, nilikuwa nikifuatilia hotuba ya Daktari wa kweli Slaa, live TBC1.
Nilishtushwa na zile data alizozitoa, anasema zilisomwa mbele ya JK katika mojawapo ya ziara zake. Milioni mia saba zilitumika kujenga matundu manne ya vyoo katika shule moja! Tunaelekea wapi watanzania?
Jamani, ufisadi Tanzania umekithiri, hivi tunaibiwa fedha zetu namna hii!
Wageni wawekezaji wanajivunia madini bila jasho, wanatuachia mashimo na kemikali chafu, wazawa mafisadi ndio wanafuja mali zetu namna hii! Inaniuma sana.
Basi jamani, inatosha, tuwang'oe sasa mafisadi hawa, ili kidogo tulichonacho kitumike kwa manufaa ya wote. Nawasilisha!