Doria Mtandaoni
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 362
- 752
Moja ya sifa ya tishio la ugaidi ni kuzuia shughuli kuacha kufanyika.
Iwe kwenda sokoni, kanisani, kwenye biashara ama kukusanyika kwa namna yeyote ile.
Kinachotokea sasa kuhusu maandamano na nchi yote hasa miji mikubwa raia kujifungia ndani na kuacha migambo, polisi, wanajeshi na askari wengine inaleta taswira ya namna gani hofu ya maandamano kuwa kama ni matukio ya kigaidi.
Sijui raia wataishi hivi hadi lini, lakini inaletamashaka na wasiwasi mkubwa wa mstakabali wa amani.
Amani inajilinda yenyewe, haiihitaji kushikiwa mitutu ya bunduki. Umewaza ikifikia hatua watu kujitoa mhanga hali itakuwaje kwenye taifa la watu wazembe wazembe.
Mamlaka zinawajibu wa kujipima na kutenda mambk yatakayoendelea kiurudishia hii nchi utulivu usio na shuruti.
Vinginevyo, wao na sisi tutabakia mateka ndani ya nchi kwa uzushi wa maandamano na kauthiri shughuli za uchumi.
Amani ni tunda la haki. Haki ni tunda la utawala bora. Utawala bora ni zao la demkrasia, na demokrasia zao la utashi wa wananchi kuwachagua viongozi wao.