MATUNDU YA CHOO BAGAMOYO: CAG ataka madai ya Dr. Slaa yafanyiwe kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MATUNDU YA CHOO BAGAMOYO: CAG ataka madai ya Dr. Slaa yafanyiwe kazi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 28, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ILIKUWA KAMA SINEMA NDANI YA TBC 1 Walipomuhoji CAG Bw Utouh juu ya madai ya Dr. Slaa kuwa Wilaya ya Bagamoyo ilitumia shs Milioni 700 kwa matundu manne ya choo. Jumla kwa vyoo vyote ni Bilioni 3.
  Mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali alihojiwa na TBC1 kuhusiana na tuhuma hizo na katika hali ya kushangaza alikiri kuwa ni kweli na kuwa hatua za kisheria zinaandaliwa.
  Madai ya Dr. Slaa yalikuwa yameripotiwa na mwananchi kama ilivyo hapa Chini.


  Dk Slaa, Marando wamwaga sumu Dar
  Tuesday, 26 October 2010 21:27 By Gazeti la Mwananchi


  Dk Slaa akiwa katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam kwenye harakati zake za mwisho za kunadi sera za chama chake

  Waandishi Wetu
  DK WILLIBROD Slaa na mwanasheria wa Chadema, Mabere Marando jana walirusha makombora mazito kwa CCM na mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete katika mkutano wa mwisho wa mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya chama hicho cha upinzani jijini Dar es salaam.

  Dk Slaa, ambaye atahitimisha kampeni zake mkoani Mbeya keshokutwa, aliwaambia maelfu ya wafuasi na mashabiki wa Chadema waliofurika kwenye viwanja vya Mwembeyanga kuwa atalazimika kupiga kura kwenye jimbo lake la Karatu kwa kuwa ndiko alikojiandikisha kwa shughuli hiyo.

  Wakizungumza kwenye mikutano ya hadhara mjini Bagamoyo, Gongo la Mboto, Vingunguti na Mwembeyanga jijini Dar es Salaam, Dk Slaa na Marando Kikwete, CCM na wagombea wengine watapata shida Oktoba 31 kutokana na kutowaonea huruma Watanzania.

  Akihutubia umati wa watu waliofurika kwenye mkutano wa kampeni kwenye mji mkongwe wa Bagamoyo, Dk Slaa alimshangaa Kikwete akidai kuwa hana huruma na umaskini wa watu wa nyumbani kwao, akidai kuwa alipiga makofi kushangilia wakati akisomewa taarifa ya matumizi ya zaidi ya Sh3.2 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa matundu manne ya vyoo vya shule za kata tano.

  Dk Slaa alisema kama Kikwete anafurahia uchafu wa ufisadi, basi bila shaka hata ule ufisadi wa mabilioni ya fedha yanayotokea ngazi ya taifa huwa anafahamu na anafumbia macho.

  Katika mkutano wa Mazese, Dk Slaa alisema serikali yake itahakikisha inarudisha fedha zote zilizochukuliwa kifisadi na kuwekwa kwenye akaunti za nje ili zirudi kusomesha bure watoto na nyingine zitumike katika kuboresha maisha ya Watanzania waliokata tamaa.

  "Nasema mimi sina utani na maisha ya Watanzania wote. Nikiingia Ikulu, lazima nitawakaba koo wale mafisadi wote waliojichotea fedha za umma na kuziweka kwenye akaunti za nje ili ziongeze kwenye idadi ya fedha za kusomesha bure watoto na nyingine ziingie kwenye huduma za jamii," alisema Dk Slaa.

  Katibu huyo wa Chadema pia alirejea ahadi yake ya kupunguza bei ya simenti hadi Sh5,000 na vifaa vya ujenzi akisema hilo linawezekana kwa kuwa amepania kuwawezesha Watanzania waishi kwenye nyumba bora.

  Akiwa Mwembechai ambako aliweka historia kwa kutangaza orodha ya watu aliowatuhumu kuwa ni mafisadi Novemba 15 mwaka 2007, Dk Slaa alitamba kuwa hadi sasa bado yuko huru licha ya Kikwete kusema angemfikisha mahakamani kwa kutaja orodha hiyo.

