Uzuri wa mwanamke upo wapi? Ni upi?

Uzuri wa mwanamke upo wapi? Ni upi?

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
2,855
Reaction score
405
Ndugu zangu, wapenzi wa jukwaa hili,

Leo naleta hoja nzito kidogo. Najua baadhi ya akina dada watakwazika. Kwa hiyo, naomba mnisamehe.

Siku hizi limezuka wimbi la akina dada na hata akina mama kujilemba kwa namna mbalimbali kuanzia rangi ya mwili, nywele, kucha, midomo na wengine wamefikia hatua ya kunywa au kupaka dawa za kichina za kuongeza makalio na maziwa. Wengine wanasuka nywele ndefu na wanaongea kwa mbwembwe huku wanatikisa vichwa vyao na kushikashika nywele kama wafanyavyo wanawake wa kizungu. Wengine wamefikia hatua ya kubadili hata sauti na namna ya kuongea!!

Najua dada zetu wanafanya hivyo kwa lengo la kupendeza na wengine lengo lao ni kuwavutia wanaume. Lakini mimi binafsi sijui ni nini kimenitokea! Inawezekana ndiyo abnomality hiyo. Kadri mwanamke anavyojilemba zaidi ndivyo hamu ya kufanya nae mapenzi inavyopungua.

Ukweli ni kwamba nikilala na mwanamke ambaye ni natural yaani mwenye nywele za kawaida anayesuka mtindo wa 'twende kilioni' au amezibana tu, wowowo, chuchu na sauti natural huwa napata nguvu nyingi za kupanda mlima ikilinganishwa na ninapolala na mwanamke mwenye kucha za bandia, nywele za bandia, na midomo iliyopakwa rangi nyingi.

Sijui ni ugonjwa au ni jambo ambalo hata wanaume wenzangu huwa linawakumba?

Tafadhali karibuni kwa mawazo.
 
Mtoa mada naomba nikuambie tuu kujiremba kwetu sio tunataka wakaka wavutiwe nasi bali ni mwenywe kuwa huru na mwili wako, kama kuna sehemu ya mwili huipendi unaifanyia marekebisho kama pesa ipo..
kumbuka kila mtu anapenda awe na id yake lol
 
Wanawake ni maua ya dunia ni lazima wajibidiishe kwa kutafuta njia nyingi za kumfanya apendeze ampite mwenzie na wanawake wamesemwa kwenye vitabu vya dini niwatu wakukaa ndani nakioo nakujiremba!!Mimi napenda mwanamke wakujiremba kapakaa marembo ya na mwili miguu i like it!Wana wake ni Zum zum nyuki lia wee...Maua mazuri yapendeza ukiyatazama unafurahia..........................>>>>>>>>>
 
Mimi napenda NATURAL. Hata upande wa kitoweo cha kuku, huwa napenda wa kienyeji. Labda ndiyo maana nguvu zangu haziwajawahi kutetereka. Nikiona mawigi na makucha ya ajabu ajabu huwa vinani-put-off completely.
 
cwakubali wanaojremba thana,napenda k2 nachural,wadhungu wamewaharibu dada zetu kuchukia kpilipili na kuona wigi ndio zuri
 
Mimi napenda NATURAL. Hata upande wa kitoweo cha kuku, huwa napenda wa kienyeji. Labda ndiyo maana nguvu zangu haziwajawahi kutetereka. Nikiona mawigi na makucha ya ajabu ajabu huwa vinani-put-off completely.

Kweli naona umepata jogoo mkubwa mnalingana na umemfunga kamba kama Ng'ombe
 
Yaani mie huwa najisikia kutapika nikinusa harufa ya nywele zilizopakwa yale madawa. Hata kama mnaenda ku - do ile harufu inamshusha jogoo kabisa. Pia niliwahi kusikia eti wakipaka hayo madawa maji hayaruhusiwi kugusa kichwani sasa si uchafu huo huenda ndo unasababisha ile harufu kaaaliiii kama nanihiiiiiii vile
 
Embu acheni watu wajirembe!Starehe yao sio lazima iwe yenu!
 
Kwangu mimi ni vyote vyote naona sawa,lakini sio kujiremba vile too much anapika milangi kama kapakaa makaa,ila vyote ni sawa tu.....
 
mimi ni mwanamke lakini ukweli,kuna urembo mwingine ni uchafu na mateso.....mtu unaweka wigi wiki nzima husafishi hadi linanuka.mba na magonjwa ya ngozi hayakuishi,kila siku we kuweka mafuta na kupulizia spray,wazungu wenzao wana osha daily or three times a week
na wengine mikucha wanaweka migundi kucha zinaharibika kabisa na wakati mwingine zinamnyima kufanya baaadhi ya shughuli,unafuga kucha ndefu mara nyingine mi-bakteria tu ......tuwe na kiasi, si issue ya hela,healthwise na comfortability iwepo pia.....