  Dk Slaa, aliyemaliza mkutano wake wa kampeni saa 12:05, alisema Chadema imeifanya Novemba 15 ya kila mwaka kuwa siku ya kumbukumbu ya mafisadi, ikiwa ni njia mojawapo ya kukumbuka kuibuliwa kwa kashfa tofauti ambazo ni pamoja na wizi wa fedha za EPA, ununuzi wa rada, ndege ya rais na sakata la makampuni ya uchimbaji madini.

  Mgombea huyo wa urais, ambaye alielezea kitendo cha magari ya abiria kupisha msafara wake wakati akielekea kwenye mkutano huo kuwa kinaonyesha anakubalika kwa kila hali, aliwaahidi wananchi hao kuwa atakigeuza Chuo cha Sanaa cha Bagamoyo kuwa Chuo Kikuu cha Michezo na kukipandisha hadhi chuo cha Malya.

  Alisema kuwa inashangaza kuona kuwa masuala la mpira yanahusu klabu mbili tu za Simba na Yanga na kwamba chuo hicho cha michezo kitafundisha walimu ili makocha wa michezo wazalishwe ndani ya nchi na kuibua vipaji vingi.

  Mbunge huyo wa zamani wa Karatu aliwakumbusha wananchi kutokubali kuingia kwenye mtego wa kupandishwa hasira wakati wa uchaguzi akiwashauri kuwa watakapochokozwa, wawapuuze wachokozi kwa kuwa hiyo ni njia kuu ya kumpuuza mtu.

  Lakini alisema CCM ndio inayoweza kusababisha vurugu kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwa sababu ni chama cha kigaidi ambacho kimeunda kambi ya kuwafundisha vijana wao mbinu za kupigana.

  Dk Slaa aliwataka wananchi kulinda kura zao kwa utulivu bila kufanya vurugu za aina yoyote na kwamba kila mwananchi ana wajibu wa kulinda kura yake isipotee na isichachuliwe na CCM.

  Akizungumza katika jimbo la Segerea Dk Slaa alimsafisha mgombea ubunge wa jimbo hilo, Fred Mpendazoe kuwa alikuwa mbunge namba moja wa CCM kukemea na kupiga vita ufisadi na kudai kuwa mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango ni mnafiki.

  Naye Marando, ambaye alirusha tuhuma nzito dhidi ya viongozi wakuu wa CCM na makada wake wakati Chadema ilipozindua kampeni zake jijini Dar es salaam zaudu ya miezi miwili iliyopita, jana alisdema kuwa Kikwete atahukumiwa na Mungu kutokana na kitendo cha kuwaachia huru watuhumiwa wa ufisadi kwenye kashfa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

  Alikuwa akizungumzia kashfa ya wizi wa fedha hizo uliofanyika kati ya mwaka 2005/06 kwenye Benki Kuu ya Tanzania. Hadi sasa zaidi ya watu 20 wameshashtakiwa kwa kuhusika kwenye wizi huo, lakini rais alitoa ahueni ya kutowapandisha kizimbani watu ambao waliitikia wito wa kuzirejesha fedha hizo kabla ya Novemba mosi.

  Marando alisema kuwa kitendo hicho ni sawa na kuunga mkono ufisadi na kuwageuka wananchi na kwamba CCM imewatetea wanachama wake kwa ajili ya kuficha madhambi yao, jambo ambalo linawafanya wananchi wa hali ya chini kuishi katika mazingira magumu ya maisha.

  "CCM inawatetea wanachama wake kwa madai kuwa hawajafanya kosa kwenye kashfa ya EPA; Mungu atamuhukumu Kikwete kutokana na vitendo hivyo kwa sababu yeye ndio mwenye jukumu la kuwahukumu wananchi hao,"alisema Marando.

  Alisema ili kutatua tatizo wananchi wanapaswa kufanya maamuzi ya mwisho kwa kumpigia kura Dk Slaa, ambaye anawania kuongoza serikali ya awamu ya tano.

  Alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa wabunge wanafanya kazi ya ubunge na mawaziri wanafanya kazi ya uwaziri ili mambo yaweze kwenda sawa.

  Alifafanua kuwa ahadi zote za barabara, maji na umeme alizotoa Kikwete zitatekelezeka kutokana na kodi za wananchi wenyewena kuwataka kusimamia utekelekeza wa ahadi hizo.

  Naye katibu Mwenezi wa Chadema, Jimbo la Ukonga, Ernest Njooka jana ametoa mpya baada ya kumpigia debe mgombea udiwani Kata ya Gongolamboto kwa tiketi ya CUF, Bakari Shingo ili wananchi waweze kumchagua.
  Mgombea huyo alitoa kauli hiyo jana kwenye viwanja vya Kampala, maeneo ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam muda mfupi kabla ya Dk Slaa kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye viwanja hivyo.

  “Katika kata hii ya Gongolamboto tumeamua kumnadi mgombea wa CUF kupitia mkutano huu kwa kuwa anakubalika na wananchi, ndio maana hatukuwa na sababu ya kumsimamisha mgombea wa Chadema... kura zote kwa kata hii kupitia udiwani mpigieni Shingo,” alisema Njooka.

  Imeandaliwa na Patricia Kimelemeta, Hussein Issa, Pamela Chilongola na Musa Mkama.
   
 2. v

  vickitah Senior Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 18, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pamoja sana, mafisadi lazima waondoke ths tym'
   
 3. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uzuri ni kuwa kila tuhuma aliyoitowa dr. Slaa imekuwa ikithibitishwa. Je hili nalo ccm watasemaje kama mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali anasema ni kweli?
   
 4. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Thanks for the info Sir. We are working on it.
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  pesa imeenda kwenye kampeni za ccm hizo
   
 6. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Je ccm sio vizuri kesho wakati wa mdahalo wakajibu tuhuma hizi? Kwa nini rais ashangilie wizi nyumbani kwake?
   
 7. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  INAWEZEKANA Kweli Kuwa zimeenda kwenye kampeni?
   
 8. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  can we know if it will be before sunday?
   
 9. M

  MULANGIRA Member

  #9
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa hakurupuki na analolisema ni la kweli lakini CCM hawana hata aibu watatea hilo. Na kama mnavyosema hizo pesa ni Kagoda nyingine ni kati ya pesa zinazotumiwa na CCM kuendesha uchaguzi. Inabidid tusambaze ujumbe kuwa CAG kathibitisha madai ya Dr. Slaa kwa njia ya simu.
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du yaani unajua mimi nilikuwa kiasi flani siamini amini, kweli JK na serikali yake ni wabadhirifu na hawana hata chembe ya huruma kwa masikini watanzania!
   
 11. M

  MULANGIRA Member

  #11
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 12. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na sasa hivi utandawazi ungiingia hawa wazee wa CCM watakuwa wanashangazwa kila siku maana document ni soft copy huitaji kubeba gazeti
   
 13. h

  hebronipyana JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakila tuhuma iliyotolewa ilikanwa au ilitafutiwa maelezo ambayo jumla yake ililkuwa ukanushaji,na baadae ilikuja aibu.
   
 14. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TBC1 inawezekana walikuwa na nia ya kummaliza Slaa kuwa ni mropokaji na muongo Kibao kikageuka. CAG Mh. Utouh aliprove huku kamera za TBC1 zikimuonyesha akijibu kwa uhakika mkubwa na kusema kuwa hatua za kisheria zinaandaliwa. Hii ni taarifa ya habari ya usiku wa 28 October, Labda watamkemea CAG.
   
 15. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kikwete ataifilisi Tanzania. Muda si mrefu, tutakuwa kama Zimbabwe
   
 16. R

  Rugemeleza Verified User

  #16
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli kama ni hivi ni bora tuiondoe CCM madarakani. Watanzania saa ya ukombozi ni sasa!
   
 17. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  CCM shall be sacked this sunday...........that is pathetic! Enough is enough.
   
 18. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nawasiwasi kama Kikwete aliwafikisha Mahakamani akina Basil Mraba na hakujifunza kwa matendo yake basi yeye anaweza kunyongwa baada ya uongozi wake kuisha. Mungu aibariki Tanzania ili iondokane na maisha haya ya ufisadi
   
 19. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahaha.... wanachadema wa JF mmenifurahisha kidogo... ngoja niwahi kwenye kikao, lala salama hii, nitawaletea salamu nzito za ushindi WA KISHINDO baada ya j2.

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
   
 20. M

  MULANGIRA Member

  #20
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu umepigwa ganzi kwako wewe yote afanyayo Kikwete na mafisadi wake yote ni sawa. Huna uchungu na pesa za nchi.
   
Loading...