mimi napenda mtu awe natural.......kujiremba kuwe minimal sana.....usiwe kama unamkosoa Mungu kwa kutaka kuongeza kila kitu hadi unaonekana hujiamini au unalazimisha jambo!!! :hand::hand:
 
mimi ni mwanamke lakini ukweli,kuna urembo mwingine ni uchafu na mateso.....mtu unaweka wigi wiki nzima husafishi hadi linanuka.mba na magonjwa ya ngozi hayakuishi,kila siku we kuweka mafuta na kupulizia spray,wazungu wenzao wana osha daily or three times a week
na wengine mikucha wanaweka migundi kucha zinaharibika kabisa na wakati mwingine zinamnyima kufanya baaadhi ya shughuli,unafuga kucha ndefu mara nyingine mi-bakteria tu ......tuwe na kiasi, si issue ya hela,healthwise na comfortability iwepo pia.....

mimi napenda mtu awe natural.......kujiremba kuwe minimal sana.....usiwe kama unamkosoa Mungu kwa kutaka kuongeza kila kitu hadi unaonekana hujiamini au unalazimisha jambo!!! :hand::hand:

Aisi unafikili tumesychronise our brain. Ni uchafu, uchafu. ............., Halfu utakuta mwingine kuambika vizuri, sura safi, halafu bado anataka kujichafua na maurembo. Nafikili wanaume ni wavumiivu sana.

Halfu nani kakwambia pua za wanaume hazifanyi kazi, tunausa na tunakereka ila basi tuu wavumilivu.
 
teh teh.............uzuri na uaharamu unaanzia ndani mwa mtu. Unafikiri nini kuhusu Mungu, wewe mwenye na binadamu mwenzako. Ukiwa na kasoro kwenye fikra utakimbilia kulipizia kwenye kurekebisha mwili (ngozi, nywele, makalio,.....).

Utamwona mrembo siku ya kwanza bata kama hana busara, hekima, hofu ya Mungu ............rahisi kumchoka mapema. Let us think outside the box.
 
Mimi napenda NATURAL. Hata upande wa kitoweo cha kuku, huwa napenda wa kienyeji. Labda ndiyo maana nguvu zangu haziwajawahi kutetereka. Nikiona mawigi na makucha ya ajabu ajabu huwa vinani-put-off completely.

Mkuu nakuunga mkono kwa hiyo thred. Mi ilinigharimu nikaachwa ila nilisimamia maamuzi yangu na nikampata aliyenielewa na sasa Tunataka kwenda kutambulishana ili iwe wazi. NATURAL INAVUTIA BWANA. Halafu Mdada akiwa Natural anaonekana Kabinti muda mrefu mi ni Shahidi kuna mama ana miaka 50 ukimwona unaweza sema ama 38 - 45 hivi ila alisema siri ni kutoweka ARTICIAL Cosmetics na ana Elimu sababu dada zetu wanasema eti wasiofanya hivyo hawana shule kichwani.
 
marashi ni artificial. marashi pia ni sehemu ya uzuri. marashi huleta mvuto sana hasa mwenye kujipulizia akiwa kayapatia. Hasa akiwa mwanamke
 
heheheheheh aluuu!
One man's meat is another man's fish..sorry poison.
Mtoa mada, we komaa na kuku wa kienyeji tu maana ndio saizi yako.Hao wengine huwawezi.

Baada ya utangulizi ngoja sasa tuwekane sawa:

1. Urembo kwa mwanamke inategemea naye anaelewa nini kuhusu urembo.Wengine hawana aah wala beeh kuhusu urembo na ndio maana hujikandika vipodozi na kukaa na minywele miezi bila kuosha! Nywele za bandia za kushonea za quality nzuri zenye kuoesheka mara kwa mara kama nywele asili ni bei mbaya.Kuna wenye kupenda urembo lakini mambo ya fedha yanagomba.

2. Urembo unaendana na mtu na kwa kipimo, kutegemeana na mtu mahali alipo, au anapokwenda,kazi afanyayo nk.Kazi kwenu kina baba/kaka kuwapa wake/marafiki wenu wa kike support kifedha na ushauri ili waendane na mnavyotaka au kutamani.Huwezi kulalamika tu bila kutafuta suluhu.

3.Wanaume kwa kiasi kikubwa mnawasukuma wanawake kwenda mbali na hata kufanya mambo yenye kuwaletea madhara ili mradi tu mfurahie. Hebu acheni kukimbizia wanawake warembo muone kama wanawake watahangaika hivyo.Mwanaume mwenye mwanamke "natural" hufurahia kupunguza matumizi nyumbani lakini huhangaika sana kuipendezesha nyumba ndogo, Mwisho wa siku mwanamke asilia nyumbani hulaumiwa kwa kujiachia! Mnadhani wanawake wanafurahia kuketi masaa 6 kusukwa au kufanyiwa waxing na mambo mengine yenye kuleta maumivu ya kutisha? ACHENI HIZO WANAUME!
 
Back
Top Bottom